Spika wa Bunge, Job Ndugai athibitisha kupokea barua ya kuvuliwa uanachama Wabunge 8 wa CUF

Profesa Lipumba sijui kapewa kiasi gani na CCM. Yaani heshima yake yote imekwisha kwa mamboa anayoyafanya sasa hivi. Yaani anafanya juhudi kubwa kuidhoofisha CUF kwa kipindi hiki kifupi, kuliko juhudi zote alizofanya kujaribu kuijenga CUF bara miaka yote kabla ya uchaguzi wa 2015. He should be ashamed of himself very useless man!
chama kinauzwa ufipa,lipumba hawezi kubali jasho lake liliwe na sultan..na litote tugawane mbao
 
hili suala la kuwavua ubunge hao waheshimiwa halijakidhi vigezo, ukitizama hapo haki kijinsia ni kama kuna uonevu mkubwa, nitashangaa sana pale Mh spika atakaporidhia maombi ya Profesa Lipumba wakati kuna shauri lake lipo mahakamani bado la uenyekiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai athibitisha kupokea barua ya kuvuliwa uanachama Wabunge 8 wa CUF. Amesema kuwa atatoa uamuzi hapo baadaye baada ya kutafakari.

======

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
________________________

Mhe. Spika amepokea barua kutoka kwa Mhe. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) na Mhe. Magdalena Sakaya, (MB) - Kaimu Katibu Mkuu (CUF) ambapo wamemuarifu kuhusu uamuzi wa Baraza Kuu la Chama hicho kuwafukuza Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili kwa makosa kadhaa ya kinidhamu.

Katika barua hiyo, viongozi hao wamewataja wanachama hao ambao ni Wabunge kuwa ni: -

1. Mhe. Severina Silvanus Mwijage, (MB);

2. Mhe. Saumu Heri Sakala, (MB);

3. Mhe. Salma Mohamed Mwassa, (MB);

4. Mhe. Riziki Shahari Ngwali, (MB);

5. Mhe. Raisa Abdallah Mussa, (MB);

6. Mhe. Miza Bakari Haji, (MB);

7. Mhe. Hadija Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na

8. Mhe. Halima Ali Mohamed, (MB).

Aidha, barua hiyo imeainisha makosa yao kuwa ni kukiuka Kifungu cha 83(4) na (5) cha Katiba ya Chama hicho kwa kutenda makosa yafuatayo: -

1. Kukihujumu Chama katika uchaguzi wa marudio wa Madiwani wa tarehe 22 Januari, 2017;

2. Kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Naibu Katibu Mkuu na Mbunge wa Kaliua, Mhe. Magdalena Hamisi Sakaya, (MB) na Wakurugenzi wa Chama;

3. Kushirikiana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupanga oparesheni waliyoiita “ONDOA MSALITI BUGURUNI” wakiwa na lengo la kumuondoa Mwenyekiti halali wa Chama hicho kinyume na taratibu za Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992;

4. Kuruhusu na kuipa fursa CHADEMA kuwa msemaji wa masuala ya CUF kinyume na matakwa ya Katiba ya CUF;

5. Kulipia pango na kufungua ofisi ya CUF Magomeni bila kufuata taratibu za kikatiba; na

6. Kuchangia fedha zilizotumika kukodisha ma-bouncer kwa lengo la kuwadhuru Viongozi watiifu wa Chama akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba; Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Magdalena Hamisi Sakaya, (MB) na Mhe. Maftaha Nachuma, (MB), Mkurugenzi wa CUF wa Mambo ya Nje na Mbunge wa Mtwara Mjini.

Mhe. Spika angependa kuuarifu umma kuwa, suala la kuwaondoa uanachama ni la utashi wa Vyama vyenyewe; na kila Chama kina utaratibu wake, hivyo bado anaendelea kuitafakari barua hiyo; na taarifa rasmi kuhusu maamuzi ya Spika kwa Wabunge waliofukuzwa ataitoa hapo baadaye.

Imetolewa na:

Ofisi ya Spika,

S. L. P. 941,

DODOMA.

25 Julai, 2017
Kusema ukweli kama huyu profesa na wenzake kwa kitendo wanachofanya kama wanaswali msikitini hawana hofu ya Mungu hata kidogo,wenzako wamepambana wakati wa uchaguzi kiasi mpaka wamepata mafanikio hayo leo hii wanadiriki kitumia hila ili wauwe chama ambacho profesa alikuwa anatamka kangangari na ngunguri watu wamepewa vile leo hii huyo huyo anatumia nguvu kubwa kubomoa?nasikitika sana
 
Kwa maoni yangu, kwakuwa kuna mashauri Mahakamani yanayojikita katika uhalali wa viongozi wa CUF, suala hili linapaswa kusubiri kuisha kwa mashauri husika. Hii ni kwakuwa hata uanachama wa Prof. Lipumba pamoja na Mbunge Sakaya unahojiwa mahakamani.

