Spika Ndugai: Nimwambie Zitto, nina uwezo kumzuia kutozungumza Bungeni chochote miaka yote ya Bunge

Kwani hukuona kwa baba yako Kabla hajafa?
Sikuona ndo maana nimeomba msaada. Nadhani unaweza kunisaidia. Nasikia huwa inaanzia kichwani kwanza, inavuruga mawasiliano halafu ndo inaendelea na mambo mengine kama vile mkanda wa jeshi, kansa, utando midomoni na magonjwa mengine nyemelezi kibao. Mtu wangu wa nguvu naomba unisaidie bwana najua unajua ila tu unafanya kejeli kidogo, hebu funguka sasa!
 
Day, Hayati baba wataifa, Mungu akupumzishe mahala pema. Yote ukiyokuwa ukiyanena kwa kuyakemea Leo tunayashuhudia viongozi wetu wanazidi kuwa Miungu watu, watu hawako tayari kuambiwa ukweli .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amezidi kumuonya mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kwa kauli zake za kudhalilisha Mhimili wa Bunge na kumwambia kuwa anao uwezo wa kumzuia kutozungumza Bungeni chochote miaka yote ya Bunge.

"Nimwambie Zitto, una uwezo wa kupambana na Spika kweli? Nina uwezo kukupiga marufuku kuongea humo mpaka miaka yako ikaisha, hakuna pakwenda, hakuna cha swali, hakuna cha nyongeza, hakuna cha kuongea chochote humo ndani ya Bunge utanifanya nini. Pambana na kitu kingine na siyo Ndugai", amesema Spika Ndugai.



Aidha, Spika Job Ndugai ameagiza tena Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kumhoji Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe baada ya kuendelea kutoa kauli za kulidhalilisha Bunge licha ya kutakiwa kuhojiwa kwa sababu hiyo jana.

===================
For the English Audience
===================

Tanzania's Speaker of the National Assembly, Job Ndugai has again ordered Kigoma Urban MP Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) to be grilled by parliamentary ethics committee following his comments on social media.

Mr Ndugai also threatened to ban Mr Kabwe from speaking in the Parliament indefinitely.

On Tuesday the Speaker ordered the parliamentary ethics committee to grill Mr Kabwe after he criticized the speaker for handing over two reports by parliamentary teams, which were formed to investigate Tanzanite and diamond mining, before they were debated in the house.

Speaking in the Parliament on Wednesday morning Mr Ndugai ordered the committee to grill Mr Kabwe over his remarks on social media that the Speaker was undermining the Parliament in favour of the executive.

Mr Kabwe wrote on Twitter on Tuesday that Mr Ndugai's performance was far behind his predecessors Samuel Sitta and Anne Makinda.

"Ndugai was dreaming to achieve a quarter of Sitta's performance but he has not achieved even 10 per cent of Ms Makinda perfomance," wrote Mr Kabwe.

Responding to Mr Kabwe’s accusations Mr Ndugai said the Kigoma Urban Member of Parliament risks long term ban from speaking in the Parliament.

"During the 9th Parliament under Mr Sitta, Mr Zitto was banned from the House for three months. Does he want me to go at that speed?" he queried.

"I can ban him from speaking in the house indefinitely because I have the powers…I advise him not to invite problems because he can fight anyone but not Ndugai,” said the speaker.

=====
Some notable comments from Forum Members:

More than half of the members are questioning to where the Speaker derives that power from.

Another member is saddened by the reaction of other MPs who were clapping and reminds them that this will not only affect Zitto but all of them.

One reminds the Speaker that his name has no power but the position has some power and he should learn how to differentiate the two.


" Power corrupts, Absolute power corrupts Absolutely "
 
saaafi saaana.... kamchana live b/w... ye si analeta siasa kwenye magezeti.... na mitandao ya kijamii... anapiga majungu kama mtoto wa kike..

Kidume jimemchana live kwamba hana la kumfanya..

Sent from "La -Vista"
 
mh, sijui nakumbuka ule mkono ulionyoshwaa kipindi kileee....yakaja yakatokea yaliyotokea...
 
Mbona ametoa vitisho bila kutaja kama utaratibu ndo huo wa kufanya uchunguzi na kukabidhi ripoti serikalini?
 
ulevi wa madaraka wa wanasiasa wetu, mtu mwenye busara na hekima na kiongozi wa chombo kama hiki huwezi kuongea ujinga huu
 
Nyie mazuzu mmenyiimarisha kumjadili spika badala ya kujadili sheria za bunge ambazo zitatumika kumuadhibu Zitto.
 
Back
Top Bottom