Stars yapoteza mchezo dhidi ya Swaziland

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya COSAFA Castel Cup dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland, baada ya kufungwa bao 1- 0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.

Stars ilipoteza nafasi zaidi ya tano kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake Saimon Msuva na nahodha John Bocco ambao walishindwa kukwamisha mpira wavuni katika kipindi cha kwanza, ambacho Taifa Stars ilicheza vizuri.

Swaziland walipata bao lao la kwanza na la ushindi dakika ya 42 ya mchezo, kupitia kwa mlinzi wa kulia Sifiso Mabila aliyepanda kuongeza nguvu ya mashambulizi na kuachia shuti lililouacha mlinda mlango wa Stars akikosa cha kufanya kuokoa mchomo huo.

Kipindi cha pili Stars walizidiwa kwani mashambulizi yao hayakua na madhara langoni mwa Swaziland na kumuacha mlinda mlango Mphikeleli Dlamnini akiwa likizo kwa muda mrefu.

Mara baada ya mchezo kocha wa Stars Mart Nooij alisema, amepoteza mchezo wa kwanza ambao alitegemea kupata ushindi, vijana walicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini bao la mapema lilionekana kuwapoteza mchezoni.

“Presha ya mchezo ilikua kubwa hasa kipindi cha pili, kutokana na vijana wangu kucheza kwa kusaka bao, huku Swaziland wakimiliki zaidi mpira na kukuta mipango yetu kutokua na madhara” alisema Nooi.

Akiongelea michuano ya COSAFA amesema anashukuru kwa kupata mwaliko huu, kwani kwake anatumia michuano hii kama sehemu ya maandalizi ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika (AFCON, CHAN) mwezi juni, huku akisema anaamini wachezaji aliowacha majeruhi nyumbani pamoja na wachezaji wa kimataifa wanaochezea klabu ya TP Mazembe, wataongeza nguvu katika kikosi chake watakaporejea Tanzania.

Baadhi ya watanzania waishio nchini Afrika Kusini walijitokeza uwanja wa Royal Bafokeng kuishangilia timu ya Taifa ya tanznaia Taifa Stars wakiwa sambamba na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili siku ya jumatano saa 11 za jioni kwa saa za Afrika kusini, sawa na saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki dhidi ya Madagascar katika uwanja wa Royal Bafokeng., ambao katika mchezo wa awali wamibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho.

Wakati huo huo kiungo wa Taifa Sars Said Juma “Makapu” ambaye anasumbuliwa na majeruhi, anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania leo kwa ajili ya kupata vipimo zaidi na matibabu.

TFF YATUMA RAMBIRAMBI RUREFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kufuatia kifo cha katibu mkuu msataafu wa chama hicho Adolph Choma aliyefariki jumamosi na kuzikwa jana.

Katika salamu hizo, TFF imesema inawapa pole familia ya marehemu Adolph Choma, ndugu jamaa na marafiki, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu nchini na kusema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

NB😛icha za mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Swaziland zimeambatanishwa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
 
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya COSAFA Castel Cup dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland, baada ya kufungwa bao 1- 0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.
Tulisahau kununua mechi ili Msuva afunge kirahisi
 
sema tu stars kama kawaida yake, yaendeleza. mtu anajua tu unaongelea nini.
 
Tulisahau kununua mechi ili Msuva afunge kirahisi
Kabla ya msuva hiyo starz yako ilifika wapi!!!
Zungumzia timu ya taifa kwa ujumla sio unaleta ushabik maandaz wa kimbumbumbu, kumbuka mpira wa miguu haupo kama mchezo wa tennis wa mtu mmoja mmoja, mpira wa miguu timu moja inakuwa na wachezaji 11, je, wachezaji wetu wa taifa starz ambao jana walipewa nafasi ya kutuwakilisha watanzania kila mmoja alitimiza wajibu wake!!!!!

Tusiwe kama wabrazil ambao walikula 7-1 kutoka kwa wajeruman huku akili zao zikiamin kuwa kama angalikuwapo Neymar wasingalifungwa goli 7.
 
Kama kuna kosa Malinzi atajutia ni kumfukuza Kim Poulsen bila sababu za msingi. Kamleta huyu jamaa wa ovyo kabisa. Mechi ya 14 hii madudu matupu.
 