Yatakapoisha mashauri hayo yaliyo mbele ya Mtukufu Jaji Ndyansobera, viongozi halali watajulikana. Na vitendo na maamuzi halali vitaonekana. Mambo ya CUF yatakwisha tu kisheria siku si nyingi.
Shughuli haziwezi kusimama kusubiri kesi.
Wafukuzwe tu bungeni,ikionekana wameonewa watarudi
 
Hiyo barua haina impact yeyote maana aliendika ni cuf fake yani ccm b,wakti wa kampeni ya kuwapata hao wabunge viti maalum yeye prof alikua anashikishwa ukuta rwanda...huyu jamaa njaa imeingia mpka tumboni yani kusoma kote kaishia kua vuvuzela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu utasikia eti wana nia njema ya kuimarisha demokrasia nchini! Nchi hii Sidhani kama tunachokifanya tunakijua. Ccm kupitia huyu profesa uchwara lipumba mnaharibu nchi
Tatizo sio CCM bali watanzania ndo tatizo. Inashangaza kuona pamoja na sanaa zote za Le prof,bado kuna watanzania wanaamini kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipumba na maalim sief wanaichanganya cuf


Mkuu; Umepofuka macho kiasi hicho?? Maalim ametoka wapi katika kutuchanganya?? Yaani, aliyeandika barua kwamba halitaki tena hilo lichama la cuf na kujiendea kutafuta kibarua ng'ambo kwa mwaka mzima akarudi. Kisha kusema hajawahi kujiuzulu bali aliamua kwenda pumzika. Hujiulizi swali; Je, hiyo cuf ilikuwa ya mamake?? Unathubutu kujifyatua akili kuwa Maalim aliyepigana kufa na kupona kuilinda cuf leo anatuchanganya kwa kusema Lipumba hatufai?? Naona una tatizo kiakili
 
Yaani kuna wakati inafika unaona kuna hoja kwa wale wanaohoji uhalali wa taaluma ya bwana Lipumba...

Nchi ya Tanzania ina watu wa ajabu sana sijawahi kuona...
Kwa maoni yangu, kwakuwa kuna mashauri Mahakamani yanayojikita katika uhalali wa viongozi wa CUF, suala hili linapaswa kusubiri kuisha kwa mashauri husika. Hii ni kwakuwa hata uanachama wa Prof. Lipumba pamoja na Mbunge Sakaya unahojiwa mahakamani.

Yatakapoisha mashauri hayo yaliyo mbele ya Mtukufu Jaji Ndyansobera, viongozi halali watajulikana. Na vitendo na maamuzi halali vitaonekana. Mambo ya CUF yatakwisha tu kisheria siku si nyingi.
 
Mzee hili jambo linahitaji busara sana katika kulishughulikia. Mzee wengi tunapenda sana mapatano na maelewano kwa kuwa tunaamini chama ni jumuia ya watu na hao watu wana hulka na tabia zisizofanana.
Kwani kuna ubaya gani kwa Maalimu Seifu kukutana na Lipumba? Mbona suala lenyewe ni dogo sana? Naamini Maalimu na kundi lake wanao wafusi wengi zaidi ya Lipumba na kwa kutumia wingi wao wanayo fursa nzuri sana ya kumtimua Lipumba. Kwani Maalimu na kundi lake wanashindwa nini kukubaliana na Lipumba halafu baadae wakamtosa Lipumba kwa kufuata na kutumia sheria za chama chao? Hizi kesi zina matokeo chanya na hasi, lazima kuweka akiba.
Wakati wanamtosa lipumba atakua amelala? Kumbuka ukifunua karata yako mwenzako anafunua

the great
 
Wakati wanamtosa lipumba atakua amelala? Kumbuka ukifunua karata yako mwenzako anafunua

the great
Mzee kwa hali ilivyo na inavyoratibiwa kuna siku utasikia Maalim kaondolewa nafasi yake ya ukatibu. Na usijie ukashangaa Maalim kabwagwa mahakamani. Na ndipo utakaposikia mchanganyiko wa hali ya juu.
 
Mzee kwa hali ilivyo na inavyoratibiwa kuna siku utasikia Maalim kaondolewa nafasi yake ya ukatibu. Na usijie ukashangaa Maalim kabwagwa mahakamani. Na ndipo utakaposikia mchanganyiko wa hali ya juu.
Maalim hana chake mpaka sasa alijichanganya sehemu moja tu kukataa kurudia uchaguzi angekua makamu wa rais angekua na nguvu kidogo

the great
 
Maalim hana chake mpaka sasa alijichanganya sehemu moja tu kukataa kurudia uchaguzi angekua makamu wa rais angekua na nguvu kidogo

the great
Hakika kabisa. Ila, hivi alifahaamu mwishilizo wa maamuzi yake? Seif ni mwerevu sana na ni mtu aijuaye kesho yake hasa linapokuja suala la mikanganyiko kama hii, mimi najiuliza je ilikuwa ni bahati mbaya au alikusudia?
 
Back
Top Bottom