SSRA:Ufafanuzi juu ya hali ya mfuko wa Hifadhi ya jamii, NSSF

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
TAARIFA KWA UMMA

logo-ssra.png

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.

Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko.
Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.
Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.

Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam.

Source: Michuzi
 
Umepewa taarifa ya NSSF wewe unataka PSPF, huo nao ni ujuha. SSRA wapo pale Victoria huna haja ya kuuliza huku JF.
 
Hizo ndizo sifa zako ndio maana unatumia masaburi kufikiri. Umeelekezwa ilipo SSRA ukawaulize unawashwa nini sasa
 
Samahani kwa kuuliza swali nje ya mada, hivi mifuko ilisharekebishwa katika kutoa mafao yenye uwiano sawa? Mfano PPF nasikia wastaafu walikuwa wanapokea pesa kiduchu sana
 
Aliyepost hii taarifa kwa umma sio SSRA ni mtu kama wewe Wanjiru anajiita Asigwa. Hapa JF hatulipi mafao brother. Lalamika hapa uone kama JF watakulipa kesho. Tumekuelekeza Ssra watakusaidia ulipwe sio hapa jf
 
Kuna mtu alietaka mafao hapa?
 
Elimu, elimu, elimu! Ww Wanjiru feki ndiye uliyetaka kujua hali ya kulipa mafao kwa pspf wakati umeona kabisa thread ni ya nssf. Hujielewi ww lakin co shida yako ni uelewa wako mdogo wa kuinterpret mambo
 
kuna kitu unakitafuta wewe sio bure
 
Hawa SSRA ni toothless dog aseee hawana jipya mwenye timamu yake hawezi kukaa chini kuwasikiliza nao wapo njia moja na mifuko wakila mema ya nchi.
 
Elimu, elimu, elimu! Ww Wanjiru feki ndiye uliyetaka kujua hali ya kulipa mafao kwa pspf wakati umeona kabisa thread ni ya nssf. Hujielewi ww lakin co shida yako ni uelewa wako mdogo wa kuinterpret mambo
Umeshaambiwa kunakitu unakitafuta ....,wewe ndo huna elimu ya hivi vitu kwa maana kilichoongelewa ni hifadhi ya mfuko wa jamii mmoja kati ya lukuki iliyopo. Nakutajia kadhaa PSPF,LAPF,GEPF,PPF
Namalizia kama mtu anaswali la mfuko wa hifadhi ya jamii ni muafaka kuulizia katika uzi huu
Wasalaaam
 
Back
Top Bottom