Startimes acheni wizi

Startimes acheni wizi

Le ngosha

Senior Member
Joined
Aug 1, 2018
Posts
107
Reaction score
104
Hii ni mara ya pili kujitokeza jukwaani nikiilalamikia kampuni hii kongwe ya ving'amuzi hapa nchini baada ya DSTV

Nimekua mteja wao tangu mwezi machi 2017 lakini kila kukicha nazidi kuboreka na huduma zao za kibabaishaji kv;

1:Kugoma kuonesha channel za ndani bure
2:Upandishwaji wa gharama za vifurushi vyao mara kwa mara

Nikijikita katika suala la pili jana asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kazini niliwasha wasafi tv ili nicheck Throw Back Thursday lakini tofauti na matarajio yangu baada ya kuangalia nyimbo kadhaa yalikuja maneno yaliyomaanisha kua siwezi kuendelea kuangalia channel hiyo [You are not subscibed to view this channel] hali hiyo ilinistua kwa sababu nililipia tarehe 07 ya mwezi huu wa Octoba ambapo kimsingi nilitakiwa kulipia upya tena tarehe 07 novemba.

Baada ya hapo niliamua kupiga simu huduma kwa wateja ambapo nilijibiwa kua muda wa kuhudumia wateja haujafika ni mpaka saa 1 asubuhi hadi saa 4 usiku,hivyo niliamua kuvuta subira nikisubiria muda ufike,ilipofika saa 9 alasiri niliwapigia ambapo nilijibiwa kua bei ya kifurushi cha nyota ni tsh 11000 na sio elfu 10000 hivyo kwa sababu nililipia tsh 10000 waliniweka kwenye mfumo wa malipo ya wiki,sasa hoja yangu inajikita kwenye mambo mawili

Mosi,ni kwa nini wabadili bei bila kuwataarifu wateja kwa sababu ningejua hilo kwa wakati ningelipia hiyo 11000 na sio 10000.
Pili,kwa nini upungufu wa tsh 1000 kwenye kifurushi cha nyota unikoseshe huduma siku 12 kabla ya muda?

USHAURI WANGU;boresheni vipindi vyenu na muongeze channel ziendane na ongezeko la gharama mnazochaji pia toeni taarifa mapema kunapokua na badiliko la bei.

Naomba kuwasilisha
 
Mkuu una maanisha nini? Kwamba zile channels za st/ zote zimetolewa?
 
ukiwa unaangalia channel utafikiri unaangalia cd inayosikrach ni king'amuzi cha hovyo.
 
Mbona ipo mkuu search channel zako upya.

Hawa jamaa hovyo kabisa wanabadilisha bei bila hata taarifa yoyote.
Ngoja nikajaribu Leo. Lakini Nimeona uzi hapa unaoelezea Kuhusu. ITV, EATV, na STARTV zimeondolewa kwenye kingamuzi cha startimes
 
Back
Top Bottom