Spika Ndugai na Tume ya Uchaguzi kwanini mnaendelea kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

vicdala55

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
1,009
1,638
Turejee kwenye chaguzi zetu. Usihangaike na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, huo hauwahusu Tume ya Uchaguzi.

Twende kwenye Uchaguzi Mkuu. Anzia kwenye uchukuaji na urudishaji wa fomu. Fikiria ilivyokuwa vigumu wagombea wa ulipinzani kuchukua na kurudisha fomu, hii ni kuanzia ngazi za Udiwani hadi Urais.

Fikiria kuna wapinzani walienguliwa kwa mabavu ili kutowaharibia Viongozi wetu Wakubwa..Anzia Jimboni kwa Waziri Mkuu hadi Jimboni kwa Spika.

Katiba ya Nchi inasema Waziri Mkuu ni lazima atokane na Jimbo, maana yake hapa hata kama haijatamkwa wazi ni kwamba Waziri Mkuu ni lazima ACHAGULIWE KWA KURA ZA WANANCHI. Leo tuna Waziri ambaye hakupigiwa kura. Tume ya Uchaguzi inaona ni sawa tu Taifa kuwa na Waziri Mkuu aliyetokana na Uchaguzi wa aina hiyo.

Uchaguzi wenyewe kwa ujumla ni kituko. Mpango uliwekwa kila Jimbo lazima Chama Tawala kishinde. Jimbo ambalo litatoa matokeo tofauti Mkurugenzi wake atakiona cha mtema kuni. Ikawa hivyo, kasoro majimbo fulani yaliyoachwa ili kuwaonyesha watu kama rejea ya majibu ya kuhalalisha uhalamia huo.

Leo kuna majimbo matokeo ya kura yamefanana kwa kila kitu kasoro majina ya waliotangazwa kushinda. Tuna matokeo ya Uchaguzi ambayo kura zake ni nyingi kuliko wapiga kura. Ukiingiza kura kutoka kwenye mabegi ukazijumlisha na za wapiga kura, tarajia idadi inayovutia watalii.. Utapata Wabunge wenye haya ya kuwawakilisha Wananchi. Ukikutana na Bunge la aina hiyo, usitegemee watakuwa na maswali ya kuuliza Serikali..hawawezi.

Bunge linaloongozwa na Spika ambaye hapendi ushindani wa hoja kuanzia kwenye kura za maoni hadi Bungeni usitegemee litakuwa na hoja za kuuliza Serikalini. (Ukimzidi hoja anakupiga bakora). Usitegemee litakuwa ni Bunge lenye uwezo wa kuchambua kwa kina ripoti za CAG. Hata kama atasema Taifa limeibiwa.

Bunge ambalo limeshirikiana na Tume ya Uchaguzi kufoji majina ya Wabunge wa viti maalum kutoka Chama walichokidhulumu uchaguzi usitegemee litakuwa ni Bunge la kuisaidia Serikali kuwajibika kwa Umma. Litabaki kuwa Bunge la kudemka.

Spika anahoji uhalali wa maamuzi ya kuwavua Uanachama Wabunge wake wa kupika lkn hataki kusikia akiulizwa kama alihoji uhalali wa uteuzi wa Wabunge wake hao. (Achana na zile gharama za mabilioni kwa matibabu yake ya maladhi yasiyojulikana). Spika wa aina hiyo anazo sifa zote za kuwa kivutio cha Utalii.

Tume ya Uchaguzi yenye uwezo wa kubumba Wabunge na kuwapeleka kwenye chombo muhimu ambacho ni Ubongo wa kutunga Sheria zote za Nchi bila soni, Tume hiyo inazo sifa zote za kuwa kivutio cha Utalii.

Kama Tunaweza kuwa na Bunge linalopatikana kiharamia, basi tunaweza kuwa ni Nchi yenye kulinda maharamia kisheria. Tutakuwa ni Taifa la Wahalifu wasio na Hatia.

Ningelikuwa na mamlaka, ningeliongeza Tume ya Uchaguzi na Spika wa Bunge kwenye orodha ya vivutio vya Utalii. Naamini wageni wengi wangekuja kushuhudia vivutio hivi viwili.
 
Chezo hili Mbowe analijua..
Mnyika analijua..

Tatizo wafuasi wa chadema ni kama misukule hawawezi kufikiri nje ya box.

Huku kujiamini kwa Ndugai kunaonesha kuna kitu anakijua.
 
Back
Top Bottom