Nilipoona ni Lutheran ikabidi niingie Google niiangalie maana sijawahi kusikia kuna shule za madhehebu mengine zinazofanya vizuri kuleko shule za Katoliki.
Nadhani Lutheran wangeweza kufika japo robo ya shule za Katoliki lakini tatizo la Lutheran hawapo kitaasisi hata kidogo, kwa nje inaonekana ni taasisi ya dini lakini kiuhalisia ni one man show kama makanisa ya Upako, ndio maana mchungaji akileta maendeleo makubwa kwenye usharika na kupata umaarufu KUMCHOMOA SIO RAHISI, watahamishwa wengine tu. Refer to Eliaona Kimaro na Matsai wa Kimara Korogwe.
Project za kanisa Katoliki huwa zinaratibiwa kitaasisi ndio maana zinafanikiwa sana na pia kuna kuwajibishana bila kujali status ya mtu lakini Lutheran wao hata kuwajibishana ni kazi na ukimgusa mchungaji maarufu atashawushi waumini WAANDAMANE.
Shule za Lutheran zungekuwa zinafanya vizuri sana kama System yao ingekuwa IMARA