Startimes imedhamilia kuwatapeli wananchi masikini

Mimi sikulamba sukari

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
1,605
2,000
Habari wanajukwaa

Kwanza nikiri kwamba sina maana nataka kuwaharibia biashara yetu ila kwa haya mnayoyafanya nidhahiri mnataka kujiaribia nyinyi wenyewe hasa kwa kuwatapeli wananchi maskini ambao tupo wengi tunatumia hivyo visimbusi vyenu

Startimes kumbukeni nyinyi ndiyo mlisababisha tukahama kutoka ulimwengu wa analogy mpaka Digital sasa iweje hii leo mnageka kuwa matapeli

Anyway Acha nitoe evidence ambayo mimi mwenyewe imenikuta, mwezi uliopita nilinunua kisimbusi Chenu mnachokipigia promo kuwa ni 49000=/Tsh ingawa siyo bei hiyo kama mnavyoinadi, haikupita mwezi kikawa hakionyeshi picha nilipokirudisha naambiwa nitoe 20000=/Tsh ili nibadilishiwe Asa huu siutapeli yaani mali yanu imezingua nawarudishia mnipe kingine mnasema yanipasa nitoe pesa hii imekaaje?

Haitoshi hao mafundi sijui mliowajaza humo ofisini kwenu wengi wao wameweka njaa mbele tuu hakuna cha ufundi wala nini

Ving'amuzi vya zamani yaani vile vya bati mlianza kuvizima sauti ili mtuuzie hivyo mlivyotoa matokeo yake navyo fake mteja akirudisha anaambiwa toa kiasi kadhaa cha feza ili tukulekebishie ili hari ninyi wenyewe mmevimute sauti.

Startimes acheni utapeli hao weusi wenzetu mliowajaza hapo ofisini watawaharibia kama mmechoka fungasheni virago mrudi kwenu chaina hatuwataki mnanyonya wananchi walala hoi, juzi nimeenda pale ofisini kwenu kuna mama alileta kisembusi chake hakiwaki kumbe tatizo niwaya ulikuwa mbovu chaajabu kapigwa 14000=/Tsh Asa huu siutapeli?

Serikali iturudishe kwenye mfumo wetu wa analogy la sivyo tutaendelea kupigwa, pesa ngumu kupatikana aisee.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,232
2,000
Hao Wachina ni matapeli daraja la KWANZA.

Mama yangu alipata shida ya king'amuzi, nikaenda kuwapelekea, wakanijibu kuwa nitoe 35,000/- 20'000/ Ni kifurushi na 15'000/- ufundi.

Nikarudi nacho home nikiwa na chenzake, kutoka Azam. Nikamuunganishia bi mkubwa anashangaa anaona vitu tofauti na vizuri zaidi.

Kwanza Startimes ililetwa na ma CCM ili tunyonywe.

Rejea mkataba mchafu unaofichwa Sana wa TBC NA STARTIMES
 

Mimi sikulamba sukari

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
1,605
2,000
Hao Wachina ni matapeli daraja la KWANZA.

Mama yangu alipata shida ya king'amuzi, nikaenda kuwapelekea, wakanijibu kuwa nitoe 35,000/- 20'000/ Ni kifurushi na 15'000/- ufundi.

Nikarudi nacho home nikiwa na chenzake, kutoka Azam. Nikamuunganishia bi mkubwa anashangaa anaona vitu tofauti na vizuri zaidi.

Kwanza Startimes ililetwa na ma CCM ili tunyonywe.

Rejea mkataba mchafu unaofichwa Sana wa TBC NA STARTIMES
Tatizo mchina kamuachia msuahili aendeshe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom