Waungwana,
Mimi binafsi nimekuwa nikifatilia mijadala mingi na yenye tija kwa taifa hili kupitia luninga ya Star, ambapo baadhi ya mijadala hiyo nimepata kuchangia.
Ninadhani sasa,, ya kwamba iwafikie waendeshaji wa kipindi hicho cha TUONGEE ASUBUHI kwamba watujulishapo juu ya mjadala/midahalo wakusudiayo kuirusha hewani siku hiyo ya j2 basi itapendeza zaidi kama wawe wanatupa taarifa humu jamvini walau 5-days kabla ya kipindi ili kama wanahitaji michango TULIVU na yenye TIJA toka humu iweze kuwasaidia na kuisaidia jamii kiujumla.
Tutoapo michango kwa 1/2/3-days before wengine huwa hatuna utulivu wa kuchambua/kunyambua vema na kujenga hoja nzuri, na badala yake huwa tunatoa michango ya papo hapo while huenda ni topic yenye ujenzi kwa taifa na jamii kiujumla.
Naomba kuwasilisha na iwafikie wadau hao nguli wa tasnia ya habari nchini.
Mkuu habari za Tosamaganga au Tanangozi au Ipogolo??????? hiyo red mkuu...SAFI IKO POA SANA HATA MiMI NAIFUATILIAGA
Waungwana,
Mimi binafsi nimekuwa nikifatilia mijadala mingi na yenye tija kwa taifa hili kupitia luninga ya Star, ambapo baadhi ya mijadala hiyo nimepata kuchangia.
Ninadhani sasa,, ya kwamba iwafikie waendeshaji wa kipindi hicho cha TUONGEE ASUBUHI kwamba watujulishapo juu ya mjadala/midahalo wakusudiayo kuirusha hewani siku hiyo ya j2 basi itapendeza zaidi kama wawe wanatupa taarifa humu jamvini walau 5-days kabla ya kipindi ili kama wanahitaji michango TULIVU na yenye TIJA toka humu iweze kuwasaidia na kuisaidia jamii kiujumla.
Tutoapo michango kwa 1/2/3-days before wengine huwa hatuna utulivu wa kuchambua/kunyambua vema na kujenga hoja nzuri, na badala yake huwa tunatoa michango ya papo hapo while huenda ni topic yenye ujenzi kwa taifa na jamii kiujumla.
Naomba kuwasilisha na iwafikie wadau hao nguli wa tasnia ya habari nchini.
'' Kwa nini watanzania wananyimwa fursa ya kuwa na Nishati ya uhakika ya Umeme'' IJUMAA WIKI HII - 24.12.2010
Muongozaji,
Taifa letu hili ni changa na lenye changamoto lukuki katika ukiaji wake, tunazo changamoto hasi na chanya.
nadhani ifike wakati sisi wananchi wa kawaida tuangaliwe vema na wakuu wetu wa nchi,
- Taifa halina misingi/mipango endelevu juu ya janga hili la umeme.
- Taifa haliwezi kusonga mbele kimaendeleo pasipokuwa na nishati kamilifu na yenye kuvutia hata wawekezaji.
- Kwa nyakati tofauti taifa limeshuhudia tatizo la nishati bila ufumbuzi wa kudumu, tunarithisha tatizo hili kwa vizazi pasipo kulitafutia ufumbuzi yakinifu.
- Nishati ya umeme inadidimiza wananchi kwa kushindwa kuendeleza hali zao za ujasiriamali na kukuza uchumi wa taifa letu.
- Maendeleo yahitaji nishati, hapa namaanisha maendeleo ya rasilimali watu-KIELIMU, maendeleo ya nchi-KIVIWANDA etc,,vyote vyategemea nishati hii adhimu ya umeme. kinyume chake kumekuwa na mipango mibovu na isiyo na dira ya janga la umeme kuwa ni historia walau tu kwa kizazi hiki.
- Katika kipindi hiki cha mitikisiko ya uchumi duniani, tungetegemea kutoweza kuona janga la umeme kuikumba nchi yetu...bali matokeo yake tumeruhusu kuuyumbisha uchumi wa nchi tena kwa tatizo la nishati.