Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Jana nimepigiwa simu na mtoa huduma nimeambiwa mnawapigia wateja wenu wote,eti mnataka kufanya maboresho??

Mtoa huduma,,,,,,,,,Habari naongea na warda.....,unaongea na mtoa huduma statimes hapa,


Mie,,,,,,habari ni njema kabisa,sijui wewe vipi kazi??


Mtoa huduma,,,,,,,,,vipi warda tokea ujiunge na statimes kuna tatizo lolote dear???

Mie,,,,,,,,hapana


Mtoa huduma,,,,,,,ni mwi#ho lini umelipia kifurushi???


Mie,,,,,,,,,,,tokea tarehe 27 mwezi wa tano na kuishia mwezi wa sita,


Mtoa huduma,,,,,,,sasa tunataka kufanya maboresho hivyo unatakiwa ulipie,usipolipoa unaweza pata shida,,,maboresho yatakuwa ni wiki ijayo,


Mie,,,,,,,,poa, nitalipia,


Mtoa huduma,,,,,,,,sawa,utalipia lini?


Mie,,,,,,,,ata leo jioni naweza kulipia,



Mtoa huduma,,,,,,,,,sawa ngoja nikiweke kwenye orodha ya watakaolipia leo,


Mie,,,,,,,,,,poa,



Mtoa huduma,,,,,,,,,,,sawa usikose kulipia,



Mie,,,,,,,,,,,,,poa.




Sasa watumiaji wenzangu mmepigiwa????


Au ndio njia ya kulazimishana kulipia????
 
Viongozi wa ccm turudishieni analog frequency channels. Digital iwe choice maana tunalipishwa hadi local channel. Mungu anawaona na vizazi vyenu vyote. Amen.v
 
Ndiyoo, Walipiga simu.
 
Mnaotaka kuhama star times mtakuja kuwakumbuka world cup ikifika, kwani ukiondoa DSTV kampuñi inayofuata kwa kuonyesha michuano mingi Tanzania na kwa bei Rahisi ni Star times, Bundesliga, laliga, Euro, world cup European qualify, Asia qualify, copa italia, Michuano yote mikubwa inayosimamiwa na caf World cup nk na pia nasikia wako njiani kuonyesha ligi ya Brazil mimi huniambii kitu kuhusu hawa jamaa
 
Toka saa 10:00 jioni nimelipia hakuna chanel,,,,huduma kwa wateja wanamajibu mepeesi na hamna muda wa kumsikiliza mteja,,,,Hamko peke enu mmekuja toa huduma au kusumbua wateja?
 

Attachments

  • JPEG_20220812_190107_9151151879247281356.jpg
    35.8 KB · Views: 43
Tunaomba mtuwekee radio za kibongo, hiyo tbc fm pekee haitoshi.
 
hawa startimes wameona kila mtu ni wa kufuatilia season za kihind
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…