Ndio! hao ndio waandishi wetu wa mpira bongo!wanaijaza misifa mijitu isiyostahili!Kama tulivyopingwa na Kenya 1 - 0 wakaandika Stars yafa kiume'.Sasa wataripoti 'tumefungwa kishujaa' na Zambia! Wanatufanya kama watoto! Zigo lote la lawama watalielekeza kwa kocha! utasikia kafikia kikomo,hana jipya,si kocha kabisa!Watasahau kabisa zile sifa walizokuwa wanamjazia wakati Morocco wakilala 3 - 0 taifa!Lakini ni kweli makocha wote waliopita tukianza na Maximo, akaja Jan Poulsen na sasa Mzee Kim ambao records zao ni za viwango vya juu vya FIFA hawana jipya?
Tatizo lipo! Tatizo ni wachezaji wetu, lazima tukubali tunahitaji wachezaji wanaofahamu nini maana ya kuchaguliwa timu ya Taifa!Kuchaguliwa timu ya Taifa ni kwenda kupigana kwa ajili ya waTZ zaidi ya mil 40!ambao hatuwezi wote kuingia uwanjani!Utaalamu wa Mwalimu unauongezea na Juhudi,Jihadi ya machozi,jasho na damu!!
Sasa mchezaji akishachaguliwa anabadilika!wengine wanasuka nywele,wengine wanazipakaza nywele rangi,wengine viduku utafikiri wanaenda ndombolo!!wengine utafikili disco joker!!! Nahodha anahojiwa anajibu 'tunaenda kushinda kama kusukuma mlevi!! aaaaarggh!wewe umejiandaa hadi useme ivyo? Malinzi lazima kuiangalia timu hii kwa jicho la tatu! WaTz tunaumia! wafadhili wanaumia pia!....nawasilisha!!