Star tv yageuka kero kwa watazamaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Star tv yageuka kero kwa watazamaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Baba Tina, Feb 3, 2011.

 1. B

  Baba Tina Senior Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thursday, February 03, 2011
  Wana jamvi napenda kutumia muda huu kuelezea masikitiko yangu kuhusiana na suala la tatizo la sauti ambalo sasa linaelekea kuota mizizi na kua kero kwa watazamaji wake wanaofuatilia vipindi mbalimbali hasa vipindi vya tuongee asubuhi na taarifa za habari.

  Kitu kinachosikitisha zaidi ni pale tatizo hilo la sauti linapotokea na watangazaji wa vipindi husika wakiendelea kuendesha vipindi na kuwaacha watazamaji wakiangalia picha ya muendesha kipindi bila kusikia sauti ya kile kinachozungumzwa. Tatizo hili si geni star tv lakini sasa imefika wakati watazamaji tumechoka na inabidi tuondoe dukuduku letu.

  Natambua kuwa matatizo ya kiufundi wakati mwingine haya epukiki na yanakua nje ya uwezo na yamekua yakitokea hata katika vituo vingine vya televisheni lakini tumeshuhudia matukio hayo yanapotokea katika vituo vingine vya televisheni mafundi wanawahi kuondoa picha hiyo na kuweka matangazo wakati wakiendelea kurekebisha mitambo na mambo yakiwa sawa wanaendelea na kipindi. Suala hili na nadra sana kutokea star tv.

  Kitu ninachojiuliza ni kwamba inakuwaje tatizo hilo linapotokea STAR TV mafundi wanashindwa kufanya marekebisho na kuacha watazamaji wakiendelea kuangalia picha ya muendesha kipindi bila kusikia maneno yanayo zungumzwa?? Au star tv haina mafundi wa sauti, au pengine mafundi wao wana uwezo duni. Jibu wanalo star tv wenyewe.

  Kinachosikitisha zaidi mara nyingi tatizo la sauti linapotokea mwendesha kipindi huendelea na kipindi kama vile hakuna tatizo lililotokea. Kwa mfano, kama taarifa ya habari inasomwa na tatizo la sauti likatokea basi habari hiyo itaendelea bila sauti na ikimalizika habari hiyo mtangazaji anaendelea na habari nyingine bila maelezo yoyote! Ina maana mtangazaji huyo anakua hajui kama sauti haitoki???

  Kwa wale walioangalia kipindi cha tuongee asubuhi leo alhamisi ambapo viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) walialikwa wameshuhudia jinsi Rymondi Nyamhula alivyokua akizungumza kwa muda mrefu bila yeye wala mafundi kujua kwamba sauti haitoki mpaka pale watangazaji waliokua Dar es Salaam walipoligundua tatizo na wao kuendelea na mjadala na kumuondoa hewani. Walau kwa leo waliomba radhi japokua bado waliiacha picha hewani kwa muda mrefu.

  Taarifa ya habari ya leo usiku pia ilikua inaboa kwa sababu sehemu kubwa ya habari iliyosomwa leo sa mbili usiku haikua na sauti. Wale walioangalia habari leo usiku wameshuhudia msoma habari Jacob Marcus akiendelea kusoma habari japokuwa mara nyingi sauti yake au ya reporter ilikua haisikiki kabisa. Kila alipomaliza kusoma habari moja aliendelea kusoma habari nyingine kimyakimya na kutuacha watazamaji hewani.

  Naamini star tv ni moja kati ya vituo vya televisheni ambavyo vimejijengea heshima kubwa hapa nchini kwa kua na vipindi bora na mijadala mizito yenye tija kwa taifa lakini wanapoendelea kufumbia macho tatizo hili la sauti wanajivunjia heshima waliyojijengea kwa watazamaji.

  Nawashauri star tv wafanye hima kushughulikia tatizo hilo kwani sasa limekua kero kubwa kwa watazamaji. Star tv wawakumbushe mafundi wao wanaohusika na sauti waamke usingizini na watimize wajibu wao ipasavyo ili kuendelea kukijengea heshima kituo hicho cha televisheni. Wawe makini kurekebisha tatizo linapotokea mapema na sio kutuachia picha isiyokua na sauti.

  [FONT=&quot]Nawasilisha:[/FONT]
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, hususan jana kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku na baadaye FUTUHI.
  Mimi huwa najiuliza, inakuwaje CNN,BBC,ALJAZEERA, SABC, SUPERSPORT, SKY NEWS etc...huwa hawana mambo kama yatokeayo kwetu Tanzania kwa kila mara (tunaomba radhi ni matatizo ya kiufundi yamejiri), inamaana bado hawajapata solution ya hayo matatizo ambayo ni kama wameshayatambua???
  Sio star tv tu, ni vituo vyote mpaka kile tunachokilipia kodi TBC1.
   
 3. B

  Baba Tina Senior Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini star tv wamezidi halafu mara nyingi tatizo hilo linapotokea hawajali wanaendelea na kipindi kana kwamba hakuna tatizo lolote. Bora wengine tatizo likitokea wanawahi kuweka matangazo na kurekebisha. Sijui kama kuna mtangazaji wa star tv ambaye hajawahi kututangazia hewa. Wote kuanzia jacob marcus, hilal ryami, mukhsin mambo, tom chilala, barhan muhuza na wengine kibao. Star tv jirejebisheni MNATUBOA SANA TU.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  hiyo station si inamilikiwa na yule kada wa ccm??kipindi chao cha magazeti asubuhi ni upuuzi mtupu,..uhuru,mzalendo,rai,mtz,habari leo,..bora kiungue kabisa
   
 5. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  si swala la sauti tu hata ratiba zao zinakera, unaweza kujua saa nne kuna tamthilia fulani, ikifika saa nne wanakuomba radhi!! Haipendezi
   
Loading...