Special Thread: Rwanda General Elections-2017

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,481
Reaction score
37,338
July 31, 2017
Kigali, Rwanda

UCHAGUZI WA RWANDA 2017: Sera za wagombeaji na historia

Mwenyeji wa kipindi Sylvanus Karemera wa RTV/RBA amewakaribisha magwiji Isidore Gahamanyi na Tom Ndahiro kufanya uchambuzi na ufafanuzi kuelekea uchaguzi mkuu Agosti 4, 2017.
Source: RTV
Nini kilichofanya uchaguzi wa Rwanda kufanyika kwa ufanisi na amani miaka iliyopita chini ya utawala wa RPF. Na katika uchaguzi wa mwaka huu tarehe 3-4 Agosti 2017 RPF kuungwa mkono na vyama vinane kupambana na Democratic Green Party of Rwanda (DGPR) katika uchaguzi mkuu. Inakadiriwa wapiga kura kiasi cha milioni 6.8 watapiga kura ktk uchaguzi huo ikiwemo diaspora ambao watapiga kura Agosti 3, 2017.
  1. Mwaka 2003 uchaguzi wa kwanza baada ya mauaji ya kimbari dhini ya Watutsi 1994
  2. Kura ya maoni kwa ajili ya katiba mpya baada ya RPF (Rwandan Patriotic Front) kuchukua uongozi
  3. Baada ya uhuru toka kwa Ubelgiji vyama vilianzishwa kwa misingi ya ukabila
  4. Mapinduzi ya mwaka 1973
  5. Mwaka 1990 RPF (Rwandan Patriotic Front) kuanzisha vita kwa kuivamia Rwanda toka nchini Uganda.
  6. Mwalimu Julius Nyerere anaheshimika nchini Rwanda kwa maono yake juu ya wakoloni kuwagawa wanachi wa nchi za kiafrika kwa makabila na ukanda
  7. Diplomasia na Usalama eneo la Maziwa Makuu ya Afrika na mbali zaidi kimataifa.
  8. Miundo-mbinu ya barabara kuuganisha pande mbalimbali za nchi na usambazaji umeme
  9. Masuala ya kijamii Asilimia 90% ya WanyaRwanda wana bima ya matibabu, elimu kwa wote bila ubaguzi na mazingira mazuri wa kuvutia wawekezaji.
 
July 26, 2017
Rwanda

Mgombea (Umukandida) wa chama cha DGPR (Democratic Green Party of Rwanda), Dr. Frank Habineza kwa nafasi ya uchaguzi wa Urais Agosti 4, 2017 akipanda majukwaa na akizunguka kuuza sera zake katika maeneo mbalimbali ya nchini Rwanda. Anategemewa kutoa upinzani mkali kwa Rais Paul Kagame wa chama tawala cha RPF (Rwandan Patriotic Front).

Source: RTV
 
Democratic Green Party Leader Frank Habineza on [HASHTAG]#1o1rw[/HASHTAG] With Eugene Anangwe

Source: Contact TV Rwanda
 
Hakuna uchaguzi hapo ni kiini macho tu
 
Aug 1, 2017
Kigali, Rwanda

Mgombea Huru wa nafasi ya Urais nchini Rwanda katika uchaguzi wa mkuu Agosti 4, 2017


Mgombea-Huru wa nafasi ya Urais Bw. Philippe Mpayimana nchini Rwanda

Bw. Philippe Mpayimana mwenye umri wa miaka 46 atachuana na wenzake wawili Dk. Frank Habineza wa chama cha DGPR na Paul Kagame wa RPF katika uchaguzi wa Agosti 4, 2017 kwa nafasi ya Urais wa nchi ya Rwanda.

Philippe ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na kwa sasa ni mtunzi wa vitabu ana degree mbili za Masters , hategemewi kuleta ushindani wowote mkali kwa wenzie walioteuliwa kutoka vyama vya DGPR (Democratic Green Party of Rwanda) na RPF (Rwandan Patriotic Front). Katika Vitabu vyake vinne vilivyochapishwa, kimoja kinazungumzia demokrasia na kingine masuala ya ukimbizi.

Bw. Philippe Mpayimana ambaye toka mwaka 1994 aliishi uhamishoni katika nchi za France na Belgium amerejea Rwanda toka uhamishoni mwaka huu 2017 na kujitupa katika kinyanganyiro cha kuwani nafasi ya juu ya uongozi wa kisiasa ya kuwa Rais wa nchi kupitia uchaguzi mkuu, akiwa na ndoto za kuchaguliwa na wananchi.
 
unaenda kwenye mechi mshindi ameshapatikana kabla ya pambano hii hutokea Africa tu.
 
Hayo ni decoy tu wa kuwafanya watu waone kuna uchaguzi huru na haki.
 
Aug 2, 2017
Kigali, Rwanda

RWANDA DECIDES 2017: Analysing the Campaigns during the process
Analyzing presidential candidates in-depth

Source: RTV
 
LEO 04/08/2017 Wananchi wa Rwanda wanapiga kura kumchagua rais mpya wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka saba. Jumla ya wagombea watatu wanawania kiti hicho, rais wa sasa , Paul Kagame anatetea kiti chake kupitia chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) au kwa kifaransa, Front Patriotique Rwandais (FPR).

Wengine ni FRANK HABINEZA kutoka chama cha Democratic Geen Party (DGP) na wà tatu ni Mgombea binafsi, PHILIPPE MPAYIMANA.
UChaguzi huo wenye vituo vya kupigia kura elfu kumi na sita (16,000) unatarajiwa kuanza majira ya saa 1:00 asubuhi hii masaa ya Rwanda au saa 2:00 kwa masaa ya tanzania.

Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa mapema Jumatano ya wiki ikayo kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa kutokana ukweli kwamba Rwanda ni taifa dogo, taifa lenye technolojia ya habari yenye kiwango cha juu kwa ukanda huu wa maziwa makuu na taifa lenye mtandao wa internet yenye kasi sana.
 
Uzuri ni kwamba rais anajulikana hapo wanapoteza muda na gharama za uchaguzi!



"mwanaume mashine"
 
Baada ya kuwaua wapoinzani competent na kuhakikisha ana watu kama Lipumbav, lazima ashinde na uchaguzi uwe wa huru na haki.

Pamoja na kuiongoza Rwanda kwenye mazuri mengi, lakini damu za watu zinamlilia tu. Amani haiji kwa wingi wa fedha ama ukubwa wa madaraka. Kufa ni mara moja na baada ya kufa ni hukumu!
 
Hakuna uchaguzi, ni process ya kumsimika mfalme!
 
He is too inferior and selfish
He does not believe on democracy

Bora hizo pesa za uchaguz zingeenda kupunguza deni la taifa tu kuliko huu uchaguz wa kiini macho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…