Stars Wafa Kiume!..waandishi wetu bwana!!

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
981
1,344
Ndio! hao ndio waandishi wetu wa mpira bongo!wanaijaza misifa mijitu isiyostahili!Kama tulivyopingwa na Kenya 1 - 0 wakaandika Stars yafa kiume'.Sasa wataripoti 'tumefungwa kishujaa' na Zambia! Wanatufanya kama watoto! Zigo lote la lawama watalielekeza kwa kocha! utasikia kafikia kikomo,hana jipya,si kocha kabisa!Watasahau kabisa zile sifa walizokuwa wanamjazia wakati Morocco wakilala 3 - 0 taifa!Lakini ni kweli makocha wote waliopita tukianza na Maximo, akaja Jan Poulsen na sasa Mzee Kim ambao records zao ni za viwango vya juu vya FIFA hawana jipya?
Tatizo lipo! Tatizo ni wachezaji wetu, lazima tukubali tunahitaji wachezaji wanaofahamu nini maana ya kuchaguliwa timu ya Taifa!Kuchaguliwa timu ya Taifa ni kwenda kupigana kwa ajili ya waTZ zaidi ya mil 40!ambao hatuwezi wote kuingia uwanjani!Utaalamu wa Mwalimu unauongezea na Juhudi,Jihadi ya machozi,jasho na damu!!
Sasa mchezaji akishachaguliwa anabadilika!wengine wanasuka nywele,wengine wanazipakaza nywele rangi,wengine viduku utafikiri wanaenda ndombolo!!wengine utafikili disco joker!!! Nahodha anahojiwa anajibu 'tunaenda kushinda kama kusukuma mlevi!! aaaaarggh!wewe umejiandaa hadi useme ivyo? Malinzi lazima kuiangalia timu hii kwa jicho la tatu! WaTz tunaumia! wafadhili wanaumia pia!....nawasilisha!!
 
Unatarajia nini iwapo ligi yetu zinacheza pesa za manji?Usitarajie timu ya taifa kufanya vizuri kama yanga ndio vinara wa ligi.Fanya utafiti!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwa mwendo huu hata tukifanikiwa kumshawishi Mzee Fugerson aje kufundisha au hata tukimleta Wenger au tuseme Mourhino akae na hili li timu!baada ya mwaka au miwili tutarudi na kauli hizi hizi za kocha gani?hana jipya!mbabaishaji etc!
Tatizo michezaji yetu kutojituma tumelifumbia macho!!We umefungwa ya Dk 6 bao la mapema! una Dk 84 unashindwa kugomboa bao!!eti tunalaumu kocha kafanya sub mbaya! Timu zimeshawahi kufanya maajabu watu wapo pungufu na mabao yanarudi! Na penalti mijitu yote inakosa hatuioni bali tunamuona kocha!!!
 
Wachezaji hawajitambui,pia hawajui thamani ya jezi ya timu ya Taifa,viongozi wa virabu waache kununua mechi.
 
Tatizo waandishi wanafuata upepo wa wasomaji
Sadakta. Mwandishi huyohuyo anamsifia mwalimu huyohuyo leo, kesho yake mwalimu huyohuyo anakuwa si malikitu kwa kalamu ya mwandishi huyohuyo. Natamani ifike siku tuwe na waandishi waliohitimu fani hiyo, sambamba na kuhitimu fani wanayotaka kuiripoti. Ndivyo wanavyopatikana waandishi mahiri. Huwa hawana upande wa kisiasa wala timu ya kimpira. Upande wao ni taaluma yao kwenye fani hizo mbili.
 
kitu kikubwa Nilichojifunza seminarini na baadae chuo kikuu kupitia maandishi ya plato,aristotle,thomas aquinos,karl max ni jambo la kukemea society bila woga, kwakweli sioni cha kujivunia kutoka kwa vijana wetu wa Kilimjaro stars, Maulidi wa Kitenge jana pia ameongea kwa uchungu sana hatuna cha kujivunia kutoka kwenye hii timu, inapaswa kuvunjwa mara moja na tuachane na usimba na uyanga hawa wachezaji vijeba wa yanga na simba hawana jipya kabisa!! tuanze kutengeneza timu from the grassroot.

nithubutu kusema sisi watanzania Shindano tunaloliweza ni mtani jembe na viroba! Cecafa ina wenyewe hilo halina ubishi.
Lakini sio mbaya hao kina ngassa na wengineo wameweza kuonesha mitindo ya nywele, kucheza kiduku, kutalii jiji la Nairobi na walau mmefunzwa jinsi gani mpira huchezwa. mtu anapiga penalt kama yupo mazoezini
Jichwa la mwendawazimu( alijisemea mzee wetu Mwinyi)
 
Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana. Tunataka mafanikio ya haraka bila kuwa na mipango madhubuti. Tunalaumu kila kitu na kila mtu lakini hakuna anayekosoa mipango na mikakati yetu ya kukuza viwango vya wachezaji wetu.

