Spika na Bunge lote lisitishe shughuli zake za kawaida, lijadili mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika na Bunge lote lisitishe shughuli zake za kawaida, lijadili mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by William wa Ukweli, Jun 27, 2012.

 1. W

  William wa Ukweli Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natoa wito kwa wabunge wenye uchungu na taifa hili, kuomba mwongozo wa spika wa kusitisha shughuli za kawaida za bunge ili kujadili mgomo wa madaktari. Hii ni njia muafaka ya kujaribu kutatua mgogoro unaoendelea baina ya serikali 'sikivu' ya CCM na madaktari. Najua hatua hii itapingwa kwa mantiki kuwa, ni kuingilia uhuru wa mahakama, lakini tusisahau 'majuto ni mjukuu'.

  Mahakama ina uhuru wake katika kuendesha kesi zake, hata hivyo suala la muda kwa sasa ni la muhimu sana.

  Nawapa pole wagonjwa wote wanaoendelea kuathirika na mgomo huu, na pia natoa rambirambi zangu kwa wale wote waliopoteza ndugu zao kutokana adha ya mgomo wa madaktari unaoendelea kusambaa kwa kasi sana nchi nzima.

  Wabunge wote nawasihi, tafadhalini sana wekeni pembeni itikadi za vyama vyenu vya siasa kwa mustakabali wa ustawi wa taifa letu.

  Vidumu vyama vyote vya siasa, katika kipindi hiki kigumu tusisahau 'umoja ni nguvu, na utengano ni udhaifu'.
   
Loading...