Ccm wanakuja na mtu mpya, tunaelewa wapiga kura wengi hawaelewi tofauti kati ya kubadili uongozi na chama, so long ni mtu mpya kutoka ccm wengi watadhani mabadiliko tayari, hii itapunguza kura za mgombea wa ukawa na hasa ikiwa mtu huyo siyo mpya eg slaa, lipumba, etc, etc.
Sitaki nieleza details lakini kwa kifupi ni kuwa suala la imani za dini mbalimbali lina ushawishi mkubwa katika uelekeo wa kupiga kura na hasa km katikati kuna propaganda za kisiasa, hivyo ukimsimamisha lipumba kura zitapungua kwa wakristo kujazwa propaganda kwamba ni zamu yao, ukimsimamisha slaa kura zitapungua sana kwa propaganda za upadre na ukatoliki.
Way forward:
1. Leteni sura mpya kwa ajili ya wale ambao kwao upya wa mtu ni deciding factor
2. Leteni mtu ambaye hawezi kuhusishwa na imani ya dini ili ku neutralise propaganda za dini
3. Leteni mtu maarufu kwa ajili ya wale ambao kufahamika kwa mtu ni kigezo cha kumpigia kura
4. Leteni mtu ambaye hajatoka kaskazini kwa ajili ya ukweli kwamba ndani ya ukawa cdm ina nguvu hivyo tutaweze kuua propaganda za chama watu wa kaskazini
5. Nampendekeza Tundu Lissu, ana weaknesses zake lakini ni msomi, mpiganaji mkubwa wa masilahi ya taifa, popular, umri wa kati na zaidi ameonesha uwezo wa kuifuta ccm jimboni kwake.
Naomba nieleweke ya kuwa ndani ya ukawa kuna wengi tu wenye uwezo lakini tunachopaswa kuangalia ni nani ataleta kura za kutosha ambayo ccm itafikiri mara mbili kabla hawajaamua kuiba kura