Prince Gasper94
Member
- Feb 26, 2013
- 13
- 4
Kuna uzi ni sawa na Story ila visa na mikasa yake kulingana na vile ilivyo msomaji ndio anaweza tengeneza jina la kile kitakacho andikwa.......
Story isiyo na Jina
Ni miaka takribani 36 alizaliwa kijana mmoja mwenye asili ya Italy
na Germany
(asili ya Babu na Bibi zake) ila alibahatika kuzaliwa ndani ya nchi yenye kusifiwa kuwa na amani ,upendo, umoja na furaha kwa wananchi wake..
Nchi hiyi iliitwa Tanzania
Kwa bahati mbaya sana Mzazi wake hakuamini kile alichokiona kwa mkewe jinsi ya uzuri na weupe wa kijana yule hadi aliposhawishiwa na majirani kuwa hawezi kua mwanaye bali ni mtoto wa mtu mwingine, alipinga ila moja ya sababu iliyomfanya kuamini ni kwa vile mkewe naye alikua akifanya kazi kwa wazungu.
Story zilivuma sana juu ya uzao wa kijana yule ,lakini mama yake hakusita kumbeba na kwenda naye kijijini kwa mumewe na kupokelewa na Baba mkwe ,cha kushangaza alipomuona mjukuu alimkumbatia mnoo na bila kusita akampa jina Lake..,Neno Lake moja lililompa Faraja mwanamke..,hiki kizazi nilikitafuta saana ila sikuwahi kubahatika kukipata HAKIKA namuona BABA yangu ndani ya uzao huu.
Alikaa chini na kumuhadithia Story iliyowafanya hadi kuingia Tanzania enzi hizo za vita katika nchi ya Tanganyika..,Mama mwenye mtoto alifurahi kwa kupokelewa vyema na Mkwe wake.
Lakini upande wa Mumewe iliendelea kua Tofauti, kuwa mtoto hakua wake..,Mama yule kwakua naye alikua na kiu yakupata mtoto wa kiume ,hakusumbuka tena kubishana na mumewe kwani alikuja kugundua Mumewe yupo na mahusiano na wanawake wengine na walibahatika kuzaa watoto wakike ila yeye pekee ndio alibahatika kupata wakiume...
Miaka ikaenda akakubali kuishi peke yake na mtoto wake huyo na kumpa jina la Baba mkwe wake.
Kadri siku zilivyokua zinasonga ndio mtoto alikua anapendwa sana haswa na wamama na wadada wa mtaani.,kila mmoja alikua akimuita kwa majina tofauti tofauti...
Mchumba .,mkwe ,mume ,Handsome boy .,sukari yao, changamoto ya mtaa n.k
Hakika mtoto alikua mzuri na wakuvutia na Mama yake alijua kumtuza vyema...
Uzuri ule wa kijana yule hakumuharibia chochote kipindi cha ukuaji wake kwani naye alijaaliwa kujua kujichanganya kwa mtu yoyote, bahati nzuri alikua akiishi sehemu za uswazi mnooo na alijua kuishi maisha ya uswazi...
Alikua akijichanganya na kila rika na watu aina tofauti tofauti, walevi, wavuta bangi ,dada poa ,popote cha msingi siku zinasonga na hakuwahi aribikiwa.
Elimu aliipata mapema sana uraiani kabla yakuingia shule rasmi ,na akawa lulu ndani ya shule ,si walimu wala wanafunzi wenzie haswa wa kike ,walimpenda saaana, isingelikua kukua kwake ndani ya kila mikono ya watu tofauti tofauti basi ukimuona unaweza usiamini yamkini ukipata bahati ya kukaa naye...
Kijana mwenye miaka 5 kuanza la kwanza miaka ya 1990+ si jambo dogo
Dogo alikua mjanja sana.,na mwepesi wakufanya jambo lolote kwa uharaka na bila kukamatwa wala kugundulika kama alifanya..,ndani ya dk 5 unaweza mkuta sehemu 3 tofauti na usijue kafikaje.
Alikua mcha Mungu ,alijua karate bali hakua mkorofi ,alijua mbinu zakufika popote nakutoka kwa muda wa haraka bila kugundulika.....
Cha kushangaza hakuwahi kuwa na utani na hao watoto wa kike ,kwani alikua na nidhamu mnooo kila alipokua akimuona mwanamke kwa kua aliishi na kuyaishi maisha ya kulelewa na mama yake miaka yote.,hivyo kitu kinatwa jinsia ya kike alikiheshimu saaana.
Ilifika kipindi akitumwa na jinsia ya kiume atajitafakari kabla yakukubali ila jinsi ya kike hawazi chochote.
Ilifika kipindi hata akiona mdada akionewa yupo radhi aokote mawe au amuaadhibu na kitu chochote yule anayemuonea mdada haswa mwanaume.,kwa tabia hiyo ndio ilimfanya Dada poa wakampenda sana, hadi kufika darasa la tatu walimnunulia simu ili likutokea tu jambo vyumbani mwao walikua wakimpigia na hasiti kutoka kwao na kwenda kuwasaidia japo mara chache siku ambazo mama yake yupo Huishia kukaa kimya ila ikifika asubuhi lazima apite kabla ya kwenda shuleni.
Mama yake wala hakuwahi kumuuliza mwanae pesa na vitu anavyomiliki ,vile anavyoviona mama yake alikua akivitoa wapi, yote kwa sababu ya sifa na tabia alizokua akizipata mtaani juu ya mwanae.
Kuna watu walikua wanamfahamu na kumchangamkia mno Mama mtu na kupewa huduma nzuri na zakuvutia kwa ajili ya mwanae tu ,hakuwahi kusikia baya lolote la mwanae zaidi ya sifa nzuri..,hayo yalimfanya kumuamini mno mwanae ila ushauri ulikua ni mmoja tu "TAKE CARE MY SON".........
Itaendelea......
Story isiyo na Jina
Ni miaka takribani 36 alizaliwa kijana mmoja mwenye asili ya Italy
na Germany
(asili ya Babu na Bibi zake) ila alibahatika kuzaliwa ndani ya nchi yenye kusifiwa kuwa na amani ,upendo, umoja na furaha kwa wananchi wake..Nchi hiyi iliitwa Tanzania