Starehe za bure, hatari sana!

Secret Star

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
1,845
Reaction score
2,058
Nguruwe ndiye mnyama pekee shambani ambaye hafanyi kazi; anakula bure, analala bure, Matibabu Bure, usafi bure na anaishi kwenye joto. Nguruwe akimtazama mfugaji na anafikiria 'Huyu binadamu ananipenda sana, yeye ndiye mungu wangu, ananipa kila kitu ninachohitaji.'

Lakini kile ambacho nguruwe hajui ni kwamba kile chakula si zawadi, bali ni uwekezaji. Hawamlishi, bali wanamvizia wanamsubiri anenepe. Siku ambayo nguruwe anakuwa amenenepa zaidi na mwenye furaha kuliko wakati wowote, ndiyo siku hiyo hiyo mfugaji anachukua Rungu na kunoa kisu chake.

Benki na mifumo mingine ya kifedha duniani inafanya kazi hivyohivyo. Wanakupa kadi za mkopo, mikopo ya mashart nafuu, na starehe ili utumie pesa. Hawakusaidii uishi vizuri, bali wanakunenepesha kwa madeni ili waweze kukufaidi vizuri.

Kama kitu ni cha bure na kinakupa starehe kupita kiasi, kuwa mwangalifu; kuna uwezekano mkubwa wewe ndiye bidhaa iliyo kwenye menyu. Acha kula ndani ya mabanda yao.

Wayahudi walijifunza hili karne nyingi zilizopita: Kitu kikionekana kama ukarimu kutoka kwa mtu au mfumo. Tegemea kwamba Nyuma ya pazia wanapata faida kupitia wewe, huo si ukarimu ni mbinu (strategy).

Wanataka uwe na starehe, Ubweteke ulale usingizi wa pono kwenye banda lao. kwa sababu wakati utakapozinduka na kuacha kukopa, utaacha kuwatajirisha."


 
Your browser is not able to display this video.
 
Benki na mifumo mingine ya kifedha duniani inafanya kazi hivyohivyo. Wanakupa kadi za mkopo, mikopo ya mashart nafuu, na starehe ili utumie pesa. Hawakusaidii uishi vizuri, bali wanakunenepesha kwa madeni ili waweze kukufaidi vizuri.📍📍📍📌
 
Mimi napenda shwaini wa kuchoma sio wa kukaanga
 
Nimelia sana , kwa nini nguruwe na sio mbuzi 😀 😀
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…