Spika Ndugai: Lissu hana kibali cha kuishi nje ya nchi, amtaka arudi mara moja Tanzania

Uchambuzi murua sana...gwiji was sheria was chadema tayari kaanza kupiga kelele kuwa kuna mpango was kumvua ubunge. Tayari anajua nini anastahili kwa kiburi na ujuaji wake. Rungu LA Spika limwangukie tu hakuna namna
 
lakini mkuu si inaeleweka hayupo jimboni kwa sababu zipi ?labda madaktari wangesema hali yake kiafya haimruhusu tena ..mi nazani afya yake ni muhim kuliko hizo milion kumi na ngap anazolipwa kila mwezi
Fedha anazolipwa kama mshahara na remuneration zingine zielekekwe kwa wahitaji bado kama nchi tunahitaji fedha kwenye maendeleo
 
Kwa u bush lawyer wangu basi mikutano mitatu itakayo hesabiwa ni toka amekuwa discharged toka hospital ambako bunge lina taarifa zake. Nayo ni last week.
Hivyo mikutano mitatu ni kama hata hudhuria hii January session, April na kikao cha Budget.
Sasa matisho ya nini mbona mbali sana huko?
Lissu anahitaji hii January na February kimwaga ukweli Dunia nzima ijue manyang'au tulio nao na kuita viongozi.
Kisha anarudi tumuandae jinsi ya kuhutubia kule AU au UN maana wakati wa kuirudisha Tanzania katika ramani umekaribia yaani 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala jitihada ziwekwe kuwatafuta waliompiga risasi,watu wanaleta hoja za kishenzi, asingepigwa risasi haya mambi yasingekuwepo walaumiwe hao watu wa jiwe walioyaka kumuua
 
lakini mkuu si inaeleweka hayupo jimboni kwa sababu zipi ?labda madaktari wangesema hali yake kiafya haimruhusu tena ..mi nazani afya yake ni muhim kuliko hizo milion kumi na ngap anazolipwa kila mwezi
Yeye mwenyewe amesema yuko vizuri isipokuwa ana ratiba ya kuzunguka Ulaya
Je hiyo ratiba ameruhusiwa na nani na kwa manufaa ya wananchi wa Singida au Watanzania

Speaker amemruhusu kwamba ratiba yake iko kulingana na kanuni za Bunge?

Ametoka hospitalini je angelikuwa nchini kwa mfano mkoa fulani angeliruhusiwa na kwenda DR Congo au Msumbiji badala ya kwenda kwake. Si ingelishangaza hata uguzaji k?wamba mgonjwa kachanganyikiwa
 
Hawakulifikiria hilo nadhani wangeenda na vifaru kabisa,sasa Leo wako uchi dunia nzima inajua kila kitu,ni heri kumnunua MTU kuliko kumpoteza,mange kapewa chake njaa imetulia,Ishu ya Ben itawasumbua sana hata kuongelewa daily ni saikolojiko torture Kwa chain yote
Badala jitihada ziwekwe kuwatafuta waliompiga risasi,watu wanaleta hoja za kishenzi, asingepigwa risasi haya mambi yasingekuwepo walaumiwe hao watu wa jiwe walioyaka kumuua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu ndugu yangu usirudi nyumbani, ubunge wauchukue tu. Hawa wanataka kuja kukuua. Period! Aibu hawana wala utu hakuna...mashetani tu.
Asirudi na kama Ni ubunge wauchukue tu. Anachofanya katika ziara yake ni muhimu mno. Kama ni kurudi basi arudi 2026.
 
