Stationery Store / Business Centre | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stationery Store / Business Centre

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by FOEL, Feb 22, 2012.

 1. F

  FOEL Senior Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu nani anajua ufanyaji wa hii biashara je ni wapi watu hununua vitu ili waviuze kwenye stationery zao na ni vitu gani vinavyotoka zaidi.

  Kwa ujumla biashara hii inafanywavipi, ndugu yangu wa karibu anataka kuanzisha biashara hii na mimi niwe partner wake lakini sina ufahamu juu ya biashara hii.

  Natanguliza shukrani.
   
 2. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uko wapi?, mkoa gani?, and mnataka muanzisha kwa mtaji kiasi gani?
   
 3. F

  FOEL Senior Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Biashara itafanyikia Mbezi Beach, Dar es Salaam, mtaji ni 15,000,000
   
 4. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kuna shemeji yangu anafanya hii biashara, ameishia kidato cha sita tu, lakini biashara hii imempa mafanikio makubwa sana, lakini yeye ameenda mbali kidogo, anauza mpaka vocha za simu za jumla na ni wakala wa hizi m-pesa, tigo pesa etc.
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nitajikita hapo kwenye red tu
  Wapi watu hununua vitu?
  Unaweza kwenda ZAMZAM STATIONERY AU MANSUMIN PRINTWAYS& STATIONERY (Jamuhuri Street-Posta) but vitu vyao ni vya gharama sana. Sehemu nzuri ni K/KOO (kongo/kipata street), Baada ta kutoka roundabout ya Msimbazi, kama unaelekea Mnazi Mmoja ni Mtaa wa Kwanza upande wa kulia. Huko ndipo utapata vitu unavyovitaka kwa bei ya kawaida.

  Kama unahitaji Copiers (used) kwa matumizi ya ofisi,
  unaweza kwenda Senga & Company. Unapotoka hapo Mansumin (Jamuhuri Street), unafuata hiyo barabara kama unaelekea Mnazi Mmoja, utakuta junction ya Jamuhuri na Morogoro road, (Ipo ICB). Unaelekea mbele kidogo upande wa kushoto, utaona Bango lenye Jina hilo.

  Vilevile unaweza kwenda Keko-unashuka Veta. Kuna majengo ya Sophia House. Ground floor utawaona, EastLand (sorry sina uhakika sana na hili jina)

  Au ukiwa K/KOO, fika stand ya daladala zinazoenda mbagala, mtongani... (fuata barabara ya kwanza upande wa kulia baada ya kutoka round about ya Msimbazi kama unaelekea kamata). Fuata hiyo barabara kama unaenda Shaurimoyo, duka la tano upande wa kulia kuna Simba Hightech, utapata huduma hiyo

  Vitu vinavyotoka zaidi?
  Hii ni ngumu kujibu kwani inategemea mazingira uliyopo, hivyo fanya utafiti kwanza
   
 6. majonzi

  majonzi Senior Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndungu yangu Biashara hii unaweza kufanya popote na mambo yakawa mswano ila sehemu nzuri zaidi kwa biashara hii ni maeneo ya mashule na vyuo. kuhusu ni vutu gani vinatoka inategemea na msimu kipindi cha kufungua shule utauza sana madaftari kipindi cha kawaida ni copy kwakwenda mbele, inakubidi uweke vitu vyote ili mteja akija asikose kitu. sehemu ya kupata bidhaa hizi ni kariakoo kwenye maduka ya wasomali
   
 7. F

  FOEL Senior Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu, nitayafanyia kazi mawazo yako, asante sana kwa mchango wako.

  Vipi upo kwenye hii biashara na ungeweza kumshauri nini muanzaje na je unadhani start up capital inayohitajika ni kiasi gani kwa wastani?

  Na je kama ukiajili mfanyakazi mshahara unatakiwa uwe kiasi gani?..
   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu sipo kwenye biashara hii kwa sasa ila nilishawahi kuifanya kwa kipindi fulani huko mikoani. Katika Business Plan zangu, huwa ninaweka exit stratergy, hivyo baada ya kupata kile nilichokitaka ktk biashara hii someone else took over. Na kwa sasa biashara imekuwa sana, lakini nikikusimulia namna ilivyoanza, unaweza usiamin (its very motivational).

  Kwa uzoefu wangu, (huku Site) biashara hii unaweza ukaianza na mtaji mdogo (3m to 4m) na bado ukafanikiwa (lakin ni kama matumizi yako hayatazidi mapato yako). Wengi walianza na mitaji midogo, halafu wakawa wanawekeza ile faida inayotengenezwa kama mtaji. Kwa hiyo nikutoe wasiwasi na huo mtaji wako wa 15M. Challenge kubwa kwa hapa Dar ni RENT na mahali muafaka pa kufanyia hiyo biashara

  Pia ninakushauri ufanye kitu inaitwa DEBT FINANCING, itakusaidia sana kwenye masuala ya kodi huko TRA. (Geuza huo mtaji wa 15m kama mkopo kutoka kwenye familia au rafiki). Hii itakulazimu kufanya deductions (principal + interest) kwenye mapato yako. Hivyo itakupunguza taxable income kwa kipindi cha marejesho. Kama utahitaji Tax Planning Measures zaidi (for tax saving purposes tena legally) unaweza ukaniPM

  Kuhusu namna ya kulipa mshahara
  Hili suala (kwa biashara hizi) kila mtu huwa analiangalia anavyoliona kulingana na ukubwa wa biashara pamoja na mapato yake kwa mwezi, bila kusahau ujuzi wa mfanyakazi husika. Personally, huwa napenda kutumia "performance indicators" kama njia ya kumlipa mfanyakazi, lakini huwa silipi chini ya Minimum wage ya serikali. Na allowance kama ya nauli na chakula (akiwa kazini) ni muhimu kama sivyo elewa kuwa atachukua mwenyewe kwa njia nyingine

