Bilionea kid
JF-Expert Member
- Oct 19, 2018
- 581
- 520
STORY-PENZI LA MSHUMAA
MTUNZI-FREDIRICK M.MZIRAY
SEHEMU YA 1
Malumbano yaliendelea kati ya Denis na wazazi wake pale nyumbani kwao.Mzee Mwamba na mkewe Bi Asma hawakutaka kabisa Denis amuoe Shaimaa.Walisisitiza kuwa msichana huyo hakuwa na sifa za kuwa mke wa kijana wao.Hivyo walimshupalia Denis kama mtoto mdogo.
“Ndiyo nimeshakuambia Shaimaa hafai kuwa mke wako hata kidogo.Na kama unataka mimi baba yako nikuachie laana,basi muoe huyo binti wa Kitanga.Nakuhakikishia nitakuvulia nguo hadharani na katika harusi yako si mimi wala mama yako,hakuna atakayetia mguu.”Mzee Mwamba alizungumza kwa jazba huku akichezesha midomo yake kuonesha hasira alizokuwa nazo.
“Hivi kwanini baba mpaka leo mnashikilia mila na desturi zilizopitwa na wakati?Kwahiyo wazee wangu mnataka kunichagulia mke wa kumuoa?Haya niambieni mnataka nimuoe nani?”Denis alikasirishwa sana na kitendo kile cha wazazi wake kumkataa mchumba wake kwa kumwambia kuwa hana sifa za kuwa mke bora hata kidogo.
“Sikiliza Denis,usitake kubishana na sisi hata siku moja.Wewe bado ni kijana mdogo na hujajua jinsi dunia inavyokwenda.Tunavyokuambia kuwa Shaimaa hafai kuwa mkeo siyo kwamba tunakuchukia mwanangu la hasha!tunakupenda sana ndiyo maana hatutaki utumbukie katika hatari yoyote ile.”Bi Asma alizidi kumshupalia mwanaye.
“Kwani mama kuna tatizo gani nikimuoa Shaimaa?Mbona ni binti mzuri tu na sasa hivi ameshapona kabisa.Hebu niacheni nifanye maamuzi yangu mimi mwenyewe.Sasa hivi nimeshakuwa mtu mzima hivyo nahitaji kuwa huru.”Denis naye alizidi kuwa Mbogo kwa wazazi wake.Hakuwa radhi kuona binti aliyeteka moyo wake ayoyome hivi hivi.
“Sikiliza nikuambie Denis mwanangu,Shaimaa ni binti mzuri sana kisura mpaka kiumbo lakini hana sifa za kuwa mkeo.Mwanangu Denis fanya makosa yote lakini kamwe usikosee katika kuoa.Ndoa yako haitakuwa na amani hata kidogo,kila kukicha itakuwa ni afadhali ya jana.Vivian ni binti mzuri tu na mwenye akili ya maisha.Yule ndiyo anafaa kuwa mke wako wa ndoa mwanangu.”Bi Asma alizidi kumshauri mwanaye lakini Denis hakushaurika.
“Lakini mama,Vivian mwenyewe si ndiyo huyo ameshanikataa.”
“Wewe nenda kazungumze naye taratibu atakuelewa tu.”
“Nizungumze naye mara ngapi mama?Yule mwanamke ni mbishi kama nini hataki kunielewa.Nilimwambia kuwa Shaimaa ni mgonjwa wangu tu sina mahusiano naye lakini hakutaka kuelewa.Sasa mimi ningemlazimisha au?Inaonesha dhahiri kuwa alikuwa hanipendi.”
“Kwahiyo huyo Shaimaa ndiyo anakupenda?”Mzee Mwamba alimuuliza Denis swali kwa hasira.
“Ndiyo ananipenda,tena sana tu,ndiyo maana yupo tayari kufunga ndoa na mimi.”Denis alijibu kwa kujiamini.
“Hivi Denis umelogwa au?Yaani unasema huyo mwanamke anakupenda wakati ndiye aliyekuingiza matatizoni mpaka ukapoteza fedha chungu nzima kwaajili yake.Si uliwekwa ndani wewe kisa Shaimaa hadi biashara zako zikayumba?Halafu leo unasema eti anakupenda tena sana ndiyo maana anataka kufunga ndoa na wewe!Si bure inaelekea kuna mkono wa mtu.”Mzee Mwamba alimtazama mke wake halafu wakahamishia macho kwa Denis kisha wakatikisa kichwa kwa masiitiko.
“Mwanangu Denis hivi wewe ni mzima au umechanganyikiwa?Yaani na kisomo chote ulichonacho unashindwa kuchambua jema na baya!Ndiyo maana baba yako anasema si bure.Yaani unamwona Shaimaa ndiyo bora kuliko Vivian eti kisa ana rangi nyeupe pamoja na makalio makubwa!Hivi wewe una akili kweli?Makalio yanajenga nyumba?Usifikiri ndani ya ndoa kuna mashindano ya umisi au unene.Mwanamke mzuri ni yule mwenye ubongo mzuri wa kufikiria mambo mazuri ya maendeleo ya familia yake.Na mtu pekee mwenye sifa hizo ni Vivian na si Shaimaa kama unavyofikiria.”
Hakika siku hiyo wazee hao waliamua kumpa mtoto wao dozi iliyokuwa chungu ndani ya moyo wake.Hata hivyo kila walichomweleza kulipitia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto.Denis aliendelea kuwa nunda kwa yale aliyoelezwa,hakutaka kukubaliana na wazazi wake hata kidogo.
“Baba,mama,nawaheshimu sana ila kwa hili nipo radhi kuvunjiana heshima na ninyi.”Denis aliwashangaza wazazi wake kwa jinsi alivyotekwa na penzi la binti wa Kitanga Shaimaa.
