Quinine Mwitu
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 5,530
- 6,122
Habari za leo wakuu,
Maisha yana changamoto nyingi sana,zingine zinaweza kukutoa kabisa kwenye hari uliyo nayo,au kwenye kitu ambacho ulikuwa umekusudia kukifanya.
Si rahisi sana kumwambia mtu fulani,usikate tamaa,wakati akijiangalia kimaisha anakokwenda na aliko toka bado hakuna dalili ya kumfanya aamini kuwa kesho yake inaenda kuwa tofauti, ila INAWEZEKANA kabisa, amini tuu na kama ulikuwa huamini basi anza kujenga imani hiyo kuwa kesho yako itakuwa yenye nuru na mafanikio uliyo nayo,
Usifikirie sana juu ya mahusiano yako yanayo zorota hivi sasa, kukosa kwako elimu, kukosa upendo kutoka kwa watu wanaokuzunguka, mkeo au mumeo hawezi kujivunia uwepo wako kwake, umekuwa bila upendo wa wazazi, madeni nk! vyote vinaweza kuwa vya kupita tuu kama ukiamua kuanzia muda huu
Binadamu alivyo,anakitu kikubwa sana ambacho labda kwa kuwa binadamu wengi tunaishi kwa mazoea kwa hiyo hatujawahi kufikiria ni jinsi gani ukubwa wa hicho kitu kilivyo UBONGO, ubongo ndio kila kitu kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu, kile unachoamini ndicho kitakuwa kupitia ubongo wako, kuna daktari mmoja alikuwa akiongea siku moja kuwa mara nyingi sana wagonjwa wengi wamepewa vidonge visivyohusiana na maradhi waliyo nayo, na walipona maradhi yao,
Kama wanavyosema kuwa ugonjwa na tiba ya mgonjwa upo kwenye akili ya Mgonjwa, hakuna dawa inayotibu ugonjwa fulani, wala hakuna dini, kitu chochote kinachoweza kukutibu zaidi ya imani yako, kama unaamini kuwa unaumwa na ili upone hiyo malaria unayopona lazima unywe mseto,huwezi kupona mpaka unywe mseto, kwahiyo kinachokutibu sio mseto ila ni imani yako,
likewise Ukiwa ni mtu wa kuamini kuwa mimi siwez kufanikiwa kwasababu sijasoma, au vikwazo vilivyoko kwenye mahusiano yangu haviwezi kunifanya nifanikiwe, au kwa kuwa mimi ni kilema nk, ubongo wako hautakuwa na haja ya kufanya kinyume na unachoamini na matendo ya mwili wako yataendana na vile unavyoamini
Amini katika mafanikio,kuwa mwenye moyo mkunjufu,samehe na kuwa mwenye matumaini muda wote,Yes! si rahisi mtu anayepitia kwenye mateso makali kumwambia avumilie,ila wanasema,jaribu lolote litakalo kukumba na kukutesa,lia sana kulingana na maumivu unayoyapta ila lengo lako kichwani lisipotee
Mafanikio yako yako kwako mwenyewe,usipoteze muda kumlaumu aliyekukwamisha,usipoteze muda kufikiria magumu uliyopitia,usikae kutwa nzim kufikira madeni unayodaiwa,uambie ubongo wako nataka maisha mapya sasa kuanzia muda huu,mwili na matendo vitatekeleza ulichouambia ubongo wako
Kila la Kheri wakuu