Starseeds

Starseeds

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
STARSEEDS
1736185592308.jpg

Sehemu ya kwanza

Imeandaliwa na kuandikwa na Dogoli kinyamkela

🔴
"kipi kitakachomdhuru mtu Kama akiupoteza ulimwengu mzima lakini akaweza kuikoa nafsi yake"?.

🗣️Ulimwengu Wala haupo ilimradi upo, Ila umetengenezwa kwa mahesabu makali Sana, Lakini huu ulimwengu Ni Kama drama tu au Ni Kama mchezo wa kuigiza Kati ya Nuru na Giza ambao umekuwa ukichezwa katika uwanda husika.

✍️Lakini huu mchezo unachezwa katika Aina ambayo inaleta maana au uhalisia, Na huu Ni mchezo wa ulimwengu mzima.

💃Na kila nafsi Ina sehemu yake ya kuucheza mchezo huu, au kwa lugha fupi Ni kwamba kila nafsi Ina scene yake ya kucheza mchezo huu.

⚛️Zipo nafsi ambazo zimekuja duniani zikiwa zimetoka katika uwanda wa juu Sana, yaani hizo nafsi siyo za dunia hii na Wala siyo za Galaxy hii, Ila Ni kutoka katika Mfumo mwingine kabisa wa sayari tofauti na huu Mfumo wetu wa hizi sayari tuzijuazo.

🤷Hizo nafsi unaweza kusema ufalme wao siyo wa dunia hii, japo vitu vingi vipo kwenye mikono yao.

🚶Zimekuja duniani Kama kujitolea tu yaani Volunteers katika kipindi hiki Cha mpito, Kwa Nini Ni kipindi Cha mpito kwa sababu kila nafsi IPO katika kipindi Cha mpito kuelekea ufahamu ule ulio mkuu.

🤔Katika kuja duniani kwa ajili ya hiyo kazi zao ya kujitolea hizo nafsi baadhi yao zikajisahau kwa muda, yaani zikasahau uhalisia wao, zikasahau Asili yao, zikasahau zimetoka wapi na zimesahau zimekuja kufanya Nini duniani, Lakini siyo kujisahau moja kwa moja Ila Ni kwa muda tu na kipindi kitafika zitakumbuka kwamba zenyewe Ni za juu Sana.

🗣️Nafsi hizi zinaitwa Starseeds, yaani nafsi zilizowahi kuishi huko nyuma, Kwa kawaida Hawa au hizi nafsi zimetoka nje ya huu Mfumo wetu wa sayari.

✍️Unaweza ukarejea Ile dhana ya reincarnation au kufa na kuzaliwa upya, Nafsi za duniani zenyewe hufa na kuzaliwa Tena hapa hapa duniani, lakini Starseeds hizi nafsi zenyewe Ni Kama daraja Kati ya uwanda mwingine wa kiroho na duniani.

🤏Hizi nafsi zimeletwa kuja kuubadirisha ulimwengu, kwa ajili ya shughuli ambazo wamekuja kuzifanya, Hizi nafsi za Starseeds zenyewe Zina Ile hekima ya ndani, na pia wanakuwa na uwezo tofauti au uwezo wa ajabu lakini uwezo huo unakuwa umelala au uko dormant mpaka siku maalum ikifika Basi ule uwezo unaamka kwa Kasi kubwa na kuanza kufanya kile kilichomleta.

🗣️Lengo Lao kubwa Ni kuikoa jamii kutokana na kile ambacho wamekibeba ndani yao, Hizi nafsi zipo kwa ajili ya kuziamsha jamii kwa namba moja au nyingine ili ziweze Kufika viwango vya juu Sana vya muamko.

✍️Nafsi hizi zipo kwa ajili ya kutenda zile kazi Chanya, Japo zipo zingine ambazo Ni ovu na zinapingana na wenzao katika kuyatenda mema.

🤷Je kwa Nini zinapingana?
itaendelea

Ulikuwa nami mwalimu wako Dogoli kinyamkela
 
Back
Top Bottom