Stand ya mkoa kuhamishiwa tegeta.

Stand ya mkoa kuhamishiwa tegeta.

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
832
Kuna habari nimezipata leo kwenye daladala kuwa stand ya mabas ya mkoa inahamishiwa tegeta,swali mbona imehamia mbezi?ni kwa muda au? Ni vigezo gani wametumia kuhamisha hii stand hapo ubungo? Hakuna kaufisadi kweli? Nijuavyo mimi terminal haiwi nje ya mji,inakuwa center kwa ajili ya wakazi wote wa jiji, ubungo wanaweka nini?
 
mabasi yatakayokuwa yanatokea mikoa ya kaskazini standi yao itakuwa tegeta boko.......na yatakuwa yanatumia new bagamoyo road mpaka kufikia msata na yataendelea na safari kuelekea kaskazini.

kwa mabasi ya mikoa ya kati na kusini yatakuwa yanatumia standi ya mbezi na yatatumia morogoro road
 
mkuu unaonekana upo mbali sana na ulimwengu wa habari!
 
kumbe ni udaku wa kwenye daladala?? haya mambo hakuna ajuaye ukweli wake ni umbea tu uliozagaa lkn sijawah kumskia waziri husika akiyasema haya.

so far mbezi ni stand ya daladala na mabasi na ni kwaajili ya kuakia na kushusha tu ila sio stand kubwa kama ilivyo ubungo manake haina ofc wala nn.
 
inawezekana mabasi yameamishiwa huko; mi natumia hii barabara Ubungo to Kibaha kila siku lakini kuanzia jumatatu mpaka leo hii siona Basi nilizozoea kupishana nazo kila siku asubuhi katika hii njia zaidi ni Coaster na Malori ya Michanga:

Swali langu kwamba, kama stendi imeamishwa mamlaka usika inashindwa nini kuutangazia umma mabadiliko yaliyopo??. Ni hatari kwa maisha ya wanaosafiri.
 
Hili ni tatizo la Watanzania wengi. Huwa hawafuatilii taarifa mbali mbali kwenye vyombo vya habari. Nafikiri jambo hili limekua linatangazwa tangu mwaka jana kwenye vyombo vya habari na sababu ya kufanya hivyo. Hata JK aliwahi kuongelea wakati anaweka jiwe la msingi la mradi wa DART. Sasa mwenzetu ulikua unasoma magazeti ya udaku na kusikiliza bongo fleva, kwenye radio mfululizo halafu unaleta unayoyajua wewe. Kwani jiji umeona lipo Ubungo tu.
 
Kuna habari nimezipata leo kwenye daladala kuwa stand ya mabas ya mkoa inahamishiwa tegeta,swali mbona imehamia mbezi?ni kwa muda au? Ni vigezo gani wametumia kuhamisha hii stand hapo ubungo? Hakuna kaufisadi kweli? Nijuavyo mimi terminal haiwi nje ya mji,inakuwa center kwa ajili ya wakazi wote wa jiji, ubungo wanaweka nini?

Ni kweli ma bus yanayo toka tanga, arusha yote stand ina hamia boko pale dawasco na eneo tayar limeshatengwa
 
mabasi yatakayokuwa yanatokea mikoa ya kaskazini standi yao itakuwa tegeta boko.......na yatakuwa yanatumia new bagamoyo road mpaka kufikia msata na yataendelea na safari kuelekea kaskazini.

kwa mabasi ya mikoa ya kati na kusini yatakuwa yanatumia standi ya mbezi na yatatumia morogoro road
Kama hii ni kweli basi nadhani itasaidia sana kupunguza msongamano wa magari hasa MOROGORO ROAD....
 
Ni kweli. Stand ya Mkoa imeshaanza kubomolewa kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi.

Kwa mabasi yaendayo Kaskazini, stand itakuwa Boko, na kwa yale ya nyanda za juu itatumika stendi ya daldala ya Mbezi.

Mabasi ya kaskazini hayatalazimika kupita Chalinze, badala yake yatapita njia ya Msata/Miono.

Shida niiionayo ni ukurupukaji wa serikali. Tonnage ya lami iliyowekwa stendi ya daladala ya mbezi itahimili uzito wa mabasi yenye kubeba tani zaidi ya 20 hali ilijengwa kwa ajili ya daladala?
 
mkuu unaonekana upo mbali sana na ulimwengu wa habari!

wewe ndo huelewi,kituo cha mabasi ya mkoa walipanga kiwe mbezi,,kupeleka boko ni uhaini,na kituo cha mabasi ya kasi kwa ajili ya nani? Kwa nini wasingekiweka kibaha? Ili kurahisisha usafiri wakuja kwetu mbagala,tatizo ni serikali.
 
Ni kweli. Stand ya Mkoa imeshaanza kubomolewa kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi.

Kwa mabasi yaendayo Kaskazini, stand itakuwa Boko, na kwa yale ya nyanda za juu itatumika stendi ya daldala ya Mbezi.

Mabasi ya kaskazini hayatalazimika kupita Chalinze, badala yake yatapita njia ya Msata/Miono.

Shida niiionayo ni ukurupukaji wa serikali. Tonnage ya lami iliyowekwa stendi ya daladala ya mbezi itahimili uzito wa mabasi yenye kubeba tani zaidi ya 20 hali ilijengwa kwa ajili ya daladala?

Hapo ndipo nilipoona kuwa huu mradi ni usanii mtupu Hayo mabasi yaendayo kasi huwa hayana stendi ya kukusanyika kwa mtindo huu huo utakuwa ni usafiri wa kawaida tu sio wa kasi
 
Kuna habari nimezipata leo kwenye daladala kuwa stand ya mabas ya mkoa inahamishiwa tegeta,swali mbona imehamia mbezi?ni kwa muda au? Ni vigezo gani wametumia kuhamisha hii stand hapo ubungo? Hakuna kaufisadi kweli? Nijuavyo mimi terminal haiwi nje ya mji,inakuwa center kwa ajili ya wakazi wote wa jiji, ubungo wanaweka nini?

Mijitu mingine bana sijui imejuaje JF. Unasikiliza umbea wa kwenye daladala halafu unaamzisha uzi eti tetesi. Hivi tungeposti habari tunazosikia kwa walevi ndani ya vyombo vya usafiri server ya JF si ingejaa siku nyingi
 
duu nimeamini jf ni zaidi greathinker, ivi unajua huwezi andika ki2 usichokijua au kusikia? Ila unaweza kuuliza ili wanaojua wakujuze,huwezi jibu kama hujui jibu, jiulize uko wapi? Magari ya mwendo kasi yana main station mbili,yanapoanzia na yanapoishia,swali ubungo ndo starting point? Mji unatanuka au kukua, je unakua kuanzia kimara kuja ubungo au kimara kuelekea mbezi/kibamba?,,serikali inapokosea lazima tuikosoe ili ijitathimini,
 
Back
Top Bottom