SPECIAL THREAD: Kufungwa kwa vituo vya mafuta nchini kwa kutokuwa na mashine za EFD

Uchumi unarudi nyuma usipolipa kodi
Mapato yamepungua Mara dufu.....kodi amezichukua amezichukua zote za nchi hii akijua atavuka lengo! From 1.2T had 700b aibu kubwa! Nchi itamshinda soon atakimbia huyu!! Ameua halmashauri zote na manispaa amekomba mapato yote ameanzisha kodi jengo na viwanja lakini wapi ! Roho yake mbaya na kutotaka ushauri anapeleka nchi kubaya
 
ndo kwa mwaka mzima mkuu kwelii,mil.7 mwaka mzima inamaana wameikosa,kwelii??kwa utetezi huu tutafika kwelii....yaaani mwaka mzima hawana uwezo wa kununua mashine ya mil.7.....nadhani ifike pahala tuondoe kitu inaitwa kubebana wote tukae kwenye mstari.
Ulipaswa uelewe kwanza context wa kile nilichokuwa nikijibu. Sijasema kama milioni 7 kwa mwaka mzima wafanyabiashara wameshindwa kuipata ili kununua hizi mashine. Hoja yangu ililenga kupinga kile kilichoandikwa na niliyekuwa nikimjibu, ambaye alikuwa anajaribu kuonyesha kwamba wauza mafuta wanapata fedha nyingi mno (hivyo ni sawa tu kuuziwa hizo mashine kwa milioni 7). Tumewaambia hizo mashine kwa manufacturer ni dola 500 na hadi kufika hapa zinaweza kugharimu dola 900 hivi kwa kila moja. Sasa kwanini wafanyabiashara wauziwe shilingi milioni 7 (ni deal za watu?).

Wafanyabiashara wanazo hoja nyingi za msingi kwenye suala hili, na ndio maana serikali yenyewe kupitia TRA (wakati wa Kamishina Kadata aliyehamishiwa Ikulu) ilikubali kukaa na wafanyabishara kuzijadili hizo hoja kabla ya kuwalazimisha wafanyabiashara kutumia hizo mashine, na kabla hawajafikia mwafaka Kadata akahamishiwa Ikulu. Sasa wewe nikuulize, kwa mfano, unafahamu kuwa hizo mashine ni kama ATM zikiharibika kidogo muuza mafuta anasimama kuuza mafuta-nani analipia hiyo hasara ambayo muuza mafuta atakuwa hauzi? Supplier ni mmoja tu wa hizo mashine nani atakuwa anazifanyia service katika vituo zaidi ya 1800 vilivyoko nchi nzima?

TRA waliingia mkataba na supplier kabla ya kujadiliana na wauza mafuta kuangalia hizo changamoto, wanachokifanya sasa serikali (TRA) ni kutumia ubabe kwa kuwa supplier anawaijia juu kuhusu makubaliano yaliyomo kwenye huo mkataba! Ndio maana tunawashauri kutojiingiza kwenye mijadala ya mambo msiyoyaelewa sawa sawa!
 
Noted and well explained
 
Na wewe jiulize ni kwanini wenye vituo vya mafuta wanapolipia tu mashine wanaruhusiwa kuuza mafuta bila mashine hizo kufungwa?
Kwa swali lako inaonekana kuna zaidi ya matumizi ya hicho kifaa Namaanisha mapato kwa ununuzi wa kifaa
 
Ningekuwa TRA nisingefungia vituo vya mafuta. Badala yake kila siku ambayo hawakutumia mashine husika, ningewapiga faini ya shilingi laki tatu kila mmoja. Wananchi wengi sana wamepata shida vituo vilipofungwa. Hebu fikiri: Kama kuna wagonjwa mahututi waliokuwa wapelekwe hospitali kwa dharura huenda wamekufa kwa sababu magari ya kubebea wagonjwa yamekosa mafuta. Nchi imekosa mapato mengi. Kuna kodi ya mapato imepotea kwenye hivyo vituo vilivyofungwa. Lakini pia kodi iliyopotea ni nyingi pale ambapo watu walishindwa kufanya biashara kwa vile wasafirishaji wa bidhaa walishindwa kuwapelekea hao wafanyabiashara bidhaa kwa kukosa mafuta. Wenye vituo vya mafuta wangepigwa faini kwa kila siku wanayochelewa, lazima wangefanya bidii sana kununua hizo mashine. Wakiwa wanaendelea na biashara zao, adha yote wananchi waliyopata isingekuwepo na serikali badala ya kukosa mapato ingejiongezea mapato.

Sent from my SM-J120H using JamiiForums mobile app
 
Jiulize ni kiasi gani cha kodi kimepotea hadi waziri anaingilia kati ! Acha kulalama kama unahusika ni bora ukatumbuliwa ! Kama kusema tu watu wanatekeleza basi kusingekuwa n'a haha y'a polisi mtaani
Mfanyabiashara anapopewa leseni, huwa anakubaliana na masharti ya leseni hiyo. Kama jukumu lake ni kuhakikisha anaisaidia Serikali kukusanya mapato, hana budi kufanya hivyo na si hadi afatwe nyumanyuma. Asipotimiza wajibu wake, lazima awajibishwe. Unasikia? Acha kulalamika, timiza wajibu wako, kwako, familia yako, na kwa nchi yako.
 
Kwa kuwa lita zinajulikana wangepigiwa hesabu walipe kisha wao wakusanye kwa wateja.biashara ya mafuta ni uhakika yataisha tu hayaozi yale ila kama kitaalamu haiwezekan basi mi sifanyi kazi tra
Ngoja na mimi nitoe maoni yangu. Unajua kuna watu wanaiba mafuta. Mfano kuna malori yanafoji kuwa yanapeleka mafuta nje ya nchi yaani transit. Hayo hayalipiwi kodi na wakifika njiani wanafungua na kuyauza. Sasa issue ya kufunga machine itaweka kila kitu wazi na Itakuwa pia kugundua kama kituo kiliuza mafuta ya wizi maana extra itaonekana. Pia kuna madereva wa makampuni wanaofoji receipt yaani mtu anaweka mafuta ya elfu kumi halafu anaandika receipt ya laki moja. Hiyo hatakuwepo tena. Yaani haki bini haki
 
Sawa kabisa. MASHINE ZA KUTOLEA RISITI LAZIMA ZIWEPO. Lakini je, wewe huoni kufungia vituo vya mafuta ni kutesa wananchi? Kwa nini wanashindwa kuwapiga tu faini wenye vituo halafu kuwashinikiza kuweka hizo mashine?

Na kwa nini wenye vituo wasipewe fursa ya kuagiza mashine hizo wao wenyewe chini ya usimamizi wa TRA? Je, kuna watu wameshafanya ufisadi katika kuagiza hizo mashine ndio maana bei yake ni kubwa sana?
 
Mfanyabiashara anapopewa leseni, huwa anakubaliana na masharti ya leseni hiyo. Kama jukumu lake ni kuhakikisha anaisaidia Serikali kukusanya mapato, hana budi kufanya hivyo na si hadi afatwe nyumanyuma. Asipotimiza wajibu wake, lazima awajibishwe. Unasikia? Acha kulalamika, timiza wajibu wako, kwako, familia yako, na kwa nchi yako.
Ingekuwa maisha ni simple hivyo basi ingekuwa hakuna haja y'a traffic police kwani kila dereva mwenye leseni y'a udereva anajua sheria zote za barabarani please lets ne realistic
 
Back
Top Bottom