Spika aongezewa ulinzi

kama sms 400 na simu 200 tena za raia wakawaida zinazomtaka spika awajibike zilipelekea spika kuongezewa ulinzi hadi kufikia kubadilisha magari kwa nini haya hayafanyiki kwa viongozi wetu wa kiroho? ambao tumeshuhudia wakipigwa risasi na hatunaye wengine kupatwa na mauti?
serikaki mna masilahi yapi na haya matukio yabayoendelea nchini sans sana haya ya kujeruhiwa na kuuwawa kwa viongozi wa kiroho?

hii inanikumbusha pia kipindi cha nyuma maeneo ya bukombe watu walikuwa wanavamiwa mara kwa mara na majambazi raia wengi sana walijeruhiwa baadhi walipoteza maisha na wengine waliporwa mali zao pia
Tabia hii ilikoma baada ya viongozi wa serikali kuvamiwa na kujeruhiwa serikali ilituma komandoo mmoja tu ambaye ndani ya wiki moja alikuwa amekamata majambazi sugu zaidi ya 30 na wengi wa majambazi walikuwa wanatoka nchi za jirani

serikali mkiamua hata hawa wanaotekeleza haya mashambulizi kwa viongozi wetu wa kiroho Mnaweza kabisa kuwadhiti tatizo ni kwamba bado hamjaamua labda hadi afe waziri ndo mtashituka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…