Star Tv mnatoa habari ndivyo sivyo

Star Tv mnatoa habari ndivyo sivyo

Mashimba1

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
814
Reaction score
303
Wanajamvi, kutokana na kile kinachofanywa na chombo hiki cha habari ku-promote ujinga hasa ktk kipindi hiki cha mchakato wa kutafuta katiba mpya, ninatangaza rasmi kutopoteza muda wangu kuangalia star tv.
 
Mkuu umechelewa sana kulijua hilo hatimaye kufanya uamuzi huo, mmiliki wa star tv ni m/kiti wa ccm mkoa wa mwanza hawezi kwenda kinyume na chama chake! Sisi kituo cha televisheni cha umma ni Itv karibu mkuu.

BACK TANGANYIKA
 
Ngoja nami nijiridhishe kabla ya kuiweka kwenye kapu la tbc
 
Nimefatilia leo habari za Star tv, sio siri nimeghafirika sana. Au na nyie -----------? Nimeona mmeweka habari za kuwaponda UKAWA , hiyo siyo haki hata siku moja. Mnaongelea UKAWA zanzibar hapo hapo mnachanganya na kada wa cccm, je mlitegemea kada wa cccm wasemeje? Acheni kutoa habari kwa upendeleo, huo ni utovu wa nidhamu na kushindwa kusimamia taaluma zenu. Nimefatilia ya Singidanayo naona mambo ni yaleyale, yaani hadi najuta kuitazama hii tv, na mkiendelea nitaihama kama pacha wenu tbccccm...hovyoooòoooooooooooooo
 
Mutahama kila TV,mpaka muache UKANDA na UBAGUZI kudadadeki!!!CDM mumekivunja kwa mikono yenu.
 
Nimekuwa nikifuatilia sana taarifa ya Habari ya saa mbili usiku kupitia Star TV kwani Kisimbuzi ninachotumia kina local channels 3 tu. Kwa siku za karibuni nimegundua mabadiliko makubwa sana hasa kwenye habari zinazosomwa. Habari za CCM zimetawala sana yani ni kila siku. Ni mara chache sana utaona habari za vyama pinzani na zikiwepo zinakuwa mda mfupi tu. Hasa kipindi hiki UKAWA walivyotoka bunge la katiba,basi Star TV wamekuwa wakitumika sana kudhoofisha harakati zinazofanywa na UKAWA. Mlioangalia habari leo mtakubaliana nami.
 
Hivi ni TV gani nzuri kwenu? Mnataka kila TV ziwaonyeshe UKAWA wakilia lia baada ya kususa bunge?
 
...ukombozi wa tanganyika unahitaji ukombozi wa fikra kwa watu wengi hasa wanaorubuniwa na ccm kuwa ukijiunga na ccm mambo yatakunyookea.,.
 
Leo nimewachoka kabisa star tv.kama dotto ni mzalendo aondoke.
 
Mkuu kwanza pole sana, Pili Star Tv ni chombo binafsi sio cha umma hivyo wana haki ya kufanya watakavyo. Tatu ni bora ukafungua kituo chako kikawa kinapromote werevu, na nne kwa kuzingatia namba mbili hutakaa tena upost -----!!
 
Kwa kweli binafsi sijapenda taarifa ya habar ya leo,full ccm tu,wamewatafuta wananchi wachovu zanzibar wawaponde UKAWA ,napata shda ni lini watanzania wataamka,mfano chadema,cuf na hata vyama vingne vikichoka kuleta ukombozi.nan atasimama kwa ajar ya wanyonge.
 
Nimefatilia leo habari za Star tv, sio siri nimeghafirika sana. Au na nyie -----------? Nimeona mmeweka habari za kuwaponda UKAWA , hiyo siyo haki hata siku moja. Mnaongelea UKAWA zanzibar hapo hapo mnachanganya na kada wa cccm, je mlitegemea kada wa cccm wasemeje? Acheni kutoa habari kwa upendeleo, huo ni utovu wa nidhamu na kushindwa kusimamia taaluma zenu. Nimefatilia ya Singidanayo naona mambo ni yaleyale, yaani hadi najuta kuitazama hii tv, na mkiendelea nitaihama kama pacha wenu tbccccm...hovyoooòoooooooooooooo

mwenyewe wamenishangaza sana eti Ukawa wawaeleze Wanzibar kilicho watoa nje ya bunge sijui habari zao wanampendezesha nani
 
Ndio maana RFA imetoka kwenye ramani ya radio tata bongo kwa ajili ya upuuzi huu, na TV yao isubiri hilo.
 
mnataka ANTONY akose tena ubunge 2015???
 
Back
Top Bottom