STAR TV inafunika TBC

dah, hata me huwa namkubali sana huyu baba. huwa anatoa habari kwa uhakika na masimulizi yake yanaeleweka. hongera zake!


Namkubali Samadu Hassani Lakini nadhani Doto Bulendu hakika nikivutio tosha hasa akiwa anaongoza kipindi cha tuongee asubuhi

Jicho letu ndani ya habari au ndani ya siasa Jmosi au Jpili utampenda mjadala huwa wa wazi sana. Big up Star TV.
 
Jamani mimi ninampenda sana samadu hassan katika anga za kimataifa 'kuvunjika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi pangu pakavu ntilie mchuzi' uko juu babaangu!

Kwa kweli Samadu Hassan anajua kupangilia habari za kimataifa,habari inakuwa na ladha ya kufuatilia
 
Umekosea sana kujaribu kuifananisha Star TV na hicho ki channel cha ccm!
 
Mitangazaji ya TBCCM ukiitazama tu utauona unafiki ulivyo dhahiri nyusoni mwao, utagundua wanafanya kazi kimaelekezo kabisaaaaa.

yaani kila wakati wanaogopa kukosea maagizo, wanajituma kushabikia ccm ili kulinda viajira vyao vya upendeleo.

naunga mkono hoja mkuuuu unafki 2
 
Huo ndiyo ushindani. Kila kituo kina sera na madhumuni yake kuna wengine wapo kibiashara zaidi na wengine kutumbuiza zaidi na wengine ustawi wa jamii zaidi. Mtazamaji ana wigo wa kuchagua na kama wewe unaona star tv ni bora kuna wengine huwaondoi clouds
 
....TBC ananiacha hoi yule (sijui mama sijui daa) Gloria Bondo kwenye chereko...."mzungu"

naangaliaga wale mabiarusi wanavyohojiwa...huwa nacheka sana maana some of them wanajishaua kupita maelezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…