SPIKA WA BUNGE: Kiti kinachangia busara bungeni

EJL

Member
Jan 14, 2012
83
54
Kwa Spika wa bunge, naibu na wenyeviti wabunge.
Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na rabsha Mara kadhaa wakati wa vikao vya bunge na Mara zote umeamuru kuondolewa kwa nguvu mbunge (ambaye wewe umeona ni tatizo). Nimekuwa mfuatiliaji wa vikao vya bunge (tangu bunge la chama kimoja). Ni wazi wako wabunge wakorofi na wenye utovu wa nidhamu wa wazi kabisa na hawa wako upande zote mbili. Ingawa ni dhahiri wako wabunge kutoka CCM ambao wamekuwa wakifanya vitendo ama kutoa kauli zisizo na staha kwa wazi kabisa na Mara kwa Mara. Hawa ndio kwa upande mwingine wamekuwa chanzo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kukasirika. Mfano, ni nadra sana Lusinde ,Goodluck kumaliza dakika zao za mazungumzo pasipo kutukana wabunge wa upinzani. Ndugu Spika, wako wabunge wa ccm ambao wamejipa jukumu la serikali/wizara kujibu hoja za wabunge wa upinzani. Hii si tatizo sana endapo wangekuwa wanajibu kwa hoja. Mara zote wao hutumia matusi tu.
Jambo la pili, (kabla hata ya bunge la sasa) utagundua bunge limekosa utulivu linapoongozwa na naibu wako au wewe (rejea hata wakati ukiwa naibu Spika). lakni ni nadra sana wakati wakiongoza wenyeviti. Huko nyuma Mama Jenister alipokuwa akikaa km Mkiti alilimudu vema sana bunge kwa sababu tu alijiepusha na USHABIKI. Mara kadhaa wewe umekuwa ukichombeza mbunge anapozungumza ama kwa kutumia lugha ya kejeli au kauli yenye utata. Mathalani, tukio la juzi binafsi ninaona wewe ulichangia kwa kiasi kikubwa sana. Maana alianza Lusinde kwa kueleza umwamba wake ama akilindwa na hata asipolindwa na kiti. Alipoanza kuzungumza nilitarajia utamsahihisha haraka. Aliposimama ndugu Mnyika na taarifa, kabla hujampa nafasi ulianza kwa kusema "Mnyika unataka kushindana na Lusinde!". Kwa Akili ya kawaida tu, hii inaibua hisia kwa Mnyika na Lusinde pia. Aidha baada ya kambi ya upinzani kutoka nje, uliorodhesha wenye makosa na hatua ulizochukua pasipo kumhusisha mbunge " wa like" aliyewasha mike na kusema "Mnyika mwizi!!. Ulionesha kukerwa sana na kitendo cha Ester Bulaya kutoka akigonga baadhi ya meza na kuzungumza. Na waandishi akiwa nje, (ukasema hii ni ni aibu kwa wana nchi wa Bunda na wanawake wote) lakani hukuwahusisha baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakitukana na kuonesha vitendo vya habari udhalilishaji. Huu ni mfano wa tukio moja la wazi na dhahiri linaloonesha upendeleo wa dhahiri .
Spika, lazima utambue kuwa wabunge ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, huumia hisia zao na kuitikia iwe hasi au chanya. Hivyo mbunge wa upande wowote anapoudhiwa huvumilia lakini ikizidi na akijua mamlaka zinamlinda anayemchokoza huamua kujihami mwenyewe, na ndicho tuonacho sasa. Utawafukuza sana wabunge wa upinzani (CHADEMA) bungeni lakini hata hawa wakiwa nje, bunge halitokuwa na nidhamu. Hii wewe ni shuhuda wa bunge la katiba na vikao vingine ambapo kambi ya upinzani walitoka lakini wengi wa wabunge wa ccm waliosalia bungeni walitumia muda mwingine ama kutukana waliotoka nje, kuongelea yaliyo nje ya Mara au kuzuia wenzao kuzungumza.
Spika, inawezekana kabisa umebanwa (tunajua Mara zote mnaitwa vikao vya chama), lakini nadhani wakati wote uungwana ni kusimama katka kweli, sheria, kanuni na utu. Ulishuhudia wakati wa kuaga mwili wa marehemu S. Sitta, kila aliyezungumza alimzungumzia utendaji wake akiwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano na si MWENYEKITI wa bunge la katiba. Kwa sababu akiwa katika kiti hicho ndipo tulipomuona akitenda kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria. Mapungufu yaliyokuwepo hajakuzuia kummbainisha kama kiongozi mweledi.
Ili kudumisha heshima ya bunge ni muhimu sana kuhakikisha kanuni zilizopo zinatumika pasipo kutazama huyu ni wa upande gani.
Heshima yako kama Spika au naibu spika itajengeka kwa kutenda kazi kwa kanuni, sheria, haki na uadilifu. Kitu chako kina mamlaka ya kulifanya bunge litende kama bunge (chombo cha kutunga sheria na kuisimamia serikali), au kama baraza la marumbano ya wanasiasa, au kijiwe cha Kahawa/pool table, au genge la wahuni. Hili liko katka mamlaka yako. Lakini pia ni muhimu kukumbuka kuwa wakati tukiwa katiba mamlaka Fulani, rejea hufanywa kwa wadhifa, lakini tukitoka hapo rejea hufanywa kwa MTU binafsi aliyekalia kiti kwa kipindi Fulani.

Lugano
 
Kile kitendo cha kupiga mtu hadi amepoteza fahamu na kulazwa hospital, bado kinasababasha msongo wa mawazo. Kitendo kile ni dhambi na mshahara wa dhambi ni MAUTI. Dhambi hiyo inaendelea kumtafuna.
 
Hawa wawili ndiyo wanalifanya bunge likose hadhi, kupandikiza u CCM na kuwagawa wabunge ndani ya chombo kitukufu. Matokeo yake Bunge linatoka nje ya majukumu yake makuu ya kuisimamia Serikali badala yake serikali ndiyo inalisimamia Bunge. Kweli nimekubali mzee wa viwango tutamkumbuka mno.
 
Mkuu umenena, atakae pingana na andiko lako basi atakuwa amevaa miwani ya mbao.
Msema kweli mpenzi wa mungu, kiti cha speaker kina pwaya, a speaker and his/her deputy must be neutral,wakiendeleza uchama legacy zao hazita mfikia mzee six rip.
Manual jukumu la backbenchers kutoka pande zote, lakin kwa nini wa upande mmoja ndio wanakuwa punished?.
 
Tatizo letu kubwa spika anashindwa kuelewa wabunge wote sawa na yeye nikiongozi wabunge wote
 
Back
Top Bottom