MANILABHONA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2015
- 462
- 351
Duh sasa hivi unaweza fungulia stesheni za televisheni hata 10 na zote ukakuta wana vipindi vya ajabuajabu, havieleweki lengo lake. Kuna kituo kimoja mara kwa mara utakuta ni kama seres za picha ya watu wanaofanana kama wachina hivi inaboa kwelikweli, halafu nyingine utakuta kipindi ni cha muziki lakini robotatu ya muda mnamsikiliza mtangazaji na siyo muziki tena. Nashauri wasimamizi wa vituo hivi mjitathmini na muulize wananchi wanataka kuona nini. mnaruhusiwa kujifunza kutoka stesheni nyingine mfano za Kenya, Uganda, hata Nigeria. Jirekebisheni