Kwa viwango vyovyote timu ya Kilimanjaro Stars, imefanya vzr kulinganisha na uwekezaji unaofanyika kwao. Tukubali viwango vya wachezaji wetu ni vya kawaida na vingine ni vidogo kabisa. Makocha wanajitahidi kadri ya uwezo wao lakini sioni jitihada ya wachezaji na vilabu vyetu kuinua viwango vyao. Unakuta mtu ana kiwango kilekile kwa miaka nenda miaka rudi.

Kwa mfano Salum Abubakari anapiga pasi zilezile, tabia za ndani ya uwanja zilezile, anapata kadi zilezile na hadi mpira utamuishia akiwa na kiwango kilekile. Ndivyo ilivyo kwa wachezaji wengine kama Erasto Nyoni, Kiemba na hata Yondani ataendelea kubutua mipira hadi atakapostaafu. Hakuna anayeonyesha kutaka kuwa bora zaidi, si wachezaji, si vilabu, si uongozi wa mpira, na hata sisi mashabiki ni matatizo matupu. Wachezaji wenye shauku ya kukuza viwango kama Ivo Mapunda na akina Thomas Ulimwengu ni wachache.

Nadhania tatizo letu jingine kubwa kwa sasa ni kuwa na timu ya taifa ya wachezaji wanaocheza ndani ya nchi mabapo ligi yetu bado haijatusaidia sana kutengeneza wachezaji wazuri. Hebu angalia mchango wa wachezaji wetu wanaocheza nje ya nchi kama Samatta, Ivo, Ulimwengu ni mkubwa mno. Kwa hiyo kwa kuanzia, ni lazima tuwalazimishe wachezaji wetu wazuri watoke nje na sio lazima waende Ulaya. Waanzie nzhi za Afrika Mashariki na kati na Afrika kwa ujumla.

Tatizo letu jingine kubwa ni kutokuwa na mikakati ya muda mrefu kama nchi ya kuandaa timu za kushindana. Kwa mfano, COSAFA kuna mashindano yanaendelea ya timu za taifa under 20. Sisi hatujaomba kushiriki wakati Kenya wameingia fainali pia, watakayocheza na SA. Masindano ya Afrika yatkapoanza sisi tutakurupuka labda angalau tutapata mechi moja ya kimataifa ya kirafiki halafu tutaingia mashindanoni ambako tutatolewa ktk raundi za awali na kisha maisha yataendelea na makocha wataonekana hawafai.

Timu ya wanawake chini ya miaka 20 Tanzanite Stars ni nzuri sana licha ya kufungwa 4-1 nyumbani na SA. Ni vijana wenye vipaji na umri mdogo sana wengi wao btn 16- 18! Hawa wakitunzwa na kuendelea kupata mechi na timu bora za Afrika watakuwa moto wa kuotea mbali ktk miaka michache ijayo. Lkn najua baada ya kutolewa na SA wiki ijayo, watasahaulika hadi mashindano mengine yatakapotangazwa ndio watakusanywa tena na kushiriki.

Yaani tabia na viwango vya wachezaji zilezile, viongozi yaleyale, mashabiki vilevile isipokuwa wanaobadilika ni makocha tu. Tujitazame upya.
 
Ndio! hao ndio waandishi wetu wa mpira bongo!wanaijaza misifa mijitu isiyostahili!Kama tulivyopingwa na Kenya 1 - 0 wakaandika Stars yafa kiume'.Sasa wataripoti 'tumefungwa kishujaa' na Zambia! Wanatufanya kama watoto! Zigo lote la lawama watalielekeza kwa kocha! utasikia kafikia kikomo,hana jipya,si kocha kabisa!Watasahau kabisa zile sifa walizokuwa wanamjazia wakati Morocco wakilala 3 - 0 taifa!Lakini ni kweli makocha wote waliopita tukianza na Maximo, akaja Jan Poulsen na sasa Mzee Kim ambao records zao ni za viwango vya juu vya FIFA hawana jipya?
Tatizo lipo! Tatizo ni wachezaji wetu, lazima tukubali tunahitaji wachezaji wanaofahamu nini maana ya kuchaguliwa timu ya Taifa!Kuchaguliwa timu ya Taifa ni kwenda kupigana kwa ajili ya waTZ zaidi ya mil 40!ambao hatuwezi wote kuingia uwanjani!Utaalamu wa Mwalimu unauongezea na Juhudi,Jihadi ya machozi,jasho na damu!!
Sasa mchezaji akishachaguliwa anabadilika!wengine wanasuka nywele,wengine wanazipakaza nywele rangi,wengine viduku utafikiri wanaenda ndombolo!!wengine utafikili disco joker!!! Nahodha anahojiwa anajibu 'tunaenda kushinda kama kusukuma mlevi!! aaaaarggh!wewe umejiandaa hadi useme ivyo? Malinzi lazima kuiangalia timu hii kwa jicho la tatu! WaTz tunaumia! wafadhili wanaumia pia!....nawasilisha!!
tatizo ni mfumo wa soka hapa nchini
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom