Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,468
- 119,622
Habari za Jumapili wakuu.
Kwa wale wanaoenda pale Ubungo watakubaliana na mimi. Kuna utaratibu huu ambao mimi binafsi nauchukia si kidogo.... Ni kuhusu wale wapiga debe wa pale stendi...kiukweli wamezidi na imekuwa kero kubwa kwa wasafiri.
Usikosee ukapita maeneo yale...utajuta usumbufu wake. Wale wapiga debe watakung'ang'ania mpaka basi hata ukiwaambia hausafiri.
Ifike wakati mamlaka zinazohusika ziliangalie hili kwa jicho la tatu...mimi naona kwa mji mkubwa kama Dar unaopokea wageni tofauti kutoka nchi tofauti haikutakiwa kuwe na uholela wa namna ile..ni aibu kwa taifa kiukweli.
Mimi nadhani kwa sababu mabasi haya ya mikoani yana ofisi zao wangekuwepo watu wachache tu pengine wasiozidi ishirini ambao watafanya kazi ya kuwaonesha watu kwenye ofisi husika ikitokea mtu hajui ofisi na utaratibu wa malipo upangwe na wenye ofisi au kila gari ikawa na mtu wake mmoja au wawili.
Najua kuna tatizo la ajira lakini ile kero ya ubungo imevuka mipaka aisee.
Naomba kuwasilisha.