Spika kificho awadanganya wajumbe wa eu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika kificho awadanganya wajumbe wa eu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, May 14, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  na Mwanne Mashugu, Zanzibar

  SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, amesema tofauti za mitazamo kuhusiana na suala la uhuru wa Zanzibar, limekuwa kikwazo kikubwa na kusababisha kushindwa kufikiwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

  Spika Kificho alisema hayo jana katika kikao cha mazungumzo kilichowakutanisha viongozi wa CCM na ujumbe wa Jumuiya ya Ulaya, ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz, Makao Makuu ya chama hicho, Kisiwandui jana Zanzibar.

  Kificho, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema wakati viongozi wa CCM, wanaamini Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, ndiyo yaliyoleta uhuru wa kweli kwa wananchi wanyonge wa visiwani, huku CUF wakiamini uhuru wa mwaka 1963, ambao CCM wameuona kama ni uhuru bandia katika historia ya Zanzibar.

  Spika Kificho alisema hali hiyo inasababishwa na kutoaminiana na hata kama Serikali ya Umoja wa Kitaifa itafikiwa mawaziri wake watakuwa katika wakati mgumu katika utekelezaji wa majukumu yao.

  Alieleza ugumu wa utekelezaji wa suala hilo, utakuwa hauna tofauti na hali ilivyojitokeza katika serikali ya umoja wa kitaifa ulioafikiwa nchini Kenya, kutokana na kutoaminiana na kuathiri ufanisi wake.

  Mpango wa kuundwa serikali ya mseto Zanzibar, ulikwama baada ya viongozi wa CUF kugoma kuingia katika kura ya maoni kama ilivyokuwa imeamuliwa katika kikao cha Halmasahuri Kuu ya CCM, kilichokutana Butiama chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Rais Amani Abeid Karume.

  Katika mazungumzo hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz, alisema nia ya CCM ni njema, ndiyo maana ikaingia katika mazungumzo na CUF, lakini mpango wa kuundwa serikali ya pamoja umekwamishwa na viongozi wa CUF.

  Aliueleza ujumbe huo wa Jumuiya ya Ulaya, kutokana na uzito wa suala hilo NEC ya CCM iliamua ajenda ya suala hilo iamuliwe kwa kura ya maoni, itakayowashirikisha Wazanzibari wote ili kulinda misingi ya demokrasia na katiba ya nchi.

  Hata hivyo, Ferouz alisema CCM imeridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Magogoni na maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu lakini alisema uvumilivu wa kisiasa lazima uzingatiwe na viongozi wa vyama vyote vya siasa Zanzibar, kwa kuweka masilahi mbele ya umoja wa kitaifa.

  Kiongozi wa ujumbe wa EU, Tim Clarke, alisema ujumbe huo umefika Zanzibar kuangalia ustawi wa demokrasia katika kuelekea uchaguzi mkuu na tayari uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni unaotarajiwa kufanyika Mei 23, mwaka huu.

  Alisema pamoja na kuwa jumuiya hiyo imeamua kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake hapa Zanzibar, lakini alisema wanapenda kuona maendeleo ya demokrasia yanapatikana kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
   
 2. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Junius eleza basi huo udanganyifu upo wapi haPO?
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  "Mpango wa kuundwa serikali ya mseto Zanzibar, ulikwama baada ya viongozi wa CUF kugoma kuingia katika kura ya maoni kama ilivyokuwa imeamuliwa katika kikao cha Halmasahuri Kuu ya CCM, kilichokutana Butiama chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Rais Amani Abeid Karume".

  pakacha,
  Haya mabazungu hapa yalipigwa sijuwi kiingereza kipi kuelezwa ubaradhuli huu. Kificho hapa kaongopa kwa makusudi kwa kusema kuwa mpango huu wa serikali ya mseto umekwama kwa CUF kugomea kura ya maoni kama ilivyoamuliwa na kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM. Pakacha ukweli wa suala hili ndivyo ulivyo?
  Hii halamashauri kuu ya CCM ilihusika vipi katika mchakato wa mazungumzo ya muafaka yaliyowahusu makatibu wakuu wa CUF na CCM, mpaka wapendekeze kura ya maoni jambo ambalo halikuwahi hata siku moja kuwamo katika ajenda ya mazunguzo ya muafaka?
  Halafu Kificho hapa kazidi kujifanya **** na akili tope (au ndo sujuwi ukereketwa tu) mambo ya uhuru na mapinduzi ya tokea siku hizo, yanahusiana na mazungumzo ya muafaka, kuru ya maoni na matatizo ya mfumo mbovu wa uchaguzi tulionao unasababisha matatizo yasiyokuwa ya lazima.
  Anataka mabazungu yale yafahamu kuwa katika mazungumzo yale CUF walisema hawayatambuwi Mapinduzi ya zanzibar na wanatambua uhuru wa 1963 kuwa ndo siku ya ukombozi ndo maana itakuwa tabu kuunda serikali ya pamoja! stupid... akili yake nyeupe kama nywele za kichwa chake, shoti kanichefua leo nimeamka vibaya kwa upuuzi wake.
   
 4. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana junius kwa kuamka vibaya. lakini kama Mheshimiwa kificho ameyasema haya katika mkutano rasmi na ujumbe mzito kutoka nje kama huo wa EU siyo sahihi. CUF hawajapatapo kueleza rasmi kama hawayatambui Mapinduzi ya 1964 na wanatambua uhuru wa 1963. Zilizopo ni hisia za vigogoni tu . sasa kama Kificho ameueleza ujumbe rasmi hisia za vigogoni sio sahihi hata kidogo (kwa mtu wa nafasi kama yake -Spika- katika nchi ya Kidemokrasia) na haikuitendea haki CUF ambayo ina wajumbe kibao pale katika baraza analoliongoza.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  ukizingatia kuwa wakati huu licha ya tafauti za kiitikadi ya vyama vyetu, wazanzibar wanahitaji umoja na kuwa pamoja kuliko walivyowahi kuwa wakati wowote. sasa kauli kama hizi hazina ishara nzuri katika kuelekea huo, hebu na watumie muda huu kuijenga zanzibar ya baadae ambayo ushabiki wa kisisa ufanywe kama wa Yanga na simba, mechi ikimalizika watu wanakuwa wamoja. wafanye just for the future of our children
   
 6. N

  Nampula JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kificho ni spika wa baraza lakini nasema ni spika wa ccm.sasa mkuu junius unadhani ccm wapo kwa ajili ya maslahi ya taifa?tusahau na sidhanii kama hao eu hawaujui huu mchezo wa ccm wanaufahamu sana tu lakini ndio hivyo tena.
   
Loading...