Spika Ndugai umeshindwa kusimamia Bunge na Serikali

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,485
96,049
Tangu bunge la 11 spika wa bunge Ndugai na naibu spika wake wameonyesha kushindwa mapema kulisimamia hilo bunge katika maombo yafuatayo.

1: Wabunge wake kutuhumiwa kwa rushwa
Huu ni mfano dhahiri kabisa kuwa Ndugai ameshindwa kulinda nidhamu na maadili ya muhimili huu muhimu.

2: Bunge kushindwa kuonyeshwa LIVE kama ilivyokuwa kwa ma spika wenzake waliomtangulia na huu ni mchezo mchafu kabisa wa kutaka kuwanyima haki ya kikatiba watanzania kupata habari.

Ndugai jitafakari na ikiwezekana unaweza kujiuzuru ili kulinda heshima yako.

NOTE: Tujadili kwa manufaa ya taifa
 
Ndugai MZEE wa Bakora sio siri hapa amechemka.

Tatizo Magufuri amejiwekea wigo wa ukuta wa moto, watu hawafanyi kazi kwa weredi, wanafanya kazi kwa uwoga na hii italigharimu Taifa.

Spika ajtoe Sadaka kwa ajili ya wengi, aamue kutetea watanzania, aseme hapana kuwakatia watu matangazo ya Bunge live, aseme hapana kufanya kazi na wala rushwa ndani ya Bunge, aseme hapana kwa Escrow kuendelea kuitafuna nchi, aseme MZEE angalia upya mikataba ya wizara ya nishati na madini...akiweza hayo kweli atakuwa ameweka historia, na vizazi vijavyo vitamtukuza
 
Mkuu tatizo ni sera na falsafa za CCM yaani chama kwanza utaifa baadae
 
Ndugai akijiuzulu hata raisi atamshangaa ( in yule mama wa rugemaila's voice)
 
Serikali inayominya uhuru wa kupata habari kwa wananchi wake ina jambo la kuficha!
 
Wanajua kuwa uoza wao ulivyo mwingi na vijana wa ukawa ndio wamekunywa uji wa mgonjwa lazima watawala wavuliwe nguo
 
Kwa staili hii ya utawala wa kuficha maovu kuna siku hata nafasi ya CAG itaanza kuminywa
 
!
!
kuna watu wataingia katika historia kama watu walitumia nguvu na akili zao katika kukwamisha maendeleo ya taifa kwa kulinda maslahi binafsi. Ni kama hawa
 
Shida spika na naibu wamegeuza bunge mali yao wakati ni mali ya watanzania Upinzani mie ndio wananichosha kimyaaaaaa kama hawapo kutwa kuulizia billioni sita.
 
Ndugai MZEE wa Bakora sio siri hapa amechemka.

Tatizo Magufuri amejiwekea wigo wa ukuta wa moto, watu hawafanyi kazi kwa weredi, wanafanya kazi kwa uwoga na hii italigharimu Taifa.

Spika ajtoe Sadaka kwa ajili ya wengi, aamue kutetea watanzania, aseme hapana kuwakatia watu matangazo ya Bunge live, aseme hapana kufanya kazi na wala rushwa ndani ya Bunge, aseme hapana kwa Escrow kuendelea kuitafuna nchi, aseme MZEE angalia upya mikataba ya wizara ya nishati na madini...akiweza hayo kweli atakuwa ameweka historia, na vizazi vijavyo vitamtukuza

Nawashangaa mnaosema amechemsha. Hajachemsha hata kidogo. Anafanya exactly kama watawala wanavyomtaka kufanya. Hatuwezi kuwa na mtu bora kuliko yeye katika "mfumo" huu. Bahati mbaya ni kwamba wengi wetu mang'amuzi huwa yanakuja baadaye sana. Kwa hiyo tuendelee kuomba siku moja atatokea Rais ambaye ataondoa mfumo wa spika kuwa mwanachama mwaminifu wa chama tawala. Najua wakati huo wengi ambao wanaunga mkono mfumo wa sasa wataonyesha kuchukizwa na utaratibu huo. Sawa tu na sasa, wale waliokuwa wanashabikia mfumo wa utawala wa serikali ya CCM chini ya JMK, sasa wanaulaani! Time, time.......will woke up the morons.
 
Back
Top Bottom