Kwakuwa kumekuwepo na tuhuma za rushwa dhidi ya kamati kadhaa za bunge na baadhi ya wabunge, mathalani tuhuma za rushwa dhidi ya kamati za bunge za madini na nishati, maendeleo ya jamii na mashirika ya umma, na mbunge Kafulila aliwahi kuwataja baadhi yao bungeni, na mmojawao amefikishwa mahakamani hivi karibuni kwa tuhuma za rushwa.
Kwanini spika wa bunge akubali kuvunja kamati ya nishati na madini pekee huku akiziacha kamati za maendeleo ya jamii pamoja na kamati ya mashirika ya umma? Hapo spika analindaje maslahi ya nchi kwa kutovunja kamati ambazo haziaminiwi na wananchi?