SSRA, PPF, NSSF hawasomeki

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,204
Mabadiliko PPF na NSSF imekuwa mwiba mchungu na wenye sumu kali kwa wafanyazi wanyonge yaani ma
Blabla zinazoendelea sasa kuhusu fao la kukosa ajira kama mbadala wa withdrawal, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii ni source nzuri sana ya mapato kwa Serikali.

Ukweli ni kwamba Gvt imeamua makusudi kuwaibia wanachama wa mifuko hii na umma unapumbazwa kupitia vibaraka kama SSRA na baadhi ya wahariri wa media.
Si kweli kwamba Serikali inajali welfare ya mtanzania atakapokuwa mzee wa miaka 60. Ni unafiki mtupu. Wanajua wakikunyima pesa yako sasa utakufa anyway na hivyo kutodai mafao yako. Hivyo PSSSF na NSSF kupendelea kuneemeka kwa pesa za wafu. Cursed SSRA. Why nilazimishwe kusubiri miaka 55 kuchukua pesa yangu ya mafao baada ya kuachishwa kazi? Kwa nini nilazimishwe kuchukua roborobo kupitia ujinga unaoitwa unemployment benefit!!?

Wanasema unapoacha kazi sehemu A uombe kazi sehemu C! Hivi akina Mhagama wanajifanya hawajui ugumu wa kupata ajira Bongo? Kwa uchumi gani? Wanapata wapi courage ya kumwambia mtu aliyeanza kazi akiwa na miaka 49 asubiri hadi miaka 60 ndio achukue pesa zake ambazo kiukweli ni ndogo masikini. Nani atamwajiri mtu mwenye miaka 50?

Nasikia hawajazingatia hata mfumuko wa bei. Ukiwa na laki moja baada ya miaka 10 utakuja kulipwa kiasi hicho hicho. No interest. No nothing. Huu ni mpango wa ovyo kabisa na ni kaburi kwa wanachama wenye mishahara midogo. Mtu ana milioni 2 mnataka kumpa kidogo kidogo eti kusubiri apate ajira nyingine. Si mumpe hela yake akajiajiri?

This is a great injustice and the whole law is bad very bad to low income earners.

Ajira hakuna waacheni wanachama watafute plan B. Kwani lazima kuajiriwa? Watu wapewe pesa zao bwana pindi tu wanapoacha kazi. Mtajitakia laana za bureee wanachama wakifa kabla ya kulipwa fedha zao.
 
Umenigusa na maneno yako. Sema nini brother, haya ni maneno ya samaki baharini,

Andika barua nenda makao makuu nssf na ssra weka kwny suggestion box. Ukishindwa peleka IG mpe dada mwambie hide my ID naye atafanya yake.
 
Mkuu hakuna namna, mimi nimeamua kuiacha tu iangamie tu huko, coz hakuna maana kuchukua pesa kidogo kidogo wakati michango ilikuwa ni ya mwaka mmoja!!
 
Reactions: rr4
Hawa wahudumu..... kwanza kama pale millenium tower majibu kama mashetani, halafu Jana nimewasikia walisema wazi kuwa walioachishwa kazikuanzi tarehe 1.8.2018 hawatapewa mafao badala yake watafute kazi mpaka wapate waendele kuchangia
Eneo hili lina huduma mbaya sana unaenda unaambiwa maneno ya kipuuzi wakati ni pesa zako kwanini wanatulazimisha tuweke.pesa zetu kwenye mamifuko yao huu ni wizi wa hali ya juu nchi HII nachelea kusema.inalaana
 
Hapa mwenyewe unababaishwa ukifa wanaokurithi watapewa TUPENI MAFAO YETU serikali imeyafanya mashirika yanakufa na kushidwa kumudu kujiendesha yanapunguza wafanyakazi kwanini hamtoi mafao yetu Tujiajiri TUNATAKA PESA ZETU PPF SAAHIZI UKIENDA UTADHANI WAPO PICNIK MAJIBU YAO KAMA WANA MIMBA WAKE KWA WAUME ... Hawafanyi kazi yoyote ati wamehama unamuuliza jambo hata halihitaji aingie kwenye computer atajibu hakuna system
 
Wakati akina Zitto wakielezea ubaya wa muswaada wa hii sheria tulikuwa kimyaaa na wengine as usual wakaendeleza upinzani Vs watawala league..... Haya ndiyo matokeo yenyewe.
Ule mswaada nilijua tu watu watalia sana, hata mm sina hamu, kama mtu ulijua utapaua kwa hela ya fao la kujitoa ni maumivu,
 
Hii ni dhuluma na ushenzi. Yaani kama mtu masikini alikuwa analipwa mshahara laki tatu eti sasa kwa hiyo sheria yao atalipwa laki moja laki moja kwa miezi sita tu. Li nchi la ovyo sana hili...tumeruhusu majizi yenye roho mbaya ndio yawe viongozi.
 
