Speed ya JPM ni ya Lockheed (hakamatiki)

Speed ya JPM ni ya Lockheed (hakamatiki)

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
677
KASI YA DKT MAGUFULI NI YA LOCKHEED

Na Elius Ndabila

Mh Dkt John Magufuli ambaye ni mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi speed yake kuelekea uchaguzi wa October 28 mwaka huu ni sawa ndege aina ya LOCKHEED. Ukubwa wa speed hii umesababisha kuwachanganya kabisa wapinzani wake kutoka vyama vingine ambao wamefikia hatua wameanza kukosa pumuzi. Mikutano aliyoifanya Iringa na Mbeya inazidi kuwachanganya zaidi.

Ninafananisha kasi/speed ya JPM na Speed ya ndege aina ya Lockheed kwa kuwa ndege aina ya Lockheed SR-71 maarufu kama "Blackbird" ndiyo ndege inayo kwenda kwa spidi zaidi duniani. Ndege hii ilitengenezwa na kampuni ya kutengeneza ndege nchini Marekani ijulikanayo kama Lockheed Martin kwa ajili ya kazi za kijeshi.

Ndege hiyo imeshikilia rekodi ya kuwa ndege inayo kimbia zaidi duniani ikiipiku rekodi ya ndege iliyokuwa ikijulikana kama YF-12.

Ni ukweli usiopingika kuwa Speed ya JPM inatisha ndio maana Wapinzani wamechanganyikiwa. Rekodi ya kazi za JPM za miaka mitano zinazidi kuwavuruga kwani kila propaganda wanayojaribu kujitengenezea inagonga mwamba. Niwakumbushe matukio machache ambacho ni kiashiria cha Wapinzani kushindwa na speed ya JPM.

Hivi karibuni kiongozi mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Mh Zitto amenukuliwa akisema vyama vya upinzani wanapaswa kuungana ili kuiondoa CCM Madarakani. Mh Zitto alienda mbali kwa kusema kuwa tr tatu watakuwa na jambo kuelekea kuungana na kuikabili CCM. Wakati Zitto akizungumza hayo Mgombea wa CHADEMA TUNDU ANTIPASI Mughwai Lisu yeye akizungumza na vyombo vya habari vya nje alipokuwa akitoa salaam kwenye vyama rafiki alisikika akisema watu wanamkubali pamoja na kuwa anapambana na chama kikubwa Afrika na Dunia. Kwa mantiki hiyo kitendo cha Zitto kuomba kuungana ni kuwa pumuzi imeshakata kwani speed ya CCM ni kubwa. Swali la kujiuliza ni je wakati wanajiandaa kugombea hawakujua kasi ya JPM? Je Kama 2015 waliungana kupambana na JPM akiwa na Speed ya kawaida leo watamuweza akiwakwenye speed ya Lockheed?

Jambo kingine ambalo linaonyesha kuwa speed ya JPM imewashinda ni kuanza kuvichokoza vyombo vya dola ili waseme wanaonewa. Tundu akiwa Nyamongo Tarime alijaribu kutengeneza tukio akijua kabisa kuwa anafanya kosa. Lakini yote alifanya ili kujaribu kutafuta huruma kuwa Polisi wanawafanyia fujo wakati ni wao walishindwa kutii maagizo ya polisi. Ikiwa hilo halitoshi jana Mgombea Mwenza wake naye ametengeneza tukio ili waiambie dunia kuwa wanaonewa. Ni dhahiri kuwa hizi ni mbinu ambazo sinatengenezwa baada ya kuona kasi ya kunadi sera wamezidiwa.

Wakati JPM akinadi sera zake kwa kuwaeleza wananchi mambo aliyofanya kwa miaka mitano na anayotegemea kufanya miaka mitano ijayo wao wanazungumza UHURU NA HAKI. Hawajui kuwa Uhuru na Haki una WAJIBU. Huwezi kupata haki bila kutimiza wajibu. Wanajaribu kuwahadaa watu kuwa Tanzania hakuna Uhuru wakiamini kila mtu mjinga.

Pia wanajaribu kumkosoa JPM kuwa kwa miaka mitano alifanya maendeleo ya vitu na si watu. Duniani kote maendeleo ya vitu ndiyo yanayoleta maendeleo ya watu. Unapojenga barabara unawarahishia watu kusafirisha biashara vizuri. Unaponunua ndege na kujenga viwanja unawasaidia watu waweze kusafirisha bidhaa kwa urahisi na wao kusafiri kufuata huduma zao kwa urahisi. Unapoboresha huduma za afya unataka kuwasaidia watu wawe na afya ili waweze kufanya kazi vizuri.

Unapojenga mradi mkubwa wa Umeme unataka kuwasaidia watu huduma ya umeme kushuka chini, na matokeo ya huduma kushuka chini kunasababisha bidhaa kushuka na watu kuweza kuzipata kwa bei ndogo. Lakini unapojenga treni ya umeme si tu kusaidia watu kusafiri haraka, lakini pia kusafirisha bidhaa na kuondoa maroli barabarani ambayo yanaharibu miundombinu.

Duniani kote maendeleo ya vitu ndiyo kichocheo cha maendeleo ya watu. Kwa tafsiri ya hoja ya upinzani kuwa hakuleta maendeleo ya watu wanataka kusema Serikali ya JPM ingetujaza fedha mifukoni. Hakuna Serikali yenye uwezo huo. Alijaribu kufanya hivyo Gadafi wa Libya lakini aliishiwa kuuawa. Kazi kubwa aliyofanya JPM ni kuweka miundombinu bora na ndiyo kazi tunataka kumpatia tena ili amalize ndoto yake.

Uchaguzi wanashinda kwa facts na si porojo. Aizyl Azlee wa mtandao wa TheNew Forward anasema "Wanasiasa wa Malaysia husema mambo ya kijinga mara nyingi kiasi kwamba hatuwezi hata kuyashika yote wanayoyasema. Kabla hatujamaliza kucheka kwa ujinga mmoja, ujinga mwingine tayari unakuwa umeshasemwa na unasambaa mtandaoni. Ni ujinga mwingi kiasi kwamba hatutaweza kabisa kukumbuka hata nusu tu ya yale tuliyoyacheka".
 
Mageuzi hayawezi kusubiri kila mtu awe tayari kuyapokea ndio yatokee, bali huja angali wengine wakiwa bado kuyapokea kama ambavyo Masiya atarudi duniani na kukuta wengine wakiwa bado hawako tayari kumpokea.
 
Hana jipya, kwa huu upuuzi wa kukatisha masomo ya watoto wetu?
 

Attachments

  • IMG-20200930-WA0006.jpg
    IMG-20200930-WA0006.jpg
    49.4 KB · Views: 5
Mkuu samahani lkn naomba kukuuliza: hivi huwa unapataga wapi mda kuandika ujinga, utopolo na upumbavu wa namna hii? Huko kwenye kata yako bwana mtendaji wa kata hukunako kazi?

Baba wa kujipendekezaaaa

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
 
Acha kumdanganya Mzee wa watu mambo ni moto fire usiku huu kule Moshi kwenye chuo cha Police wameshindwa kuwatoa watu uwanjani wakimsubiri Lisu
Ikipigwa na ile 'one love' ndio wajuba hawatawanyiki kabisaa bila lissu kutoa Neno.
 
Back
Top Bottom