Story: Side Chic & Main Chic ~ A Forever Battle

Wewe mtu sikuweziiii kabisaa dah
 
CHAPTER 5

K...FRIENDA AND FAMILY

Baada ya harusi ya Kelis, Fish akatonywaaa kuwa sande alionekana kwenye harusi na mke mdogo Khadijaa,
Amina akiwa mkono wa kuume wa Fish akaona hapa sasa haitoshi akasubiri mpaka Fish ameondoka akajifanya ameenda bustanini kutembea akachomoa simu iliokuwa kwenye maziwa yake kwa chini, si unajua tena vitochi vyetu vya nokia, akampandia hewani Tamiaa, mambo yameharibikaa sande kaonekana na anatafutwa balaaa.. Mficheni na mkewe, akaizima simu, mwe hizi kazi jameni ni sheedah!
Tamia akampandia orijinal mtoe sande watammalizaa, Sande akafichwa na aminaa, wale majambazi kuja wanakuta holaa, hayupoo mwe ni balaa!
Wakarudi kwa Fish, sande amefichwa nahisi tunae snitch amemtonyaa ndo mana kafichwaa, wakapewa kazi ya kumfuatilia traitor ni nani,
Papaa akarudi hm anamafuraha, kelis anaambiwa mama we lala, me ntapika, me ntafua, me ntafanya kila kitu gadame, Kelis akaona sasa mchaga

Naona ntakuwa mlemavu bila sabab, hapa lazimanikomaee, akaforce kwenda jobuni, mwee anapiga mzigo mara 2 ya zamani, Papaa ameongea mpaka kachokaa, kelis hasikii mpaka Papaa alipomwambia mimba ikitoka hatutaelewana we endelea na masihara, ndo akapunguza masifa ya kufanya kazi
Baada ya mwezi m1 Kelis akaenda kwa Tamia kumweleza kuwa ana mimba miezi 5, Kelis akachokaa, nguvu kazi yake inapunguaa, maana alimtegemea sana Kelis bin jembe amsaidie kwenye kum seduce Fish, dah basi bwana, akamwambia na Irene nae ameshajifunguaa, mtoto wa kiume, Mutashobya amepata mtoto wa kiume so kesho twaenda kumwona Irene maana Khadija hayupoo na hi hoe bado yupo kwenye uzazi mwemaaa.. KELIS Akashangaa ya Irene na kwanini amekaa kimya hakutaka Baby shower,
Mutashobya baby na mamake wamefurahije kupata mtoto na mjukuu, Yeleuuwi ni sheeda!
Mama mkwe sasa anavyo msujudia Irene utadhani cjui nini, Irene anashaa huyu ndo mama mkwe
Wa Kelis? Mbona me napapatikiwa kama mungu mdogo, whatsup, why? Akaamua a enjoy the ride aone mwisho wake, Irene anakandwaaa, anaogeshwaa, mwezi mzima kazi yake ni kulea na kunyonyesha mtoto tuu, muda mwingi anaangalia tv, akatamani ampigie mama yake amweleze ila yule maza alivyo mnoko akaona bora anyamaZe tu isiwe kesi, maza wake akampandia hewani, we mwana naskia una mimba.
Irene: nani amekwambia mama?
Mama Irene: ni stephano huyoo
Irene: akaona hamna haja
Irene: ndio mama na nimeshajifungua mtoto ana mwezi sasa

Mama irene: mbona haujaniambia sasa?! Jamaaan yeleuuuuwi Yeeesu na maria baba irene mwanetu ana mtoto kajifungua ana mwezi hii si aibu sasa jaman uuuwi

Irene: nimepata mtoto wa kiume, nipo na mama mkwe hapa bibi wa mtoto wangu wa kiume.. nimeshindwa kukweleza maana najua unavyopanic nikaamua kukaa kimya

Mama Irene: uuuuuwi wa kiume baba Irene tuna mjukuu wa kiume Yeeeeesu na Maria na Yosefu!
Usujali mwanangu haina neno kuhusu kuchelewa kuniambia, sasa nambie umeshaolewa na kuolewa au mbona unataja mtoto wa kiume sasa?!

