Story: Kariakoo

Kindly refrain from tagging me endlessly in your useless posts.

Upgrade your writing, make more sense then I just might read a sentence or two.
Kumbe ulitagiwa
Bahati mbaya sikumaanisha mkono uliteleza
 
c. 1988 - 1991
(KAMA HAUWEZI KUWASHINDA JIUNGE NAO)




Asee embu nikatie kipande cha muhogo hapo baalia wangu

Baalia: ah dogo mbona unaleta njaa njaa mi mwenyewe nimemegewa na bimdashi hapo ndani
Dogo: ah brooo! mbona unaleta roho mbaya mjini hapa, nimegee hata kiduchu basi unajua sikuile mimi nimekutetea kwa bimdashi wakati umejifungia na mwajuma pale, nimegee bwana nimegee
Baalia: akaona isiwe kero mimi nakumegea muhogo lakini nikienda kujibanza na mwamtumu leo jioni pale kwenye kona ya mwuza machungwa pale club ya simba usinisemee
Dogo: haina shida bro we nigee kipande,
Dogo akapewa kipande akawa anatafuna muhogo akapewa na chumvii, taaaamuuu akasema
ila kaka naniliii kaka baalia, kwanini wewe unapendaga kuliza wanawake, juzi nilikuwa nakushikia pale usikamatwe na bimkubwa si nikawa naskia mwajuma analia anakwambia basi inatoshaaa wewe ndo kwanza hata haumwachii kwanini lakini unaumiza watoto wa watu?
Baalia: akacheka sana, dah kweli wewe dogo ni kilaza hamna mfano wake
wale pale nilikuwa nawaambia sikunyingine tuonane sehemu nyingine sasa akawa anataka kuondoka mwajuma nikamzuia ndio akawa anasema nimwachie namwumiza mkonoo
Dogo: ahaaa basi sikunyingine mtakuwa mnaenda wap?
Baalia: sikunyingine tutakuwa tunaenda kule karibu na bondeni unakuwa unalinda kama miguu 20 mbele yako

Dogo: sawa kaka leo pia tunaenda kule bondeni
Baalia: ndio tukimaliza mechi pale atakuja Mwamtumu ukae nae mpige stori alafu nitakupa ishara unakuja nae sawa?
Dogo: sawa kaka Baalia,
Mara akaja rafiki wa Baalia, asee naona mnakula kula tu miogo mibichi mtakufaaa na minyoo, leo mechi tunachezea Upanga kwa watoto wa mboga 7, kwahiyo sasa hivi tunaamsha kwa mguu mpaka pale Upanga, wenzetu hao hapo wameshavalia, twende sasa
Akainuka nduki kwenda kujiandaa njaa inamwuuma vibaya mno akaja amependeza mwenyewe na jezi yake haooo mpaka upangaaaa

Mechi ikapigwa pigwa wahindi wakawafunga goli la 1.,... la 2... la 3 watoto wa kihindi wanajiita team yanga, yanga hio vepee? kila saa wanashinda wao tuu kiruu!

Mijeda ya kariakoo ikajiona haifaaai, ikajiona kama mitoto ya kikeee tunafungwaje kiboya boya na hawa watoto wa getini tuu kila kitu kinaletwa ndanii

wakaomba break, wakawa wanajadili jinsi gani ya kurudisha magoli 3 waondoke hata bila bila

kurudi ulingoni ni sheedah, hamna cha kungunga wala nini.. wanapigwa tuuu goli la 4 watoto wa kariakoo wakaona labda huenda ni mwendo waliotembeeeaaaa... goal la 5 mpenzi msomajiii, watoto wa Kariakoo aibuuu wakaona hapa isiwe shida, mechi dk 90 watu 5 bila... wakaamua kuwafanyia fujooo. ngumi ngumi na wewe mara sungusungu haooo wanapita ndio kuwafukuza watoto wa kihindi wanajua vichocho vyao wakapanda magorofani,... watoto wa Kariakoo sasa mpaka wakatize Faya wafike ma kwao kuna ka mwendo na sungusungu wako vizuri fukuza fukuza na wewe kila mtu kaingia kichocho anachokijua... madogo wameingia makwao saa 3 usiku na kulala hamna cha msosi wala nini

shida ilikuwa kwa Mwamtumu kulipo kuchaaa, mwamtumu anamtafuta dogo ampeleke kwa Baalia.. dogo akacheuaaa akamponyokaaa Mwamtumuu kuja kuangalia Dogo hayupoooo akaondoka kwa hasira

Dogo akazama kijiwenii alipo Baalia anamkuta anavuta ganja ganja ganjaa

Dogo: ah baalia kakangu wa ukweli tena unavuta sigara

Baalia: ah dogooooo, niambiiieee naona umekuuujaaa mapemaaaa!