Tulisahau kununua mechi ili Msuva afunge kirahisi

Ndiyo kwanza Msuva kacheza chini ya kocha huyo. Siku za nyuma ilikuwa vipi? Tatizo Stars imechanganya wachezaji wa kimataifa na wale wa mchangani a.k.a boti to Zanzibar. Inabidi wawe International wote.
 
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya COSAFA Castel Cup dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland, baada ya kufungwa bao 1- 0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.

Stars ilipoteza nafasi zaidi ya tano kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake Saimon Msuva na nahodha John Bocco ambao walishindwa kukwamisha mpira wavuni katika kipindi cha kwanza, ambacho Taifa Stars ilicheza vizuri.

Swaziland walipata bao lao la kwanza na la ushindi dakika ya 42 ya mchezo, kupitia kwa mlinzi wa kulia Sifiso Mabila aliyepanda kuongeza nguvu ya mashambulizi na kuachia shuti lililouacha mlinda mlango wa Stars akikosa cha kufanya kuokoa mchomo huo.

Kipindi cha pili Stars walizidiwa kwani mashambulizi yao hayakua na madhara langoni mwa Swaziland na kumuacha mlinda mlango Mphikeleli Dlamnini akiwa likizo kwa muda mrefu.

Mara baada ya mchezo kocha wa Stars Mart Nooij alisema, amepoteza mchezo wa kwanza ambao alitegemea kupata ushindi, vijana walicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini bao la mapema lilionekana kuwapoteza mchezoni.

"Presha ya mchezo ilikua kubwa hasa kipindi cha pili, kutokana na vijana wangu kucheza kwa kusaka bao, huku Swaziland wakimiliki zaidi mpira na kukuta mipango yetu kutokua na madhara" alisema Nooi.

Akiongelea michuano ya COSAFA amesema anashukuru kwa kupata mwaliko huu, kwani kwake anatumia michuano hii kama sehemu ya maandalizi ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika (AFCON, CHAN) mwezi juni, huku akisema anaamini wachezaji aliowacha majeruhi nyumbani pamoja na wachezaji wa kimataifa wanaochezea klabu ya TP Mazembe, wataongeza nguvu katika kikosi chake watakaporejea Tanzania.

Baadhi ya watanzania waishio nchini Afrika Kusini walijitokeza uwanja wa Royal Bafokeng kuishangilia timu ya Taifa ya tanznaia Taifa Stars wakiwa sambamba na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili siku ya jumatano saa 11 za jioni kwa saa za Afrika kusini, sawa na saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki dhidi ya Madagascar katika uwanja wa Royal Bafokeng., ambao katika mchezo wa awali wamibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho.

Wakati huo huo kiungo wa Taifa Sars Said Juma "Makapu" ambaye anasumbuliwa na majeruhi, anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania leo kwa ajili ya kupata vipimo zaidi na matibabu.

TFF YATUMA RAMBIRAMBI RUREFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kufuatia kifo cha katibu mkuu msataafu wa chama hicho Adolph Choma aliyefariki jumamosi na kuzikwa jana.

Katika salamu hizo, TFF imesema inawapa pole familia ya marehemu Adolph Choma, ndugu jamaa na marafiki, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu nchini na kusema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

NB😛icha za mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Swaziland zimeambatanishwa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER

Kwani Wewe Lini Timu Yetu Ya Taifa Stars Imeshinda Ikiwa Na Michezaji Mibovu Kama Ngasa, Msuva Na Oscar Joshua? Hivi Kocha Mwenye AKILI Timamu Ataweza Kweli Kuwaacha Wachezaji Kama Jonas Gerald Mkude, Ramazan Kessy Na Mohamed Hussein Tshabalala Na Jana Kuwaweka Nje Akina Ibrahim Hajibu Na Abdi Banda? Tena Ktk Mtu Aliyeshangilia Jana Timu Letu Kufungwa Ni Mimi Na Kesho Wala Samaki Wa Madagascar Wanaenda " Kutuchapa Nao " Tena.
 
Kwani huko SA hakuna magazeti na redio!? ...sisi taifa kubwa tunacheza mpira kupitia magazetini wakati Swaziland taifa dogo sana wanacheza mpira uwanjani. Wanaolielewa hili wala hawatakaa washangae matokeo haya!
 
Timu imejaa wachezaji wa Yanga unategemea nini hapo?

Kombe lenyewe wamechukua kwa mlango wa nyuma
 
Malinzi alikua hana sababu ya msingi kumfukuza Kim, walau mpira ulikua unaonekana
 
Back
Top Bottom