Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai
Job Ndugai alisema hayo alipokuwa akitoa maana ya neno fala bungeni ambapo ilibidi arejee maana hiyo kwa kusoma kupitia kamusi ya Kiswahili ambayo ilitoa maana kuwa fala ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri.
"Kwa neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye tafsiri ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa yule unayemwambia 'Fala' ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula. Ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani mwenzako huwezi kumfanyia hivyo" alisisitiza Job Ndugai
Chanzo: EATV