Dogo: Mwamtumu anakutafuta kaja kufanya tukio pale nyumbani nikamkimbia kumcheki kwenye ukuta nakuta anaongea na bimkubwa anateta nae mimi sirudi nyumbani umeniachia msala na marafikizako

Baalia: dogooo tatizoo lako unaongea sanaaaa unaniumiza maskiiooo ( kwa sauti ya kitejaaa)
Dogo yule masap ukitaka kumweza inabidi ushushie vitu shwaaariii kama hivi ( kwa sauti ya mateja)

Dogo akaona hapa anaongea na ukuta, mtu keshapendeza macho yameshabalika kama jini mkata kamba akaona bora aondookeee tu mtu keshajidunga na masindano anahemea juu juu mara amshike mguu dogo ohooooo mtu anapaaa Mbingu ya 100

akawa anatembea dogo wa watu kuelekea nyumbani kuchezea bakora maana mwamtumu kesha-haribu nyumbani dah akawa anajipanga staili ya kubana matako akiwa anachapwa bakora, akawa anajaribu kuingiza kaptura nyingine kwa juu basi tu akichapwa asiumieee... kawaza na kuwazua mara anaskia mziki unapigwa hapo kariakoo club ya simba

Watu wamejaaaa akaona ajongee na yeye akaone burudani maana nyumbani wamsehamuharibia bora ale raha awahi nyumbani achapweee aondokeee

akasogea watu kibao wamekaa mlangoni wanasikiliza bendi inaimbaaaa... kumbe ni bendi ya Juwata Jazz Band,



Dogo akanogewaa akakaa na chini kabisaa, Dogo bwana dogo midadi kibaooo, uuuwi kuja kushtukaaa saa 1 nanusu usiku akakimbia kwenda nyumbani bakora kwa kwenda mbelee!
kesho yake hajakomaa karudi pale pale kakuta band hamna wanafanya rehesal watu wengine

dogo basi likizo yote ya mwezi wa 12 kaimalizia kwenye kuskiliza bendi na miziki ya watu... kwasababu alikuwa mwanachama wa kila siku akawa anapewa mike awe anaimba kidogo anapasha pasha wakati wanatest mitambooo

eh mara kawa mzoefu dogo akija tu anapewa back up singer.. kule kwenye mipira kwa akina baalia haonekani tena

siku wakaja kumfuma dogo anaimba kweli kweli... wakubwa wa bendi wanamkubalii dogo nomaaa... akina baalia wanashangaa dogo vepe tenaaa anaimba imba iyo vepee?

mpaka likiza kuisha dogo akawa anaimbia shuleni anajitahidi afanye twishen afaulu lakini nguvu ya mziki ni ya mziki tu matokeo ya darasa la 7 dogo kafeli uuuwi mamake alichapa kazi ya kushinda kwenye miziki tu we mwanangu hasara sana

Dogo kimya basi shule kafeli ndio anashinda pale uwanja wa simba pale Kariakoo... eh dogo akaanza kuimbaa baada ya miezi 6 akawa anbazunguka na bendi yake mwenyewe anaona faari wanamlipa vihela hapo keshakuwa fundi mitambo wa vyombo

Mwaka dogo akawa sio dogo tena, kutoka kwenye jina la dogo mpaka Abdull mpaka dula

imba imba na wewe mpaka leo dogo dula aliishia darasa la 7 tena kafeli... kwenda form 1 mpaka form 4 kwa mbinde kufika form 4 sasa kapasua divishen 0 kabisaa kumwonyesha mama yake yeye shule sio alioitiwa ameitiwa mziki

Wakaamua kumuacha asafiri na bendi weee mpaka atakapochokaaaa

Dulla siku anapita pita mitaa ya kariakoo anakutana na mziki unapigwaaaaa kanisani pale kwa walokoleee akaamua akachungulieee ndio anakutana na rafiki yake waliosomaga nae shule ya msingi Lora

Dulla: samahani dada nahisi kama nakufananishaaa

Lora: kugeuka uuuuwi ni wewe dully?!

Dulla: ndio mimi upoooo?

Lora: ndio nipoo ni mimi... nimeokoka nampenda Yesu kwetu sisi ni walokole so huwa nakujaga kusali hapa ingawa wazazi wangu wanasali Upanga TAG kwa walokole na hapa ni TAG so ni pale pale

Doh Dulla akashangaaa... totoz Lora amenawirijeee amekuwaje wa ukwelii ana rangi ya mtume waswahili wanasemaa

Dulla akakosa pozi na kilichomvutia zaidi ni kumkuta Lora anaimba imba pale nini mziki mnene wakaongea weee basi kila jioni anakuja pale Kanisani wakati bendi hazitembei anakuja kuimba na Lora wake kwaya kwaya na Tenzi za rohoni woyooooooo Bonge la SHOW!



KUMALIZIA NA HADITHI HII NENDA KARIAKOO... - MONEY PENNY TZ

ASANTE SANA KUSHIRIKI


Haya
 
Back
Top Bottom