  N:B
  Compliance ni muhimu sana, hivyo nakushauri usajili biashara yako katika mamlaka zinazohusika (itakusaidia kwenye mambo ya kibenki, utaepuka usumbufu na utajenga image nzuri kwenye jamii. Na kubwa zaidi utashiriki katika ujenzi wa Taifa lako kupitia Kodi yako.
  Mamlaka zinazohusika ni BRELA, TRA na Local Government Authorities (kwa case yako ni Manispaa ya Kinondoni)
   
 9. F

  FOEL Senior Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu asante sana kwa Mchango, Mwenyezi Mungu akubariki sana.
   
 10. F

  FOEL Senior Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mjasiliamali, asante sana kwa mchango wako nimefaidika sana, nikiwa na shida yoyote kuhusu hii project nitakupa PM.

  Mungu akubariki sana.
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Kama alivyofafanua mkuu Entrepreneur, rasimisha biashara yako, na ukiweza isajili kama kampuni then uwe unatafuta deals za kusupply kwny taasisi, inafaida zaidi!
   
 12. F

  FOEL Senior Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu biashara imesashajiliwa na eneo la biashara tayari tunalo, tunbahitaji michango yenu ya mawazo kama nilivyo ainisha hapo juu, ili tuingie kwenye biashara hii na elimu ya kutosha.

  Asante sana kwa post yako mkuu.
   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Anytime FI. You are welcome
   
 14. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Thanx brother. Binafsi sijawahi kufanya hiyo biashara, lakn nina jamaa zangu wanafanya: mmoja four years back alikuwa na duka lamahtaji ya nyumbani, hyo biashara ikawa kwake haiendi vzuri mtu mmoja akamng'ata skio akaingia kwenye stationery, ndani ya miaka minne amenunua ghorofa mkoani, amepaki gari nne za kutembelea, kila gari thamani yake haipungui 70M!...dalili kwamba anaingiza kiasi kikubwa kuliko uwezo wake wa kuwekeza, ni kijana. Nachoweza kukuhakikishia ni kwamba uwe karibu na procurement officers wa taasisi/na rushwa kidogo watakupa kazi nyingi ukiwahakikishia percent yao, kama uko kinyume na rushwa bora uache tu, itakuwia vigumu kupata kazi.
   
 15. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo kwenye red kunaibua maswali mengi kuliko majibu :suspicious:. Ninachoweza kusema ni kuwa, sio kila kitu kipo kama kinavyooneka.

  Hapo kwenye blue imekaa vizuri sana, na kwa sasa jamaa anaweza akajisajili GPSA (Government Procurement Services Agent) ili atambuliwe kama supplier baada ya kujaza zile bidding documents kama hiyo hapo chini
   

  Attached Files:

 16. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna Wahindi hapo bongo wanasomesha watoto wao huku US kwa ajili ya biashara hiyo, sina ufahamu mkubwa lakini wanadai kama utakuwa mjanga na kupata dili ya ku supply kwenye corporate companies, NGO na serikalini huku unaendelea kuwauzia wananchi wa kawaida basi kufanikiwa ni kwa kiasi kikubwa.

  Mimi naamini Tanzania bado ushindani siyo mkubwa, kwa biashara yoyote kama ukiwa makini na unasimamia biashara yako vizuri, unaongeza mtaji mara kwa mara basi utafika mbali tu.

  Karibu kwenye dunia ya kujiajili kaka.

  GJ
   
 17. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Thats true mate.
  Lakin wengi wao hawafanyi retail business na ukikuta wanafanya basi ujue wanafanya na wholesale hapo hapo, kwan wao ndio Importers. Halafu wamethibiti sana distribution chain, hivyo ni rahisi kufanya conspiracy

  Vilevile hawa jamaa wanamitaji mikubwa sana, sio kama wa huyu Mdau wetu (Fake Id) ambaye ana 15M. Na ukiwakuta ambao hawana mitaji in term of cash, basi wana social capital kubwa, hivyo wanauwezo wa kutumia nyaraka za wenzao kuombea tender somewhere na kuchukua mzigo mkubwa bila kulipia. Na kwa kuwa wanajua njaa ya waswahili, ni rahisi kufanya regulatory capture, na kukamata tender kubwa kubwa!

  Lazima nasi waswahili tuangalie namna ya kutengeneza sound business network kama wanavyofanya watanzania wenzetu wenye asili ya Asia
   
 18. F

  FOEL Senior Member

  #18
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kaka unajua kazi za town ni kujituma kwa hali ya juu.

  Asante sana.
   
 19. F

  FOEL Senior Member

  #19
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa kutiana moyo na shime kiasi hii Mzee wa @ DC
   
 20. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka ninafahamu printers watatu wakubwa sana sasa hivi huko Tanzania na walianza na stationery kama kijana fake id anavyotaka kuanza tena labda yeye anawezakuwa anaanzia juu kidogo kuliko hawa jamaa.

  Na kuna jamaa mwingine ni importer mkubwa sana kwa printers wa large format na paper na yeye alitokea huko huko aliko fake id.

  Kijana wewe kuwa makini na fanya kazi kwa moyo wote, hata kama ni kutoa photocopy hadi saa tano usiku wewe fanya kazi, siku moja utapata muda wa kupumzika na kuja kula raha huku majuu huku biashara zao ukifanya kwa simu na email.

  GJ
   
Loading...