Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,031
- 6,876
Mwanafunzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania (SAUT), Stephano Joseph (24) maarufu kama 'Steve Magufuli' amejitosa kuchukua fomu kuomba nia ya kugombea ubunge jimbo la Nyamagana kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025
Mwanachuo huyo ambaye alijizolea umaarufu mitandaoni kipindi cha uongozi wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuigiza sauti za viongozi mbalimbali amesema ni wakati wa wananchi kuwapatia nafasi vijana katika uongozi ili kuimarisha jamii kiuchumi na kisiasa.
"Nimeamua kuchukua fomu ya kutia nia jimbo la Nyamagana lengo kubwa ni kuimarisha ustawi kwa Watanzania maskini, kiuchumi, kisiasa na kijamii mimi ni kijana na kitu ambacho kimenishawishi sana ni mchango wa Rais Samia kwamba vijana tujitokeze kuwania nafasi mbalimbali na yeye atakuwa nyuma yetu, amesema.