Special kwa wadada: Ushauri mtamu

Special kwa wadada: Ushauri mtamu

Think Hard

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
318
Reaction score
307
SPECIAL KWA WADADAS...Ni ndefu lakini jitahidi kusoma...utajifunza kitu kizuri sana......

Jamani enyi wada nisiwafiche, watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuoneshana fahari, ukoo wa Mume na ukoo wa mke nao wanaoneshana umwamba hawa kwenye Send-off na hawa wanajibu kwenye harusi.
Na ule usiku baada ya reception sijui ndio mnaita hivyo mnaingia kwenye gari kuelekea kwenye fungate. Hapo hata wanakamati huwa wanakimbiana ninyi mkishaondoka kwani shughuli yao imeishia pale. Hata wasimamizi watawasindikiza mpaka chumba mnacholala kisha wanawaacha hapo. Lakini kazi yako ndio inaanzia hapo. Wewe humalizii siku ya harusi. Hapa ndio unaosha make up na kubandua hizo kope
artificial na kucha na kuingia kwenye mapambano kupigania Ndoa yako. Ukweli ni kwamba wanaotarajia NDOA itakushinda ni wengi nikiwemo Mimi, na tunapokupigia simu kuuliza "Mnaendeleaje? " huwa tunatarajia jibu lolote kutoka kwako. Kwa sababu NDOA Inaanza baada ya harusi. Usiingie huko ndani kwenda kucheza.
Naomba nikwambie kauli ngumu na ndio ukweli kwa sababu nakupenda. Hicho cheti ni karatasi tu yenye nembo ya Taifa ili kukutambulisha kisheria kama mke wa Mtu. Shetani hakiogopi wala wanawake wa nje hawakiogopi. Na hizo Pete ni kama urembo vidoleni mwako, usidhani kuwa zimemfunga mume wako kufanya maamuzi magumu ikiwa utamvuruga kichwa.
Ukweli ni kwamba sijaona mwanaume anayeogopa cheti, labda wapo ila Mimi sijaona. Nakushauri binti yangu usikose adabu ukajivunia Pete na cheti. Hata kama mtajenga nyumba kwa majina yenu, mwanaume anapokosa amani anaweza kuacha ghorofa akaenda kupanga chumba kimoja uswahilini. Usidhani wote wanaopaki magari huko kigogo huku wameacha nyumba zao bahari beach, zenye Jacuzzi na wanaenda kuoga kwa ndoo na kopo uswahilini, sio wote wamefungwa na uchawi. Wapo wengi wamekimbia makelele na ugomvi usiokoma.
Mdomo wako unapaswa kuleta faraja kwa Mumeo na sio maumivu ya kupasua moyo wake. Sheria ya maisha ni kuvuna unachopanda na asilimia kubwa ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo yao na kutunga sheria, akitoka huko hata uje na jeshi la malaika wa mbinguni na baragumu hutarudisha nyuma maamuzi atakayofanya. Usijibweteke. Nyumba inajengwa na Mwanamke mwenye akili au kubomolewa na Mwanamke Mpumbavu. Yote yako mikononi mwako. Ukitaka kupendwa pendeka, ukitaka kukalia kaa la moto, jifanye pasua kichwa. Asili ya mwanaume ni games, ukianza kushindana naye na wewe unataka kibesi ligi haitaisha. Ila ukishuka na kukaa nafasi yako utadekezwa kama yai. Namalizia na hili binti yangu usimnange Mumeo, amekuamini mpaka kukufanya mkewe. Anashambuliwa na kila kitu kwenye maisha yake. Hebu msaidie nyumba yake iwe sehemu ya makimbilio. Usimfanye moyo kupasuka kila anapowaza kurudi nyumbani utajitengenezea tabu ambazo kuzituliza itakuwia vigumu.
Hii NDOA ni yenu, usitumie mfumo wa mashost zako kuendeshea nyumba yako, wanaume hawafanani. Ushauri mwingine uishie kwenye magroup usilete nyumbani. Nimekwambia haya ili NDOA yako ikadumu. Zaidi sana katika adhabu zote unazoweza kumpa Mumeo usimnyime tendo la Ndoa. Huo mwili ni mali yake. Hizo moods zako ziishie sebuleni, kule chumbani wasilisha rejesho la siku. Hayo ukiyazingatia duniani utaitwa heri.

Huo ndo ushauri wangu kwenu
 
Thread kama hii imepata replies 8 tu means kwamba kweli waliosemwa wengi wao wana tatizo na kilichosemwa ni ukweli mtupu ndo mana wnaashindwa kuchangia
 
Kuna ukweli mwingine unaingia moja kwa moja. Yaani haina ubishi!! Wengi wetu tumeishia kuguna ,wenye ujumbe waufanyie kazi.
 
Tatizo mafundisho kama haya wanapewa wa upande mmoja tu wakati wa upande wa pili ndo waharibu wa kwanza wa hizi ndoa. Kuweni fair sio mnamtwishwa mwanamke jukumu la kuli ndoa pekeake wakati wako wawili pale.
 
Ingekuwa ndoa ina kanuni namna hii tunge print tukabandika chumbani kwetu ili kila siku tupitie tusisahau! Ila looooooo! Binadamu sisi ni waaina yake, kuna wanawake wanafanya hivyo ila wanapigwa mateke.

Ninachoweza kusema sisi wanawake tusiwe static daima tujitahidi, sio kutaka wenza wetu watuadapt ila tutafute namna ya kuwaadapt wao, na wao watafute namna wa kutuadapt sisi. Sio tukae tu tukingoja yeye ajifunze tunavyo vipenda ila na sisi tujifunze waume wetu wanavyo vipenda.
 
Back
Top Bottom