Nchi ya asali na maziwa hii jamani.mm m3 zng nimesamehe najipanga nitafute naul nihame nchi ntakuwa nakuja kama mtalii am tired.
 
Hao wanaojiita viongozi wamefanya ukatili mkubwa sana. Hilo lisheria lao haliendani kabisa na mazingira ya bongo.
Mishahara midogo pia viajiri vinalipa hiyo michango kwa kusuasua sana na huto tumafao ndio tunawasaidia kuanzisha shughuli za uchumi. Heee nato mnataka kuwapora?! Kassim Majaliwa vipi bwana. Unaona rahaaaa wananchi wanyonge wanadhulumiwa!
Wafanyazi kama wa PPF nahisi nao wamechanganyikiwa kwani hawajui hatma yao. Mashirika yanapoungana lazima baadhi ya wafanyazi watatemwa tu!

Si kila mtu anataka kuajiriwa. Ni nusu utumwa. But wakati mwingine mtaji wa kufanyia biashara ili ujitegemee, unatokana na kufanya kazi for sometime.
Sasa gvt inapotaka kuwanyima mafao yao ni kama kuwataka wawe 'watumwa' for life! Wafanyazi tz poleni lakini stand up for yr rights
 
Kwa hili la mafao, serikali ya wanyonge mnataka kutufanyia dhulma. Tupeni fwezwa zetu bana tujiajiri. Binafsi naumia sana maana kwa haya maisha niliyonayo alafu ukizingatia kuwa Kuna fedha ambazo nilikatwa kwa miaka 5...kwenye kuhangaika niwe mimi then matumizi napangiwa. This is not fair, maana hata hilo fao la kukosa ajira halijawa applied ijapo tuliambiwa 1.8.2018,litaanza rasmi. Wanasiasa acheni kucheza na maisha ya watu kwa mambo yenu ya kijahilia.
 
Umenigusa na maneno yako. Sema nini brother, haya ni maneno ya samaki baharini,

Andika barua nenda makao makuu nssf na ssra weka kwny suggestion box. Ukishindwa peleka IG mpe dada mwambie hide my ID naye atafanya yake.

Huo utaratibu wa kusubiri sijui miaka 80 wafanye kwa wenye mamilioni 100 huko. Watu wa hela za mboga kama mil. 50, 20, mil moja hadi laki walipwe haraka. Kadri inavyozidi kuchelewa ndivyo inavyoshuka thamani.
Alas!! SSRA chini ya Irene, PPF chini ya Eliud na NSSF chini ya Erio wanatengeneza 'mv Nyerere ya kimyakimya' !!! If you know what I mean.....
 
Dawa ya Sheria kama hizo ni Mahakama. Tujifunze kufungua kesi mahakamani kwa ajili ya kupinga sheria kama hizo, kuaamikia humu mitandaoni aafu mnachagua wabunge wa ccm wengi hakuta saidia
 
SUBIRINI MSUMARI UINGIE MMEWAPELEKA WENYEWE
 
Serikali ilipaswa kurizika na kodi wanayopata kwa mwezi tena kodi yenyewe anayokatwa mfanyakazi ni kubwa mno,wakaona haitoshi wakaamua kuchukua tena na hiyo michango ya mlala hoi.
 
Dawa ya Sheria kama hizo ni Mahakama. Tujifunze kufungua kesi mahakamani kwa ajili ya kupinga sheria kama hizo, kuaamikia humu mitandaoni aafu mnachagua wabunge wa ccm wengi hakuta saidia
Ingekua Kenya ndio wamefanyiwa huu upuuzi pasingekalika
 
Hii ni dhuluma na ushenzi. Yaani kama mtu masikini alikuwa analipwa mshahara laki tatu eti sasa kwa hiyo sheria yao atalipwa laki moja laki moja kwa miezi sita tu. Li nchi la ovyo sana hili...tumeruhusu majizi yenye roho mbaya ndio yawe viongozi.
Nchi yawiziiikwann wanachukua pesa zetu hakuna sheria ya kukataa kuwekewa pesa si bora uweke kwenye kibubu naapa ukifa watoto wako hawapsti HII pesa serikali ya Tanzania ni wezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…