Stori ya mti na baskeli

Coolant

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
1,256
Reaction score
2,201
Bila shaka mtakua wazima wa afya wana JF!

Leo nimeona ni vizuri kushea stori ambayo kwa kiasi fulani ni maarufu na ya kushangaza kidogo ijulikanayo kama "mti na baskeli" kama ulikua huijui basi isome hapa...

Katika kisiwa cha Vashon kilichopo King County Washington kuna mti ujulikanao kama Vashon Island bike tree. Kama unavyoonekana kwenye picha

Stori yake inaanzia mnamo miaka ya 1950, na inasimuliwa na Don Puz afisa mstaafu wa polisi wa King County ambaye ndiye kijana aliye itelekeza baiskeli yake kwenye mti huo miaka hiyo ya 1950 akiwa ni kijana mdogo wa miaka nane ambaye kwa sasa anaishi Kennewick.

Puz anaeleza kua mnamo mwaka 1954 baba yake alifariki kwa ajali ya moto iliyotokea nyumbani kwao, na kumuacha mama yao na watoto wa tano. Baada ya msiba wa baba yake kuisha, majirani zao katika kisiwa cha Vashon walikusanyika kwa ajili ya kuwachangia ili waweze kujikimu kimaisha kutokana na kupoteza kila kitu katika ajali ya moto. Baadhi ya vitu walivyopokea kutoka kwa majirani ni pamoja na baskeli kwa ajili ya mtoto Don Puz.

"Sikuipenda baskeli ile kwasababu ilikua kama ina matairi matatu lakini yalikua mawili, mipira ya matairi ilikua migumu sana pia sehemu za kushikia zilikua nyembamba na ndogo sana" alisema Puz.

Puz anasema baada ya hapo familia yao ilihamia eneo lingine, katika eneo walilohamia kulikua na eneo la swampy (eneo lenye maji maji) ambalo watoto wengi walikua wanapenda kucheza hapo. Na hapo ndipo alipoisahau baskeli yake aliyokua ameiegemeza kwenye mti mdogo, na hata alipo ikumbuka hakurudi kuichukua kwasababu alikua haipendi.

Ndio hapo tunaona nguvu ya asili iliyopo kwenye huo mti wa pine, mti huo umekua kivutio kikubwa sana kwa wakazi wa Vasion Island na duniani kwa ujumla. Mimi pia nimevutiwa na huo mti ndio maana nimeamua kushea hii stori hapa.
 
Story mbona kama maajabu tu hamna mkasa kamili
 
Naomba kujua mti na baiskeli vilikutana vipi i mean ilikuaje kuaje mpk baiskeli ikawa katikati ya mti??

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
mkuu sio kweli kuna page moja fb iliposti iyo picha kwamba iliachwa na kijana ambae alienda kupigana ww2
na huo mti ulikuwa mdogo kama mchungwa dogo alipiga chain baiskeli yake akaelekea vitani
na sio kama ulivyoandika hapo juu
 
Inasemekana hivyo hata mimi niliiona ila nikawa interested kuifatilia zaidi ndio nikapata ukweli wake
 
Naomba kujua mti na baiskeli vilikutana vipi i mean ilikuaje kuaje mpk baiskeli ikawa katikati ya mti??

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.

Iliegemezwa kwenye huo mti pindi ukiwa bado mdogo, ulivyokua una nenepa na kukua ukaimeza hiyo baskeli
 
Iliegemezwa kwenye huo mti pindi ukiwa bado mdogo, ulivyokua una nenepa na kukua ukaimeza hiyo baskeli
Wow!!! incredible.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
huo mti ulikuwa mdogo mithili ya mchungwa na yule kijana aliipiga chain baiskeli pamoja na huo mti
Oooh.... interesting

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…