“Denis mwanangu,Vivian ndiyo mwanamke bora wa kumuoa.”Bi Asma aliamua kuzungumza na mwanaye kwa upole.
“Vivian!Vivian ndiyo nani?Mwanamke fehedhuli kama nini!Mimi nilimweleza ukweli yeye akajifanya mbishi.Nimeshachukua uamuzi wa kumuoa Shaimaa basi,Vivian simtaki tena.”Denis alikwapua funguo yake ya gari mezani na kutoka nje.Mlangoni alipishana na dada yake ambapo alimpiga kikumbo na kumdondosha chini paa!
“Mamaaa!!Haaaa!!kaka Denis unaona ulivyonibwaga chini?”Brenda aliongea kwa sauti ya unyonge baada ya kulamba sakafu.
“Shenzi mkubwa wewe!Kama una kisirani chako peleka huko huko.Usiniumizie mwanangu mie.”Mzee Mwamba alisimama na kumfokea Denis kwa hasira kutokana na kitendo kile alichomfanyia mdogo wake.Denis alimgeukia Brenda na kumtazama kwa dharau kisha akavuta hatua mpaka garini.Aliwasha gari lake aina ya Range Rover na kuyoyoma zake.
“Huyu mpumbavu sijui amechanganyikiwa siku hizi!Au anavuta bangi?Mshenzi mkubwa wewe.”Mzee Mwamba alizidi kufoka kwa hasira.
“Pole mwanangu,msamehe bure kaka yako.Shaimaa atakuwa amemtengeneza kisawasawa.Tena kwa huyo mganga aliyemfanyia mandingo ni fundi kweli kweli,si unamuona jinsi alivyokamatwa!Yaani hafurukuti hata kidogo.”Bi Asma alimpa pole mwanaye huyo wa kike baada ya kupigwa kumbo na Denis.Brenda alijibaraguza pale chini kisha akainuka na kwenda kuketi karibu na mama yake.
“Inamaana bado kaka Denis anang’ang’ania suala la kumuoa Shaimaa?”Brenda aliuliza kwa mshangao.
“Mmmh!mwanangu kapatikana.Hataki kuambiwa wala kusikia chochote juu ya kubadilisha maamuzi yake.Yaani amefikia hatua ya kusema yupo radhi kuvunjiana heshima na sisi wazazi wake kama tutaendelea kumwandama juu ya huyo mchumba wake.”
“Haa!masikini kaka yangu anapotea hivi hivi.Mmmh!chezea Wantanga wewe!”Brenda alimsikitikia kaka yake Denis kutokana na kushikilia msimamo wake wa kumuoa Shaimaa.
“Siyo kwamba anapotea,ni ameshapotea kabisa.Yaani amejitumbukiza mwenyewe kikaangoni.”Bi Asma alisistiza.
“Inawezekana kaka Denis kalogwa hii si bure.Haiwezekani hata kidogo wala haingii akilini kwa mtu kukufanyia ubaya kiasi kile na kumtwisha mzigo usiyostahili halafu leo ndiyo aje kumuoa!Siyo siri kaka Denis ana moyo wa ajabu sana.”Brenda alizidi kupigwa na butwaa.
“Na sitaki kumwona hapa nyumbani kwangu tena.Shenzi kabisa huyu!”Mzee Mwamba alikasirika sana kutokana na ubishi wa Denis.Aliamini kuwa mali alizonazo Denis ndizo zinazompa kiburi na kuyaona mawazo ya wazazi wake si lolote si chochote.
Denis ni kijana aliyepata mafanikio katika umri mdogo mno.Ndiyo kwanza alikuwa na miaka 27 tu lakini alifanikiwa kumiliki sheli 30 za mafuta katika mikoa tofauti tofauti nchini Tanzania.Jijini Dar-es-salaam alikuwa na sheli 10,Tanga sheli 5,Mbeya sheli 5,Kilimanjaro nako alikuwa na sheli 5 pamoja na Mwanza sheli 5.Vile vile alikuwa na vitega uchumi chungu nzima kama vile majumba ya kifahari,maduka,gari za abiria na vinginevyo.
Utajiri huo aliupata baada ya kuibuka na madini toka katika mchimbo ya Mererani mkoani Manyara.Alipomaliza kidato cha sita hakutaka kuendelea na masomo ya chuo kikuu badala yake alijitosa machimboni na ndiyo akabahatika kufumania madini na kwenda kuyauza kwa mamilioni ya pesa.Kutokana na akili za maisha alizokuwa nazo,Denis hakutaka kuzichezea pesa zake kwa starehe zisizokuwa na tija kama vijana wengine wanavyofanya.Aliamua kuwekeza katika biashara ambapo alifungua sheli kubwa Jijini Dar-es-salaam ambayo baadae ilifanikiwa kuzalisha sheli nyingine.
Basi kutokana na juhudi zake katika kazi,Denis alipata mafanikio makubwa sana.Jina lake lilivuma sehemu nyingi za Jiji la Dar-es-salaam.Pia alijulikana baadhi ya maeneo katika mikoa iliyokuwa na vitega uchumi vyake.Mpaka kufikia umri huo Denis alikuwa bado hajaoa.Aliendelea kuhangaika na shughuli zake za kumwingizia kipato ilihali kwenye akaunti zake za benki kulikuwa na noti za kumwaga.
Siku hiyo baada ya kugombana na wazaze wake,Denis aliamua kumpitia rafiki yake aliyemwacha baa moja hivi maeneo ya Temeke mwisho.Baada ya kufika huko alimkuta Dickson akiwa na marafiki zao wengine wakibadilishana mawazo huku wakiendelea kukata vinywaji.
To be continued....