Spika Ndugai: Lissu hana kibali cha kuishi nje ya nchi, amtaka arudi mara moja Tanzania

Katika mazingira ambayo Lissu alishambuliwa, akaponea chupu chupu kupoteza maisha, mpaka sasa hakuna aliyekamatwa wala kuhojiwa na vyombo vya dola, sio busara wala hekima kwa kiongozi yoyote wa serikali kupendekeza au kuamrisha Lissu kurudi nchini. Mnamtafutia nini Lissu?
LISSU usirudi mpaka dokta akuambie sasa rudi.. na urudi pale wasiojulikana wakijulikana
tapatalk_1547909900544.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri wa awamu hii hai entertain UPUUZI. Mliweza kumjaza upepo Mbowe alipokiuka masharti ya Mahakama na mlishangilia sana alipokuwa huko Ulaya,kaamkaje na anaendeleaje saiz imekua ni jukum la yy na family yake. Kama mnaona kazi ya mbunge ni kuangaika Ulaya basi muda atakua mwalim mzuri sana.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
mtaumiasana shwain nyie
Screenshot_2019-01-15_191219.jpg
tapatalk_1547881127288.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Ndugai aliugua kidogo tu tukaombwa tumuombee kila wakati tukisistizwa kumuombea, huyu mwingine hata kuumwa haumwi tunaambiwa kumuombea kila siku. Je! Ingekuwa ni wao yamewapata haya Je! ni kweli wangesitishiwa ubunge wao? Sisi watanzania tumeisha fahamu ni nani alitekeleza shambulio dhidi ya lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Busara ya spika alivokuwa kwenye matibabu ilitumika sasa amepona. Sasa kwan ndugai alivopona alibak uko uko ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaomtia kicha lisu kuhusu kuendelea kuzulula Nje bila kibali huku akiwa ameshapona ni wapumbavu hawana akili hata Moja

Ebu jitafakarini wapumbavu nyie kauli ya kumtaka Mhe lisu kurejea nchini imekuja baada ya lisu kupona na kuanza ziara,sasa spika wa bunge amwache tu asimkumbushe majukumu yake na wajibu wake kama mbunge?

Hii kanuni haitungwi Kwa ajili ya lisu isipokuwa ipo siku nyingi sasa ni yeye arudi kuchapa Kazi zake Kwa sababu sasa walishindwa kumwadhibu Kwa sababu alitoka akiwa hoi bila kibali cha spika leo ni mzima arudi kosa la spika lipo wapi?

Mdanganyeni atajikuta yuko Nje ya uwanja kama hatatii ushauri tunaomshauri kurejea nchini ,na wala hoja ya kusema Usalama wake uko mashakani haina mashiko kwani anaomba uraisi kampeni atazifanyia wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli anatakiwa arudi kulitumikia taifa lake.... lakini tukio lake si dogo la kukurupuka tu kurudi kisa kapona wakati waliotaka kumuua hawajakatwa wala tetesi kuwa ni watu gani.
Nadhani ni busara kuangalia usalama wake kwanza kabla ya kurudi nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi binafsi naona Lissu asirudi,, ubunge na uhai, uhai ni kitu muhimu sana, aombe tu hifadhi ya kisiasa ktika nch yoyote had ipite miaka mitano ndio arudi,
Kurudi wala sio ushujaa, nahis wabaya Wake jp hawajulikani, hatujui akirudi Safari hii watamfanyaje
 
Kama kweli SPEAKER atatendea haki wananchi wa Singida na WaTanzania wote ni kusoma sheria ya Bunge na kanuni za Bunge zinazohusu Mbunge kukosa sifa ya kuwa Mbunge.

Fikiria ameitangazia dunia kwamba yuko anadhulura Ulaya na kupiga show kwenye media, kwa nini asirudi nchini halafu atakuwa anaenda clinic kama wengine huko Hospitalini?

Tabia hii itakapoachwa baadae itakuwa ni utaratibu na itakuwa ni rejea.

Nadhani akirudi yeye na dreva wake itakuwa ni fursa hata vyombo anavyotuhumu havipelelezi vitaanzia kwake maana yeye na dreva wana kila kitu kuhusu tukio.

Kama watumishi hewa waliondolewa kwenye payroll kwa nini naye asiwe mtoro kazini kisha atolewe kwenye uwakilishi isitoshe muda umebaki kidogo aweze kuitembelea dunia nzima akisema chochote huko?

Nishauri mamlaka ya speaker ili asiache mwanya wa dhihaka afanye kama sheria na kanuni zinavyosema kwa Mbunge mtoro na kama zimekaa kimya tujue pia.

Nawasilisha
 
Watu wa ufipa mnataka aendelee kuvunja sheria ambazo bunge limezitunga halafu akiadhibiwa mseme anaonewa? Acheni kumuingiza matatizoni mwenwenu. Ina maana hata wewe ukae kazini kwako bila ruhusa kisa ulikuwa unaumwa halafu unaonekana unapiga misele kitaa boss wako akikufukuza kazi utasema kakuonea? Kuweni na fikra pevu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena jambo mkuu inatakiwa tufike mahala tuelewe sio watu wanamtaka arudi wanamipango nae mibaya ila ni kuondoa dhana asije kuvuliwa ubunge kwa kufata sheria ionekane kaonewa watanzania unawaacha tz unaenda kuzurura ulaya kushtaki njoo nchini pambana wapigania uhuru wote hawakukumbilia kwa wazungu walipambana nchini kwao mpaka kikaeleweka mfano Mandela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: e2n
Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa ,

..hii hoja inawahusu wanasheria wetu hapa JF.

..Je, utoro wa TL unaanza kuhesabiwa lini?

..Je, alipokuwa Nairobi alikuwa mtoro?

..Je, alipokuwa Ubelgiji alikuwa mtoro?

..Je,Vikao alivyokosa kuhudhuria akiwa Ubelgiji ilikuwa kwa ruhusa ya Spika?

..Au, utoro wake unaanza kuhesabiwa wakati akizurura Uingereza, na Ubelgiji?

cc Nguruvi3, Zitto
 
Back
Top Bottom