Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakina hoja ya msingi ya kuzuia Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwani kama ni mabadiliko wanayoyazungumza yameshafika tayari.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 27, 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kahama,Wasira aliyekuwa akihutubia wananchi hao amesema sheria zilizofanyiwa mabadiliko ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na madiwani.