Spika abariki mbunge kuikashifu CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika abariki mbunge kuikashifu CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mlaizer, Feb 12, 2011.

 1. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  KATIKA hali ya kushangaza jana Spika wa Bunge Anna Makinda alimruhusu Mbunge wa Nkasi, Ally Kessi Mohamed (CCM), kusema kuwa angepata ubunge kwa tiketi ya CHADEMA ingekuwa kashfa kubwa kwake.
  Mbunge huyo alisema hayo bungeni jana alipokuwa akichangia hoja kuhusu mjadala wa hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 10 Novemba mwaka jana.
  Akizungumza awali alianza kwa kuwapongeza wapigakura wa Nkasi na kuweka bayana kwamba alikuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo kwa muda wote aliokuwa huko hakufanikiwa kupata ubunge hadi alipoingia CCM.
  "Nawashukuru wapigakura wa jimbo langu la Nkasi kwa kunichagua mimi; nilikuwa mwana CHADEMA lakini sikufanikiwa kupata ubunge hadi nilipoingia CCM nimeokoka sasa nimepata ubunge nikiwa CCM… ingekua kashfa kubwa kwangu kama ningechaguliwa kuwa mbunge kwa CHADEMA," alisema mbunge huyo aliyetumia zaidi ya dakika 5 kujinasibu badala ya kuzungumza hoja za msingi.
  Baada ya kauli hiyo Mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHadema) aliomba utaratibu wa Spika kuhusu kauli za mbunge huyo kupitia kifungu cha 64 cha Kanuni za Bunge toleo la mwaka 2007 ambapo alimtaka mbunge huyo kuomba radhi ama kufuta kauli yake.
  "Kuhusu utaratibu mheshimiwa Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 64 kifungu kidogo (g) kinasema bila kuathiri masharti ya ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge; Mbunge hatatumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine.
  "…Mheshimiwa Spika CHADEMA ni chama kilichosajiliwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi, ni chama makini chenye watu makini hivyo mchangiaji aliyepita kusema ingekuwa kashfa kubwa kwake ni lugha ya kuudhi namtaka afute kauli yake au aombe radhi au turuhusiwe kusema lugha za maudhi," alisema Mdee.
  Baaada ya kauli hiyo, Spika wa Bunge alimwambia Mdee kuwa yeye ndiye mwenye kuruhusu wabunge kuongea lugha za kuudhi na sio mtu mwingine kisha akamruhusu mchangiaji huyo kuendelea.
  "Mimi ndiye mwenye uwezo wa kuwaruhusu mzungumze lugha za kuudhi siyo mwingine naomba ukae chini mtoa mada endelea," alisema Spika huyo akimweleza Mdee aliyeonyesha kutoridhishwa na majibu hayo kisha mjadala huo uliendelea.
   
 2. F

  Fahari omarsaid Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ww unategemea nini wakati ana makimba katumwa kutetea C hukua
  C hako
  M apema
  au umesahau usemi wa wahenga kunya anye kuku akinya bata kaharisha
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Makinda akili yake kinda pia, dont pay any attention to her, she will feel important, to me, she is useless speaker and servant of corruption.
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Huyu Kigagula Makinda ananichefua na anani-bore stiff.Sura kashetani anawanga! Pambaf kabisa.

  Hivi hakuna kifungu cha kupiga KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA SPIKA?????????????
  Maana huyu mwanamke inaonekana kutaka kulipeleka BUNGE TUSIKOTAKA WATANZANIA. Hivi hajasikia kuwa MUBARAK keshaachia ngazi kwa nguvu ya umma????

  Kauli za mtu kama Makinda ndizo zinazoweza kuchochea NGUVU YA UMMA KUUONDOA UTAWALA WA CCM AMBAO UNAWAKANDAMIZA WATANZANIA NA UPINZANI KWA UJUMLA!!!
   
 5. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu Mama Makinda ameshalifanya Bunge letu kuwa ndio sehemu ya Mipasho:twitch:
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hakika Makinda amechanganyikiwa, akili zake wala hazijakaa sawasawa
   
Loading...