Spika Ndugai afanya tena mabadiliko ya Kamati za Bunge

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865
image.jpeg

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko mengine ya kamati za Bunge kwa kuwahamisha wajumbe kadhaa kutoka kamati moja kwenda nyingine.

Taarifa za mabadiliko hayo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga ambaye aliwatangazia wabunge katika kikao cha jioni.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ambayo ni ya tatu tangu Bunge la Kumi na Moja kuanza, Ezekiel Maige amehamishwa kutoka Nishati na Madini kwenda Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wengine waliohamishiwa PAC ni Allan Kiula kutoka Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Omary Mgumba kutoka Sheria Ndogo, Rhoda Kunchela kutoka Masuala ya Ukimwi na Joseph Kakunda kutoka Kamati ya Uwekezaji.

Wengine waliobadilishwa kamati ni Ahmed Salum aliyetoka PAC kwenda Huduma na Maendeleo ya Jamii, Neema Mgaya kutoka Huduma na Maendeleo ya Jamii kwenda Ardhi, Maliasili na Utalii na Salma Mwassa kutoka Bajeti kwenda Ardhi, Maliasili na Utalii.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wabunge ambao wako kwenye kamati zao ambao watakuwa wajumbe waalikwa katika kamati ya Bajeti ni Andrew Chenge, Joseph Selasini, Dk Dalali Kafumu, Japhet Hasunga, Albert Oboma na Mussa Zungu.

Wabunge wawili, Dk Hadji Mponda na Najma Giga wameondolewa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku wabunge watatu wakiteuliwa kuingia kwenye kamati hiyo ambao ni Asha Juma, Emmanuel Mwakasaka na Augustino Masele.


Chanzo: Mwananchi
 
miezi 7 kamati zimebadilishwa mara 3?! ndugai ana kazi kubwa sana kuwaongoza hawa wabunge.
 
Back
Top Bottom