Irene: bado nilipata ujauzito tu

Mama Irene: Yesuu embu rudi nyumbani kwako basi me nataka kuja kukuhudumia huko kwa wakwe haturuhusiwi kabisa kutia mguu maana ni dhambi,najisi, hairuhusiwi kabisaa, mila imekatasa kabisaaa uuuwi

Nitakuja kukulea uzazi mwanangu naomba uhamie kwako uniambie nitakujaaa

Irene: sawa mama.. wakaongea weee na baba akaongea nae wakaagana simu ikakatwa

Akaja Mutashobya, Irene akamweleza kila kitu natakiwa kuhama kwako ili mama aje aniuguzee na mama navyomjua anaweza akakaa miezi 3 kama sio 6

Muta akaona dah tena kwenda kwa hi hoe kwanza padogoje akaenda kupanga nyumba nyingime mikocheniii, akamwamisha wakati mama yake ameends kanisani j2, aliporudi mkwe na mjukuu hawapooo akasema wazazi wake wamekuja juu wamemchukuaaaa,
Mama Mutashobya akaamini, sawa mwanangu basi fanya ulipe mahari uoe kabisa kweli kimila tumekosea sana wanaweza kukulaani wale watu ulahangaika maisha yako yote fanya tulipe mahar
Mutashobya akajipanga kwenda kulipa mahari na nene, akamchukua Piere mume wa Amber, Sande ambae alikuwa hapatikan hakuelezwaaa, Papaa akamsindikiza

Mama Irene akajaaa, na mashangazi na Baba yake Irene wanashangaa Irene anakaa fancy home kuliko yaooo, mama Irene akamwuliza vepee?!

Irene: nimepangishiwa na baba mtotoo na wapo tayari kulipa mahari alafu tubatizeeee

Mama Irene akaenda kumwambia mumewe wanaleta mahari mume wanguu, ita kaka zangu kaka zako waje haraka waje tuuu

Baba Irene aka gather wajomba baba wadogo na msemaji mkuu baada ya wiki 2, akina Papaa wakaleta mahariii, akina Tamia vigelegele vepeee? Mahari ya uchumba kama harusi mwe wachaga jaman mmetisher kwa kutuangushia sherehe kubwa mmekubuhuuu!

Basi Irene akalipiwa mahari ndani ya miezi 2.5 tangu amejifungua akafurahi mwenyewe Tamia anashangaa kweli Mutashobya kapendaaa sio kwa chap chap hizooo! Du!

Irene akawa Engaged the ring was 6 karrat with diamond rings, mehn hawa vijana wa zamani wanajua kutoa vyuma vikali kwenye kidole, i wish ningempata na mie kijana wa saman, hawa wa kisasa wanakuvisha Tanzanite tuuu mwe me hata sizipendagi kwakweli

Baada ya mwezi m1 mbele Harusi ya irene ikafungwaaa, harusi simple but sure si unajua mtoto bado mdogo ana miezi 3 ikawa ya wandugu wachache 20 na marafiki 20 kisherehe kidogo harusi ikapendeza wakapanga meza ndeeefu ya watu 40 Kempinski Hotel

Wachaga wanasangaa sangaa Kempinski on fleekest! Walikuwa wanapasikia tu Yessssu na maria leo wamefika

Siku ya harusi ya Irene na Mutashobya
Ndio walimbatiza mtoto wao Gerald!

Changudoa au side chic au malaya wawili haooo washaolewa hivi hivi watu mjini wanatoa toa tu machoo, hooooow! Tena bonge la bwana .. watu na mapovu yenu wametumia kizizi wamewaloga, mxiiiiiiou! Penzi halilogwi hata siku moja kama ipo ipo ndo ivo sasa muache kuwaona wanaochepuka kama mashetan flan wajaa laana flan Mungu pekee ndio anaeweza kuwahukumu sio mimi wala wewe gademit!

Mauno waliokatika wanaume kwenye danguro unadhani mchezo, we unachezea mitarimbo na mipini kwenye danguro ya ajabu ajabu, hujui fyucha yako ikoje, kila umri kila lugha kila kabila kila rangi, kwa miaka 2 ndio unampata Mr wako mucheeezooo? The higher the risk the higher the return

Sio kwamba natetea machangudoa au malaya au whatever unavyowaitaaa but kwangu mimi binadam wote ni sawa, kama anachukua mume au bwana wangu amchukue tu kwani wanaume wameisha?! Kiru! Hata sie akina mama tunaweza lea watoto bila wanaume vile vile na wakatoka watoto wa ukweli kinyama

Oi oi leo saa 4 NANUS usiku kweeeliii, Yesu na maria

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…