SSRA iache kutafuta simple solutions. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SSRA iache kutafuta simple solutions.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njaare, Aug 1, 2012.

 1. N

  Njaare JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikijiuliza ni nini kimewafanya SSRA kupitia serikali kupeleka sheria kandamizi bungeni huku wakijitetete ati kuwa wanataka kuwasaidia watu wastaafu vizuri. Huu wema umetoka wapi? Tokea lini serikali ya CCM ikawa na wema kwa wastaafu wake? Mbona wazee wastaafu wa ilokuwa Jumuia ya Africa Mashariki mpaka leo wanasota na si serikali iliyowasilisha msaada bungeni wala SSRA imeonekana kuwasaidia? Naona hela za wazee wa jumuia ya Africa Mashariki zilikuwa tamu sasa wanataka kutafuna na za vijana wanaofanya kazi kwa mikataba.

  Nasema haiiingiii akilini hata kidogo. SSRA kama inasema ina nia njema, ituelezee imefanya nini kuibana serikali na mifuko husika kuhusu kurejeshwa fedha zilizochukuliwa kwenye mifuko na serikali hata bila ya mkataba kwa ajili ya kujenga UDOM na miradi mingine. SSRA inataka fedha zetu ziendelee kuchotwa na serikali halafu sisi tukae tukisota kama wale wazee wa Afrika Mashariki? CAG alishatoa riport kwamba serikali haijaanza kurejesha hizo fedha na ndiyo maana mifuko inaelekea kushindwa kuwalipa wanachama nando maana wanakuja na sheria ya kuzuia watu wasidai chao.

  SSRA, acheni kuchukua solution za kijinga kama "mtaka cha uvunguni, kitanda nyanyua". Wabaneni serikali irudishe hela za wanachama. Pia tunapenda kusikia kuwa wakurugenzi na Bodi zilizotoa fedha za wanachama bila mikataba ya kueleweka wanatimuliwa.
   
 2. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njaare,

  SSRA ni kweli Akina Mama tunaweza!,, yeah ule wimbo wa Beijing. I have a lot of respect to women lakini sio kila Mwanamke / Mwanamume anaweza kufanya kazi. It has to do with intergrity, maturity and conviction. Hii Tabia ya kuwakabidhi madaraka every Jack , Tom and Happy kuongoza taasisi nyeti iko siku tutajuta.
  The provident funds should belong to a body formed by members apart from that the Regulator should only regulate and not formulate operational matters. The outline of the funds should be left to the members .

  It doesn't make a lot of sense for the Govment kujeuza hii mifuko kuwa ATM zake . Kukomesha huu upuuzi the government should not interfere . Nashangaa hata NHIF inakopesha serikali fedha za wanachama wakati bila huruma huku Houma zikiwa Mbuzi??

  Huyo binti anayeongoza SSRA ni aina fulani ya kituko Kama alivyofanya Ndugai Bungeni. If you read her posture and the message are just miles apart hana hata aibu ni lini serikali ikawa na huruma na future ya retired and old people?.? The pension itself has no dynamism I thought SSRA could have come up with a solution ili kiasi cha pension anayo pokea mstaafu kisiliwae na inflation plus devaluation .

  Let us peg it to say 40% ya mshara wa mtu aliyeajiriwa in a similar manner Kama Mafao ya Waziri Mkuu mstaafu who is required to be paid 80% of the salary of a sitting Prime Minister. Sasa huyu mdada anakuja na mauzauza ya kuweka pesa mpaka mtu afikishe 55+ years na hao Wabunge wahuni na wala rushwa ( Regardless of their parties) wakapitisha simply because they are excluded? I am talking about the time value of money I am not sure if you all understand what I mean. Vinginevyo let it be in USD of course take on board time value!!

  Nawauliza Wabunge and those party hooligans how would it sound if the 40m/= MPs severance pay is withheld until they reach 60 years wanaongea nini???? Mkuki kwa Nguruwe Eeee! ( ashakum kumbe huu mwezi wa toba)
   
 3. N

  Njaare JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inatia hasira sana. Tatizo vyama vyetu vya wafanyakazi havitaki kufanya kazi yao. Kama vingewajibika hata hii shera isingepita. Sasa wafanyakazi waamke ili Serikali iache kuifanya hii mifuko kama akaunti zake.
   
 4. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  tunasifika kwa kusahau lakini kwa hili...?????sijui, kwa namna flani kama movie ya kutengeneza matukio ya kusahaulisha watu, issue ya madokta, ikafuata ya docta ulimboka, ikaja mafao, mara bunge na mafisadi na sasa tunaongelea walimu na wanafunzi wao..
  nadhani director wa hizi movie ni mkali kweli...
   
Loading...