Startimes wanataka tulipie kuangalia hata TBC?

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
10,323
18,541
Jamani mambo ya startimes yamezidi kua hovyo kwelikweli.
Jana nimeishiwa kifurushi katika king'amuzi changu cha startimes cha ajabu channels zote mapaka TBC hazishiki, channel inayoshika ni Startimes guide peke yake.
Hivi ni sahihi kulipia mpaka TBC? hapa startimes wanachemka sasa yaani ukiishiwa kifurushi TV inabidi uizime?
TCRA sijui kama wametusahau au kuna nini

Nilipoona mambo yamekua hivyo nikawapigia customer care, wananiambia nisipolipia basi hataTBC sitaangalia aisee huu ni utaratibu mpya au ni kwangu tu
 
Bora wewe wamekuachia hiyo gaid mimi wamwebakisha channel inaitwa one, vipindi vyao vingi ni recorder vya afrika magharibi, michezo wanaonyesha ambayo bongo haiwezekaniki kama kukwepa kwa helcopter, ni maigizo na muziki muda wote hata kipindi cha alfajiri, Waliweza kunifurahisha kitu kimoja tuu, ni kuonyesha LIVE ndondi baina ya JOSHUA na KLITHKO
 
Wanasiasa walituaminisha yakuwa chanel za bongo ni bure,ngoja mkulu siku atakapoenda tutajua mbivu na mbichi
 
Kwa mujibu wa aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye, akiongozana na wajumbe wa kamati ya bunge chini ya mwenyekiti Peter Serukamba walipotembelea ofisi za TBC, waliambiwa matatizo yanayolikumba shirika hilo..

Nape aliyekuwa bosi wa wizara, alitoa maoni yake binafsi kuwa TBC inahitaji maboresho makubwa yanayohitaji pesa nyingi.. Hakuishia hapo bali alienda mbali na kusema "Wamekaa na wadau mbali mbali ikiwemo mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, na wakashauriwa ili shirika liweze kuwa la kisasa zaidi ni lazima lijiendeshe kibiashara zaidi tofauti na ilivyokuwa". Yaani TBC iondolewe kwenye channel za bure na iwekwe kwenye zile za kulipia ..

Hivyo mdau hapo juu ya kupasa kutambua kuwa, mojawapo ya taasisi za umma zinazoongoza kuwakandamiza waTANZANIA wa leo, TCRA ni mfano ulio hai kwani hakuna jema walilowahi kuwafanyia waTANZANIA hata siku moja ..

[HASHTAG]#kulipia[/HASHTAG] habari wao
[HASHTAG]#kuzima[/HASHTAG] simu wao
[HASHTAG]#kupandisha[/HASHTAG] cost za mawasiliano wao
 
Jamani mambo ya startimes yamezidi kua hovyo kwelikweli.
Jana nimeishiwa kifurushi katika king'amuzi changu cha startimes cha ajabu channels zote mapaka TBC hazishiki, channel inayoshika ni Startimes guide peke yake.
Hivi ni sahihi kulipia mpaka TBC? hapa startimes wanachemka sasa yaani ukiishiwa kifurushi TV inabidi uizime?
TCRA sijui kama wametusahau au kuna nini

Nilipoona mambo yamekua hivyo nikawapigia customer care, wananiambia nisipolipia basi hataTBC sitaangalia aisee huu ni utaratibu mpya au ni kwangu tu

Unadhani wao Kodi ya JPM wataitoa wapi Mkuu?
 
Hivi kuna watu mpaka sasa wanaangalia TBC
Hivi wewe unapomjibu mtu "sina hata shilingi kumi" ni kweli ukiwa na shilingi kumi utaitumia?
Kusema sioni hata TBC ni lugha ya picha sawa na kusema sina hata thumni ukimaanisha huna pesa kabisaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom