stori: Sitakusahau Yohana

stori: Sitakusahau Yohana

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,784
Reaction score
6,183
wadau leo naileta kwenu hii hadithi ya kusisimua,
>>>>>>>>>>

Wazazi wangu walikuwa na kila kitu na ikiwemo migodi ya dhahabu, zoo, na kila aina ya utajiri, wakti huu nilikuwa namaliza chuo nchini Canada na ndio nilikuwa narudi nyumbani, baba hakutaka niajiriwe popote kwani mimi nilikuwa mtoto pekee hivyo akanitaka nisimamie shughuli zote za biashara kwa ajili ya faida ya baadae wakiwa hawapo tena duniani,

Nakumbuka mwaka 2015 mwezi wa 10 baba aliniletea mchumba na kutaka niolewe nae, baba alisema amenitafutia mtu makini, mtu jasiri tena baba akadai huyu ni "bulDozer" eti haogopi kitu
kwa haraka haraka nilivutiwa na yohana, ingawa kuna kitu kilinitisha naam...mavazi yake, yohana alikuwa Rafu mno, ni kama baba alijua mashaka yangu aliniita pembeni na kuniambia, nisijali kwani Yohana ni mtu ambaye hana tamaa, pamoja na pesa alizo nazo lakini hana majivuno.. pamoja na hayo baba aliniambia sababu kubwa ya kumchagua Yohana ni suala la miradi na biashara, alidai Yohana ana uzoefu mkubwa katika suala la kusimamia miradi na biashara hivyo ni mtu sahihi kwangu, hatimaye octoba 25 tukafunga ndoa na Yohana, kama kawaida siku ya harusi Yohana alivaa koti ambalo halikufanana na suruali! ilibidi kila wakati kutazama chini kwa aibu, Yohana yeye alitabasamu tu na kunikumbatia kila saa.
baada ya ndoa tu baba alijitoa na mikoba yote akapewa Yohana!
>>>>>>>>>>>
baada ya miezi minne ya ndoa Yohana alibadilika kabisa, kwanza alifukuza wafanyakazi wote wa ndani, akinitaka nifanye kazi zote, Yohana hakupenda kabisa kuona nikiwa nimepumzika Yohana yeye alipenda kazi tu, kazi tu...

mbaya zaidi Yohana alichukua akaunti zote za benki na kuziunganisha kwenye akaunti moja na akaanza kulipa mwenyewe mishahara badala ya kutumia mhasibu wa kampuni kama tulivyozoea, hii ilipelekea wafanyakazi wetu zaidi ya 200 kukosa mshahara na kuleta usumbufu mkubwa, Yohana hakupenda vikao au majadiliano akidai majadiliano na vikao huleta majungu,

hatimaye uzalishaji ukapungua kwenye kampuni zetu na ikatulazimu kufunga baadhi ya kampuni na kupunguza wafanyakazi, hata wafanyakazi waliobaki walikuwa wakilalamika kila siku kuhusu udogo wa mishahara na mazingira ya kazi, lawama nyingi zilifika kwangu lakini Yohana alisema tuwaache tu
"walizoea kupiga dili,waache wapige kelele" yalikuwa maneno ya Yohana kila siku...

kutokana na kuzidiwa na kazi hali yangu ilidhoofu, na sikuwa tena mimi angela niliyekuwa mzuri na kupendeza... aliongea Angela akitoa machozi,

"juzi alichukua mapato yote akaenda kununua magunia mawili ya misumari na kuyaleta nyumbani, nilipomuuliza kwanini anunue misumari mingi kiasi hicho alijibu anataka kujenga, hio ni mbinu ya kupunguza gharama, mafundi wanaiba sana kama ukiwapa pesa ya vifaa wataongeza bei, ndio maana nimenunua mwenyewe,

"lakini Yohana, misumari hii ni mingi sana, bora hata ungenunua chakula ukawapa wale wafanyakazi kule shambani, kumbuka kila saa wanapiga simu hawana chakula ....

"kwani hawalipwi mishahara? kazi ya mshahara ni nini? Yohana alinikatisha,
"lakini Yohana kumbuka mshahara huu hata kama ungekuwa unalipwa wewe usingetosha....
Yohana aliondoka zake kwa hasira huku akisema mimi natumika, kuna watu wananituma lakini atadeal nao,

hakika Yohana alibadilika sana..

itaendelea....
 
Back
Top Bottom