Kama kazi inagharimu maisha iache ipite
 
Hakuna kitu kama hicho inajulikana yuko kwenye matibabu, matibabu na utoro ni vitu viwili.Alisema atarudi lzm hadi pale daktari wake atakapofanya clearance ya mwisho kuwa amepona na mwenye kuthibitisha afya ya MTU ni daktari na sio mwanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wote akiwa hospital sio utoro ndio maana Bunge limendelea kumlipa mshahara wake kamili. Utoro unahesabiwa baada kutoka matibabuni na kuanza ziara za ulaya na America kitu ambacho kinathibitisha mgonjwa ametoka hospital na kuonekana BBC London. Hivyo kwa kanuni za utumishi anapaswa kuripoti kazini au mwajiri wake apewe taarifa rasmi.
P
 
Jamaa wameshaandaa plan B ya kumuua Lissu na sasa wanamlazimisha arudi ili awepo kwenye target zao
 
Hii ya mwisho ya political asylum ndio hakika. Lissu hatakanyaga tena ardhi ya Tanzania. Atakuwa mkimbizi mburuya hadi pale atakapofukiwa mavumbini. Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daktari wake ameshamruhusu kurudi nyumbani au aondoke bila ruhusa ya daktari? Kwanini bunge lisiwasiliane na lissu ama hospitali anayotibiwa ili kujiridhisha kama ameshapona ama laa? Au tatizo ni lissu kwenda uk?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli Mungu hamfichi mnafiki, wauaji wa Lissu tumewajua huu ni mwanzo mtajitaja wote.
 
"Robot la Matope, post: 30097236, member: 283757"]Ibara ya 71 "C" inamkamata Lisu kama atakosa mikutano 3 mfululizo bila Ruhusa ya Spika. Kwa maana hiyo Ubunge wa Lisu upo mikononi mwa spika kama hatakidhi kipengele hiki.
Bandiko #13 JokaKuu ameuliza maswali muhimu sana, utoro wa Lissu unaanza kuesabiwa lini?
Haijulikani kama hadi sasa wakati Lisu alipokuwa akitibiwa kama alikuwa na Ruhusa au ni fadhila na Busara tu za Spika kutokana na upekee wa tukio la Lisu.
Mwandishi wa makala ameshindwa kuelewa kuwa Lissu alikuwa na 'ruhusa' ndiyo maana Mh Spika anamwita na hakuwahi kumfukuza licha ya kutokuwepo
Kwa sasa na kwa matamshi take Lisu anaonekana kapona.
Huyu Thadei Mushi anaelewa maana ya kupona? Mwenye uwezo wa kusema kapona ni Daktari. Mtu akitembea haina maana ni mzima. Sasa jukumu la kuthibitisha na kuthubitishiwa ni kati ya Dr na Spika. Ili Spika aweze kupata taarifa za TL lazima awe na ridhaa( consent) yake. Spika akiomba ridhaa kwa TL tayari anatakiwa aongelee gharama za matibabu. Hili ndilo linaleta ugumu na wanataka kumfukuza kienyeji tu
Lisu kwa sasa kajipangia ratiba ya Shughuli zake njee ya Ratiba ya Bunge. Yaani anafanya shughuli zake binafsi kwa matakwa yake.
JokaKuu kauliza, ratiba ilianza lini? Pili, kujipangia shughuli ni kupi?
Kutembea inaweza kuwa sehemu ya kupima uwezo wake kuhimili mazingira mapya wakati anaendelea na matibabu. Mwandishi anaposema anafanya shughuli zake binafsi, lini alikuwa chini ya uangalizi wa Bunge?
Ingelikuwa bado anaendelea na matibabu busara iliyombeba toka mwanzo ingeweza kuendelea kumbeba sasa. Lisu ameonekana London, Lisu anadai atakwenda Marekani na atakwenda Brussels huko kote si kimatibabu Bali ni kwa Ratiba zake.
Nani ana uthibitisho kuwa kamaliza matibabu? Hivi ikiwa ana appointment kila wiki kumuona Dr wake, atakuwa nje au ndani ya matibabu?
 
Mbona wengine wanakwenda kutibiwa UKIMWI nje, Lissu hakupenda kuwa nje ya nchi na daktari wake hajamruhusu kurudi Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…