GE2025 Steve Nyerere: Vijana maarufu jitathimini kwanza kabla ya kutangaza kugombea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, ameonya kuhusu wimbi la vijana maarufu – hususan kutoka mitandao ya kijamii na burudani – kujitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, akisema si wote wenye nia ya dhati ya kuhudumia wananchi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Kishamba Media, Mengele amesema kuwa siyo kila kijana mwenye umaarufu anapaswa kuwa kiongozi, bali ni muhimu kila anayejitokeza kugombea kutafakari upya dhamira yake.

Mengele ambaye pia ni msanii na mwanaharakati wa kijamii, amesema kuwa katika kipindi hiki ambapo vijana wengi wanavutwa na mvuto wa siasa, kunahitajika busara na tafakari ya kina juu ya jukumu la mbunge katika jamii.

CCM ni kama kokolo ziwani linazoa kila aina ya uchafu(takataka), stive Nyerere ni uchafu (takataka)anaowashauli kina Mwijaku nao ni takataka pia.
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, ameonya kuhusu wimbi la vijana maarufu – hususan kutoka mitandao ya kijamii na burudani – kujitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, akisema si wote wenye nia ya dhati ya kuhudumia wananchi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Kishamba Media, Mengele amesema kuwa siyo kila kijana mwenye umaarufu anapaswa kuwa kiongozi, bali ni muhimu kila anayejitokeza kugombea kutafakari upya dhamira yake.

Mengele ambaye pia ni msanii na mwanaharakati wa kijamii, amesema kuwa katika kipindi hiki ambapo vijana wengi wanavutwa na mvuto wa siasa, kunahitajika busara na tafakari ya kina juu ya jukumu la mbunge katika jamii.

Hivi kama msanii ana kazi gani kwenye data base ya sanaa?!
 
Kwanza hao vijana maarufu ni akina nani hasa.

Umaarufu wao unatokana na nini hasa. sijawahi kuona vijana maarufu zaidi ungesema vijana ambao ni chawa maarufu
 
Vijana "maarufu" anamaanisha wale ambao sisi tukitoka majumbani na kuelekea kwenye majukumu,wao hubaki nyumbani kwa kupitia luninga zetu ili wacheze,kuwaimbia,kwabembeleza na kuwachunga watoto wetu na hosegirls kwa mtindo wa maigizo na tamthiliya.
 
Ni kweli anachosema, ila kwa vile ameyasema hayo baada ya kugombea na kushindwa mara kadhaa, basi waache na wenzake nao wachangie vyama vyao kwenye kuchukua form na vile wahangaike na wajumbe huko, watoboke mifuko akili ziwakae sawa kisha warejee kwenye majukumu yao ya kila siku.

Wasanii wengi walivyoona Sugu, Prof. Jay, na Mwana FA (Hamisi Mwijuma) wameingia bungeni wakaoona ni njia ya mseleleko, let them go, and later they will realize that it is not as easy as they think. Chezea wajumbe wewe, kila leo tunakuona omba omba fulani, chawa na kujigalagaza mavumbini kusifia ujinga eti tukupatie ubunge, ebo.
 
Back
Top Bottom